Idara ya Maji Mwanza-MWAUWASA: Kukatwa kwa maji siku ya pili leo na hili tatizo la Corona!! Huu ni ukatili dhidi ya binadamu viongozi mko wapi?

Grahamm

Member
Jan 3, 2020
13
18
Jamani enyi Viongozi wa Mamlaka ya Maji Mwanza, Ina maana hamlioni hili? Au majumbani mwenu kuna uhakika wa maji muda wote?

Siku ya pili sasa Mitaa ya Nyakato, National Buzuruga kote hakuna maji na haya ni maeneo ya stand kunakohitajika maji ya uhakika kwa watu kunawa mikono angalau kujikinga na hili janga la CORONA

Viongozi wa Mamlaka hii ni hatari kubwa mno hasa katika kipindi hiki cha janga hili la CORONA, Ni vyema hatua za harka zikachukuliwa otherwise hayo mandoo mliyoagiza watu wayaweke madukani na stand kwenye mabasi yatakuwa ya kazi bure maana leo karibu kila duka unakuta ndoo tupu hazina maji sababu maji yamekatika siku ya pili leo bila hata ya taarifa yoyote toka kwa mamlaka.

Ajabu ni kwamba wakishasoma mita tu hapo hapo unapata taarifa ya deni kwenye meseji, huu uzito wa kutoa taarifa ya kutukatia maji unatoka wapi? kwa nini nguvu ile ile isitumike kuwaambia wananchi tatizo ni nini?

Jitafakarini, Huu ni ukatili dhidi ya binadamu, otherwise inabidi wanamnchi wakanawe ziwani sasa
 
Duh hii ni hatari Sana kwa kweli.. nilidhani Ni kwangu tu. Jana nimerudi kwenye pilika pilika za siku nzima nikijitahidi nisishike uso kwa matumaini nitafika Nyumbani kwangu na kunawa kufungua bomba hola. Nikalazimika kwenda kwa jirani kuomba maji hata kwenye jagi nioshe mikono..

aisee hii nchi ni ya kipekee...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko butimba labda ndiko wanaishi binadamu wa daraja la kwanza. Mitaa aliyosema mtoa mada wao wanaweza kuwa pangu pakavu watumie tu santanaiza kuosha mikono


Sent using Jamii Forums mobile app
Huko alikokutaja ndiko town sasa, Buzuruga ndo mitaa ya karibu na Bugando

Huku tuna hospital ya wilaya na Gereza ila maji 24HRS.
 
Ila mkuu nadhani wana namba zao katika zile msg za madeni wanazotuma ungewapigia kuwafahamisha..
Kulileta huku nikuharibiana ugali nao wana familia mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
Sina nia ya Kuharibia mtu kibarua chake ila ni taarifa tu kwa mamlaka hadi muda huu hakuna maji, taarifa ingetolewa mapema labda tungejiaandaa kwa kukinga maji ya ziada.

Pia nikurekebishe meseji wanazotuma za madeni ni automated hazina namba za kuweza kupiga. Labda kupitia bandiko hili wanaweza kuona na kuchukua hatua, hii ndio nia yangu
 
Lakini kiongozi maji yakikosekana Buzuruga ina maana maeneo ya Nyasaka, kiloleli na maduka tisa haya yote pia yatakuwa hayana maji.

Na mabomba ya huko ndio yanaenda sehemu kubwa sana ya mji, hilo tatizo nadhani ni la vijisehemu sehemu si kote ama umefatilia na kuona ni kote?
 
Huko alikokutaja ndiko town sasa, Buzuruga ndo mitaa ya karibu na Bugando

Huku tuna hospital ya wilaya na Gereza ila maji 24HRS.

Mkuu una roho ngumu, hembu kuwa na roho ya huruma kwa wasukuma wenzako. Huku kwetu tulishasahau hata uwepo wa maji ya idara ya maji. Tunajitwangia tu maji ya kuchimba na magadi kibao life linasonga


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Bugando iko Buzuruga? ama kweli mwanza nitakuwa mgeni mie
Mitaa ya karibu kutoka Buzuruga hadi Bugarika si unaenda kwa miguu tu utafananisha na sisi wa huku kufika tu Mkuyuni kiwandani kijasho hadi kwenye ndevu
 
Lakini kiongozi maji yakikosekana Buzuruga ina maana maeneo ya Nyasaka, kiloleli na maduka tisa haya yote pia yatakuwa hayana maji.
.
Na mabomba ya huko ndio yanaenda sehemu kubwa sana ya mji, hilo tatizo nadhani ni la vijisehemu sehemu si kote ama umefatilia na kuona ni kote?
Siifahamu vizuri mitaa ya Mwanza lakini naona kuna maeneo ameyataja sijui kama ndio hayo hayo unayoyataja wewe.

All in all nyakati Kama hizi sio sahihi kwa mamlaka kukata maji. Kama Kuna tatizo Ni vyema kuwaeleza wateja wao mapema ili waweze kuweka akiba ya maji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom