Idara ya Uhamiaji: Acheni kuchelewesha passports za wananchi nje ya nchi tutawashitaki kwa Rais Magufuli

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Wananchi nje ya nchi wanapply passport mpya mtandaoni, wanalipia hela kila kitu vizuri kabisa lakini mnawacheleweshea kwa visingizio vya eti gharama za diplomatic package.

Acheni habari zenu za diplomatic package, passport za wananchi ni haki za wananchi, zisafirisheni haraka hizo passport ziwafikie wananchi haraka.

Hizi documents ni muhimu kwa ajili ya mipango ya muda mrefu ya uwekezaji na biashara, sasa mnapozichelewesha kwa visingizio vya gharama za diplomatic package hamueleweki.

Wekeni basi hizo gharama za diplomatic pakage au gharama za kusafirisha hizo passports ili watu walipie na mtoe risiti!

Watu nje wanataka kufanya transactions kubwa za pesa, kuchukua credits, na wanahitaji passport unakuta mnazichelewesha hadi miezi mitatu kusudi eti walipie gharama za kuzisafirisha, Mbona hizi gharama hamzisemi katika gharama zenu official?

Nawaomba tu hapo uhamiaji, kuweni transparent. Hii ni serikali ya Magufuli, msimkwamishe, mtajuta!

Safirisheni passports za watu haraka ziwafikie wananchi katika nchi mbalimbali kabla ya Christmas na mwaka mpya ili wananchi warudi nyumbani wakiwa na uhakika wa kuwa salama dhidi ya deadline ya kuexpire la sivyo tutawashitaki kwa Rais Magufuli asiyetaka mambo ya msingi kupigwa danadana.

Kuna watu wameapply passport zamani wanasubirishwa, wengine wanapply ndani ya wiki chache wanaletewa fasta, ina maana hiyo diplomatic package au njia za usafiri zinabagua au kuna watu wanatoa pesa ili zije?

Kama hiyo ndio policy yenu ya kimya kimya basi waambieni watu watoe hiyo pesa waziwazi kwenye mitandao, na risiti mtoe. Msiwacheleweshee watu document hii muhimu!
 
Inawezekana ishu ni transport cost nani anabeba serikali au mwenyepasport.
yaani hata hili linahitaji ukiritimba wa maamuzi ? wambebeshe mwenye passport.Watu serikalini wako so slow kwenye maamuzi.Hilo nalo linataka Raisi magufuli aingilie kati? mtamuua Raisi jamani kwa uchovu wa kazi looo

Yaani digrii zote pale uhamiaji hawajui cha kufanya kwenye hili.?
 
Sidhani kama ni ukiritimba ishu ni nani agharamie,kutuma document nje ni gharama zaidi
 
Sidhani kama ni ukiritimba ishu ni nani agharamie,kutuma document nje ni gharama zaidi
Waweke wazi gharama, ili wakati wa application watu walipe.

Kwa taarifa yako pia, Inaonekana kama kuna gharama mara mbilimbili, Watu wakienda kwenye balozi kupeleka documents huwa wanaambiwa walipie gharama za kusafirisha yaani kutuma document TZ na kisha kutoka TZ kuleta passports Ubalozini katika nchi ambazo watu wapo na watu huwa wanalipa.

Cha ajabu Zikishafika TZ, kuna gharama zisizo rasmi tena watu walewale wanaambiwa watoe ili passports zao ziwahishwe!

Wale wanaotoa pesa mara ya pili zao, passports zao zinaletwa fasta, za wale waliotoa mara moja zinazunguushwa zunguushwa miezi kibao

Kuna mazingira ya rushwa hapo!

Nawaonya uhamiaji, kama hili ni dili la mtu litamtokea puani.

Tumeni paspports za wananchi haraka maisha yaende
 
Sidhani kama ni ukiritimba ishu ni nani agharamie,kutuma document nje ni gharama zaidi
Agharimie mwombaji passport.Apewe gharama za kumpelekea akilipa apelekewe chap chap.Hakuna haja ya malumbano yasiyo na kichwa wala miguu
 
Agharimie mwombaji passport.Apewe gharama za kumpelekea akilipa apelekewe chap chap

It seems something fishy hapo uhamiaji.
1. Ukiwa nje ya nchi ukapeleka midocument yako unalipia gharama extra za kusafirisha documents zako kuja TZ, na passport kutoka TZ kurudi ubalozini na kisha kutoka ubalozini hadi kwenye address unayowapa

Cha ajabu sasa:
Pamoja na ghrama hizi extra unazolipa. Huko Uhamiaji wanazichelewesha hizo passport wakidai utoe tena pesa za kusafirisha. Maana yake mtu anakamuliwa gharama mara mbili, halafu cha ajabu bizi gharama ziko silent hakuna cha receipt wala nini.

Hii double payments isiyo rasmi inayotozwa na watu wa uhamiaji inatoka wapi?

Something smells fishy hapa!
 
Missile of the Nation,
Mbona nchi za wenzetu ziko very clear ukitaka passport ije kwa njia expess unapewa gharama zote ubalozini ukitaka ije kwa njia ya kawaida unapewa gharama hapo hapo ubalozini sielewi kitu yaani ina maana balozi zetu na uhamiaji kila mtu yuko kivyake hawana coordination ya pamoja kwenye hili?
 
Serikali inakosa fursa hizi kujiongezea mapato. Ingeweka option ya fast tracking na ada yake.

Passport ya Marekani, kwa mfano, ukienda kujaza form Post Office. Unaambiwa utatumiwa nyumbani kati ya wiki 4 na 6. Mara nyingi katika wiki 3 unatumiwa nyumbani, kwa njia ya posta.

Ukiwa na haraka nayo, wanaweza kukutumia ndani ya wiki 2 au 3, unalipia zaidi tu ku fast track.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inakosa fursa hizi kujiongezea mapato. Ingeweka option ya fast tracking na ada yake.
Passport ni eneo ambalo ni chimbo la dhahabu.Serikali ingeweza pata mabilioni kwa kutoa passport tu kwa wananchi wake.Mfano serikali ingehamasisha kila raia anayetaka passport apewe watanzania tuko milioni 50.Serikali ingefanikiwa kutoa passport milioni kumi tu kwa bei ya sasa ya shilingi 150,000 ingeingiza kiasi cha shilingi bilioni 1500

Ingeongeza na hizo chaji za kusafirisha passport mtu akilipia tungekuwa na pesa nyingi mno

Serikali iache kuhangaika na vikodi vidogo vidogo vya machinga na mama ntilie .Kwenye eneo la passport kuna pesa nyingi ila serikali imelala
 
yaani hata hili linahitaji ukiritimba wa maamuzi ? wambebeshe mwenye passport.Watu serikalini wako so slow kwenye maamuzi.Hilo nalo linataka Raisi magufuli aingilie kati? mtamuua Raisi jamani kwa uchovu wa kazi looo

Yaani digrii zote pale uhamiaji hawajui cha kufanya kwenye hili.?
Ndio maana kunahitajika mifumo imara na sio rais mkali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Passport ni eneo ambalo ni chimbo la dhahabu.Serikali ingeweza pata mabilioni kwa kutoa passport tu kwa wananchi wake.Mfano serikali ingehamasisha kila raia anayetaka passport apewe watanzania tuko milioni 50.Serikali ingefanikiwa kutoa passport milioni kumi tu kwa bei ya sasa ya shilingi 150,000 ingeingiza kiasi cha shilingi bilioni 1500

Ingeongeza na hizo chaji za kusafirisha passport mtu akilipia tungekuwa na pesa nyingi mno

Serikali iache kuhangaika na vikodi vidogo vidogo vya machinga na mama ntilie .Kwenye eneo la passport kuna pesa nyingi ila serikali imelala
Ingepiga hela za mabaharia wa nchi kavu wote wanaotaka passport bila safari.

Uchumi inao, lakini inaukalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingepiga hela za mabaharia wa nchi kavu wote wanaotaka passport bila safari.

Uchumi inao, lakini inaukalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wengine hutaka passport for prestige tu hata hawasafiri serikali ingehamasisha mfano vyuoni kuwa kila mwanachuo awe na passport fursa zikitoka awe nayo wangechukua wanavyuo kibao tena wakiwa mwaka wa kwanza! serikali ingevuna mipesa hadi basi
 
Back
Top Bottom