Idara ya maji Wilayani Missungwi na maji yao machafu

viva666

Member
Oct 11, 2016
86
125
Habari zenu wapendwa! Itifaki imezingatiwa.

Hivi karibuni nilitembelea moja ya wilaya za jiji la Mwanza iitwayo missungwi.
Tofauti na idara za maji mikoa mingi niliyofika kuwa na usambazaji wa maji safi kabisa ambayo mtu aweza kunywa bila wasi ,hali ni tofauti wilayani hapa kwani maji yanayotoka kwenye bomba ni kituko sana.Maji machafu na hayafai kabisa kwa utumizi wa kibinadamu.

Inasemwa kua maji haya yanatoka ziwani moja kwa moja kwa pump zao yanasambazwa mjini .Sasa swali ni je wao hawajui kama maji yanatakiwa kutibiwa kabla ya kumfikia mwananchi.

Majuzi alikuja waziri wa maji hapa na wakazi wakalalamikia idara hii kuhusu ucheleweshwaji wa kuunganishwa na mtandao wa maji hali wamelipa gharama zote,kama ilivoada awamu hii ni ya kutumbua tamati yake meneja akaondoka .

Lakini naona bado kuna jambo haliko sawa kwa maji haya hayasitahili kulipiwa bill ila bure visimani .

Rejea hapa chini
IMG_20191214_070544.jpeg
IMG_20191214_070538.jpeg
IMG_20191214_070516.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom