Idara ya Ardhi Jiji la Dodoma, wiki ya 3 hakuna printer wala wino -- kulikoni?

chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
2,829
3,824
Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada.

Nyinyi watu wa ardhi jiji la Dodoma, kiukweli mnatupa tabu wateja wenu, nimefika hapa ofisini kwenu kufuatilia hati yangu nina mwaka wa 2 huu tangu mwaka 2019, hadi leo hati bado sijapata. Leo nimefika hapa asubuhi na mapema saa 12 asubuhi, niliona bora niwahi asubuh na mapema maana kero zenu nazijua, nikaona isiwe tabu bora baridi inipige lakini nijue mchakato wa hati yangu imefika wapi.

Kwa bahati njema, namba ikaitwa nikaingia ndani, nikapewa kikaratasi na madam fulani akaniambia nikachukue faili, nikaona isiwe tabu ngoja niende, dirishani kwenye kale kadirisha kenu ka kuchungulia kana kero pia, uzuri mlikaweka ka bati ili ukigonga basi mhudumu masijala akusikie, pale nimeumiza vidole vyangu kwa kugonga, mwisho nikafanikiwa fail likaletwa, kucheck fail pale pale nilipo ishia mara ya mwisho kuja ndo hapo hapo lika-stuck hadi leo hii,

Kilichonichosha zaidi madam anayeshugulikia hiz plot za nala lugala(na ndiko iliko plot yangu pia)akasema tunatakiwa tuchape fail kwa ajl ya hati yako, ila printer hakuna na wino hakuna! Tumeomba hivi vifaa wiki ya 3 sasa hatujapewa, . Nikamuangalia nikaoshiwa pozi kabisaaaa! Yaani wiki ya 3 jiji la Dodoma ardhi hiyo printer na wino kweli vimeshidikana kuweko ofisini? Au mmeagiza dubai mnasubili ifike bandalinia? Huu ni uzembe wa hali ya juu.

Basi bana ikabidi huyu mhuumu aliyepewa dhamana ya kushugulikia hiz plot za nala, atumie busara kwa kuwa hati yangu imekuwa ni muda mrefu, akaniambia sasa kwa kuwa hapa hatuna printer wala wino, basi itakubidi isubiri hapo nje, tulipeleke hili fail ofisi nyingine waka print huko ila uwe mvumilivu itachukua muda mrefu, nikaishiwa poz kabisaaa.

Basi hapa niko nje muda huu nasubiri huko sijui wapi fail lilikopelekwa ku printiwa na sijui saa ngapi wataniita .
 
Kawaida Sana hiyo kwenye ofisi nyingi za Ardhi za nchi hii. Mie huku niliko hakuna kompyuta, printer, photocopy machine wala wino,na natrajiwa nikusanye Kodi ya pango la Ardhi la kutosha na kuwapa wananchi hatimilki kwa wakati😂maajabu haya, hapo bado sijatatua migogoro ya Ardhi🏃, Tanzania Kama Tanzania.Hii sekta ya Ardhi imeachwa nyuma Sana ingawa inaingiza Pato kubwa kwenye makusanyo ya kodi nchi hii.
 
Wizara ya ardhi na ofisi zake nyingi ni shida bin taaban. Ofisi nyingi hazina wafanya kazi na vifaa vya kutosha. Dodoma jiji uhitaji wa huduma za ardhi ni mkubwa. Tangu walipo timuliwa wafanya kazi wa kujitolea huduma ofisi zai ni tabu, nafuu huwepo kipindi wakipokea wanafunzi wa field.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Vipi ndugu mteja, bado uko kwenye benchi ukisubiri waprint rasimu yako ya hati manake toka umepost thread imepita nusu saa, pole sana kwa usumbufu. Ila waweza ongea na huyo afisa achukue kazi kwenye flash mkaiprint huko mtaan kwenye stationary, ili kuokoa muda,ingawa siyo utaratibu.
 
Vipi ndugu mteja, bado uko kwenye benchi ukisubiri waprint rasimu yako ya hati?manake toka umepost thread imepita nusu saa, pole sana kwa usumbufu. Ila waweza ongea na huyo afisa achukue kazi kwenye flash mkaiprint huko mtaan kwenye stationary, ili kuokoa muda,ingawa siyo utaratibu.
Asante, bado niko kwenye benchi hapa, ngoja nichukue huu ushari. Ngoja niingie nikampe hili wazo huyu afisa ardhi.
 
Inefficiency kama hiyo ipo kila sehemu serikalini. Halafu mtu anashangaa tunakuwaje maskini.
 
Kawaida Sana hiyo kwenye ofisi nyingi za Ardhi za nchi hii. Mie huku niliko hakuna kompyuta, printer, photocopy machine wala wino,na natrajiwa nikusanye Kodi ya pango la Ardhi la kutosha na kuwapa wananchi hatimilki kwa wakati😂maajabu haya, hapo bado sijatatua migogoro ya Ardhi🏃, Tanzania Kama Tanzania.Hii sekta ya Ardhi imeachwa nyuma Sana ingawa inaingiza Pato kubwa kwenye makusanyo ya kodi nchi hii.
Huna laptop?

Printer nunua hata used mzee.

Utafanya kazi katika mazingira magumu kisa serikali haijaleta vifaa?
 
Vp ndugu umeshapata huduma?
nilipata huduma mkuu,tayari nishalipeleka fail leo hii saa 6 kwa commissioner wa ardhi pale karibu maktaba ya mkoa,so wameniambia niende baada ya mwezi mmoja .kwa leo nikaishia hapo.hapa nasubiri kamwezi kapite niwatembelee tena.ila mpaka umeipata hati umepiga safari za kutosha .
 
Huna laptop?

Printer nunua hata used mzee.

Utafanya kazi katika mazingira magumu kisa serikali haijaleta vifaa?
Laptop na printer nililikuwa navyo wakaiba,so saivi nafanya kazi manual,nachapa na kubandika wadaiwa sugu stendi na mitaani😂kazi na iendelee.
 
Back
Top Bottom