ng'adi lawi
JF-Expert Member
- Sep 27, 2014
- 2,956
- 1,114
Idara yetu ya zimamoto na uokoaji inapata shida wakati wa dharura za kuzima mioto katika miji yetu kwa sababu ya udhaifu wa idara ya mipango miji katika halmashauri kuruhusu ujenzi holela. Katika maeneo yaliyopimwa ujenzi wa nyumba ni lazima uwe na kichochoro cha mita moja na nusu ambacho kina mlango au grill unayofunguka. Huu mlango kazi yake ni kuruhusu wazima moto kupita kwa urahisi kuzunguka nyumba wakati wakizima moto.
Hivi sasa katika miji yetu vichochoro vyote vimezibwa na kuwekwa viduka ambavyo vina leseni za halmashauri!!!!!!!!!!!!!
Wakuu wa wilaya na mikoa wanajua tatizo hili? Wakurugenzi wa Halmashauri wanajua tatizo hili? Madiwani wa maeneo husika wanajua tatizo hili? Wenyeviti wa serikali za mitaa wanajua tatizo hili? Bila shaka wanajua ndiyo maana hivi viduka vina lesene! Kama hawajui sababu ya michoro ya hii ya milango midogo kwenye kwenye ramani za nyumba wawaulize wahandisi wao na waanze kuvunja hivi viduka ili kuokoa mali na maisha wakati wa dharura.