Idara ya adhi mwanza na urasimu wa viwanja na rushwa

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
12,013
10,169
Wana JF embu tusaidiane kuleta mabadiliko katika idara hizi za serikali, kuna ndugu yangu anamilki kiwanja cha kupima Buswelu ambacho alikinunua tangu mwaka 2006 na kwa mujibu wa utaratibu wa viwanja vya kupima halmashauri na idara mbalimbali zinatakiwa zilete huduma za msingi kama maji, umeme na barabara lakini mpka sasa haluna hata kilichotekelezwa japokuwa kutokana na shida kuna watu ambao wameanza kujenga bila kujali yote hayo. Kichekesho wiki hii iliyoita wamepita kwenye nyumba zote ambazo zimeezekwa na kuanza kuwaandikia barua wenye majengo kwamba wanawadau kodi ya majengo ilihali hata barabara hwajajenga na hakuna mtu anaeishi kwenye nyumba hizo kwani nyingi zipo zinaendelea na ujenzi. SWALI HAPA NI HIVI: NI HAKI KUMDAI MTU KODI YA MAJENGO WAKATI UMEMUUZI KIWANJA KTK ENEO AMBALO HALINA HUDUMA ZA MSINGI AMBAZO WEWE UNAEDAI NDIO ULITAKIWA UZIWEKE KABLA YA YEYE KUANZA KUJENGA NA MBAYA ZAIDI NYUMBA ZENYEWE ZIPO KATIKA HATUA YA UEZEKAJI? na wakati huohuo kuna kila dalili ya wao watu wa ardhi Mwanza wanauziana viwanja na ndio maana viwanja vingi mpaka sasa havijajengwa na ajbu mpka sasa ni miezi ni miezi 72 (miaka 6) imepita wakati sheria inasema usipojenga kwa miezi 36 unanyang'anywa lakini kwa kuwa ni viwanja vyao hakuna anaetekeleza hilo la kunyang'anya VIWANJA na la kutengeneza VIWANJA badala yake wanakusanya kodi ya majengo yasiokwisha pia maeneo ambayo hata uongozi hakuna kwa kuwa bado ni porini.
 
ashukuru hata amepata hicho kiwanja, miradi ya viwanja elfu 20,000 wanapata wenyewe ardhi na vigogo,na baaada siku mbili tatu watu wa ardhi waviuza kwa bei ya juu
 
Back
Top Bottom