Idara sugu ya serikali iliyoshindikana

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
Idara ya Uhamiaji ipo chini ya wizara ya mambo ya ndani, idara hii ni moja kati ya idara ambazo uwepo wake hauna faida kwa taifa, idara hii imezidiwa na Rushwa hivyo inahatarisha usalama wa nchi. Wageni katika nchi hii ni wengi sana, huku uraiani tunashangaa uwepo wa raia wa kigeni hasa kutoka nchi za Burundi, India, Pakistan , Bangradesh, China, Kenya, Malawi, Rwanda, Congo DRC na Somalia.Kuna baadhi ya wageni ambao ni vigumu kidogo kuwatambua kama wageni kutoka Malawi, Rwanda na Burundi kwa sababu ya sura na kuongea Kiswahili fasaha.

Kwa sasa Raia wa Malawi wamejaaa kila kona wakifanya kazi za ndani, Hotelini, Nyumba za kulala wageni na mama Ntilie. Warundi wamejikita katika maisha ya kawaida na biashara ndogondogo, hawa ni vigumu kuwatambua kwaani wengi wamesoma hapa nchi kuanzia miaka 1980 mpaka 2000 katika shule za serikali na vyuo. Miaka ya 1990 walichaguliwa kujiunga na shule za secondary kutoka makambi yao katika mkoa wa Rukwa kama mishamo na n.k, Ulyankulu Mkoani Tabora. Wengi walifanikiwa kusoma mpaka vyuo vikuu na kupata mkopo wa serikali ya Tanzania.

Binafsi nawafahamu wachache kama uhamiaji wanaweza ku trace kujua walipo wameaajiliwa katika taasisi za serikali; mfano CHIZA CYPRIAN alisoma SUA kwa mkopo 100% kutoka serikali ya Tanzania, Hatangimana, sasa maarufu kwa jina TANGMAN anafanya kazi kwenye NGO. AZMAVETH yupo wizara ya Elimu. Ndayizeye yupo mambo ya ndani na nk.

Wanaokela na kusumbua ni wenye jamii ya kihindi; jana katika pitapita zangu nilipita maeneo ya Masaki Dar katika jengo moja la AMVERTON TOWER chole road, niliwakuta vijana wadogo na wakubwa kma 5 hivi wenye asili ya asia/wahindi wakifanya kazi za kusaidia mafundi, niliwasalimia watanzania walinambia hawajui Kiswahili wa Kiingereza ndiyo tu wametoka kwao huko india.

Nikajiuliza wanawezaje kupata vibari vya kufanya kazi za kawaida wakati watanzania mafundi wanatafuta kazi bila mafanikio? Wale watanzania walinipa jibu kuwa wapo hata hawajui chochote, lkn ndiyo hivyo wameletwa na wenzao. Kwa kifupi raia wenye asili ya ASIA ni wengi sana kwenye viwanda mahotel na makampuni ya ujenzi. Je Idara ya UHAMIAJI inatimiza wajibu?

Utendaji wa jeshi la POLISI, MAHAKAMA, TAKUKURU unafahamika sina haja ya kueleza kwa sababu wengi tunajua kuwa usiombe ukapata kesi ukapelekwa POLISI hutatka bila pesa, mahakama usiseme, TAKUKURU wameshindwa kufanya hizi hizi taasisi zote kutenda haki.
 
Back
Top Bottom