Idara gani za serikali/binafsi zinaruhusiwa kutumia dola?

Mbona nakumbuka mama Zakia Meghji wakati huo akiwa waziri wa fwedha aliwahi kupiga marufuku wafanyabiashara wa Tanzania kuweka bei zao kwa dollar. Lakini kama kawaida matamko ya viongozi wa nchi hii huwa yanasahaulika na kupuuzwa kabla hayajatamkwa!
 
Serikali isilifumbie macho suala la matumizi ya dola nchini mwetu. Nchi za wenzetu ukiwa na hela zako za kigeni mahali pekee pa kubadilishia ni benki tu, mfano dhahiri ni china, kule hakuna mzaha kila kitu ni mwendo wa fedha yao RMB.

Serikali ipi?, ipo?
 
QUOTE=FaizaFoxy

Kama nimekusoma vizuri, unamaanisha serikali iendelee kukaa pembeni ishuhudie vurugu zote kwenye uchumi, isubili mambo yatarekebika yenyewe!! Una akili nyingi sana kupitiliza
 
Niliuliza mwaka jana juu ya tatizo ka uchumi wetu hasa ni nini? Majuzi nimemwagiza ndugu yangu aniangalizie vibali na vitu fulani hapo dar. Amekuja na kunipa quotes jatika dola. Nikauliza kwa hela yetu ni kiasi gani hakuweza kukumbuka mara moja.

Nikawa nafuatilia malipo ya mwingine hapo Kampala University. Original quote was in Tanzanian Shillings but when the time came to make payments akatakiwa alipe kwa dola kiasi ambacho hakikulingana kabisa na ile hela ya madafu.

Kuna tatizo gani la kutumia shilingi? Kama dola inaakisi haki yetu ya kiuchumi why not peg our money to the dollar? Au tuamue tu kuwa dola ni legal tender kwa malipo yote nchini na mahali popote. Tunaweza hata kuamua kuita shilingi yetu "dola" kama itatufanya tujisikie vizuri.

Otherwise, are we screwed or what!?

Enzi zile aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakhia Hamdani Meghji, alipiga marufuku matumizi ya dola nchini, siku hizi kuna hata shule ya msingi inalipisha ada kwa dola kisa inafundishia kwa Kiingereza!
 
Toka lini dollar haijawa "legal tender"? au bado uko enzi zile?

tunaposema tz shilling is a a legal tender maana yake ni kwamba the currency shall be accepted in settling debts..sasa inakuwaje unaingia hotelini unatoa tz shilling inakataliwa?kuna tatizo hapa.
 
Hivi tukianza kuhamasisha watu wakatae kutumia dola uraiani na kulazimisha shilingi kutakuwa na madhara gani au itakuwa ndio uchochezi wenyewe?
 
Back
Top Bottom