Idara nyingi Tanzania haziko tayari kikazi au wanadharau majukumu yao

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,750
4,958
Inasikitisha kuona kuwa Idara zetu nyeti haziko tayari katika kazi zao, na ndio maana tunaona wanavyo litia aibu Taifa wakati huu wa kifo na mazishi ya Raisi wetu mpendwa.

1. IKULU na Idara zote zinazohusika na Raisi wa nchi, hawakuwa sawa na madhubuti tokea Raisi aanze kuuguwa, si ajabu hata walishindwa kumuuguza Raisi kwa wakati muafaka. Hili linahitaji Uchunguzi wa kina na iwapo kutapatikana dosari zozote basi sheria ichukue mkondo

2. Idara Husika zingechukua hatua zilizopangwa vizuri kuwajuza wananchi kuwa Raisi anauugua, ili watu wangekuwa wanafuatilia hali ya kiongozi wao. Tanzania kama dola tumepata aibu sana kwa kigeugeu hichi kilicholetwa na unprofessionalism ya wahusika. HAPA PANAHITAJIKA KUBADILISHWA NA WATU MAKINI KUWEKWA

3. Wakalimani kwenye mazishi, Hawa wametutia aibu sana. Ninashauri Boss wa hawa wakalimani ATUMBULIWE HARAKA SANA, huyusi ajabu amelitia janga Taifa pahali pengi. Hawa wakalimani sijui wamepewa hii kazi kiNDUGU au Kikabila. Tokea Jana najiuliza hivi hawa ndio waliokuwa wanawatafsiria mazungumzo Raisi na Mawaziri katika mikutano na viongozi wa njee au Mashirika yanayokuja kuwekeza, kama ni hivyo basi mambo mengi yameenda MRAMBA. HATUA STAHIKI ICHUKULIWE

4. Mheshimiwa Waziri Kabudi, kama MC wa tukio la Jana, jee alikaa na wahusika wote hata hawa wakalimani na wakafanya mazoezi ya hii shughuli kubwa na muhimu kwa TAIFA, au kama kawaida ya viongozi wetu, watakuwa wamekurupuka papo hapo na kumparamia mkalimani kwa matusi na vitisho, Huku kosa ni la kwao. Sijui Marehemu Raisi alijisikiaje kwenye JENEZA, nadhani alipiga kelele nyingi za SAMIA TUMBUWA HAO WOTE NA HATA HUYO PROFESSOR JALALANI, lakini maskini sauti yake inasikika peponi na haisikiki duniani tena.
 
umeanza na idara nyingi za serikali kumbe ulimaanisha watu wachache tu wa Ikulu, kimsingi watanzania wanafanya kazi sana tena kwenye mazingira magumu hawana mshahara ulioongezeka kwa miaka sita sasa kwahiyo unapo generalize huwatendei haki, sisi tuna ndugu zetu huko wanapiga kazi kama mchwa ukiwauliza mbona hamuachi na hali yenyewe ilivyongumu wanakwambia wanafanya kwaajili ya uzalendo kwa nchi yao.
 
Kila mtu alikuwa kashamchoka jiwa ...

Ndio maana wakaamua kukaa kimya mpaka sir God amchukue tu
 
Mkalimani anaachakutafasiri maneno jwa usahihi badala yake anaweka maneno ya kwake mwenyewe hii ni aibu kubwa kama Taifa ambalo tunajinasibu ni waasisi na wataalamu wa kiswahili fasaha duniani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom