ndiga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2014
- 582
- 592
WanaJF salaam,
Binafsi ninashukuru jitihada zilizochukuliwa na serikali katika suala zima la kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huu wa corona ikiwa ni pamoja na kufunga shule zote za msingi sekondari na vyuo.
Ni kweli kuwa hawa wanafunzi wanatakiwa waendelee kujifunza wakiwa majumbani kwao lakini siyo kwa njia ambayo imependekezwa na idara ya elimu wilaya ya Kwimba.
Idara ya elimu Kwimba imezitaka shule zote za msingi kutunga mitihani kwa drs la nne na drs la saba kila wiki na kisha kuwapa wanafunzi wa madarasa hayo kupitia kwa w/viti wa vitongoji/ serikali za mitaa .
Baada ya kufanya mitihani hiyo wairudishe kwa walimu kwa ajili ya kusahihisha na kupanga matokeo yatakayokuwa yanatumwa wilayani kila wiki .
Je, hawa watu wamejipanga kupambana na corona au wanampango wa kuwatoa kafara hawa walimu watakaokuwa wanasahihisha hizi karatasi za mitihani na masikini hawa wenyeviti wa vitongoji wa serikali za mitaa wasio na posho za kusambazia mitihani hiyo kwa kila mwanafunzi wa drs iv na vii huku wakijiweka katika mazingira ya kupata corona.
Nawasilisha.