Idara gani za serikali/binafsi zinaruhusiwa kutumia dola?

niliuliza mwaka jana juu ya tatizo ka uchumi wetu hasa ni nini? Majuzi nimemwagiza ndugu yangu aniangalizie vibali na vitu fulani hapo dar. Amekuja na kunipa quotes jatika dola. Nikauliza kwa hela yetu ni kiasi gani hakuweza kukumbuka mara moja.

Nikawa nafuatilia malipo ya mwingine hapo kampala university. Original quote was in tanzanian shillings but when the time came to make payments akatakiwa alipe kwa dola kiasi ambacho hakikulingana kabisa na ile hela ya madafu.

Kuna tatizo gani la kutumia shilingi? Kama dola inaakisi haki yetu ya kiuchumi why not peg our money to the dollar? Au tuamue tu kuwa dola ni legal tender kwa malipo yote nchini na mahali popote. Tunaweza hata kuamua kuita shilingi yetu "dola" kama itatufanya tujisikie vizuri.

Otherwise, are we screwed or what!?

tatizo kubwa ni sisi wenyewe kwani kila idara tupo watanzania wenyewe,lakini tunaweza endapo kati ya mabo mengine pia serikali yetu iamue kuwa kila mwenye huduma au bidhaa apange bei zake ktk tshs. Ili yule anayekuja na dola atafute madafu kwanza ndipo apate huduma au bidhaa,vinginevyo kusneee mfumuko wa bei nsasa ni zaidi ya 30%
 
wakuu ukienda mbuga za wanyama wageni wanalipa kwa dola ila wa east african wanalipa kwa shilingi. nadhani hiyo lipa lipa kwa dola hasa walengwa ni wageni na si waTz, siunajua pale BOT wanataka kuongeza stock ya dola? Anyway kwa waTz kulipa kwa dola is not fare at all.
 
Inawezekana kuwa hii ni mbinu ya watu kujitajirisha? Wanakusanya ada kwa dola lakini wanapeleka hazina shilingi na ile tofauti wanaerka kibindoni? Mbona ukija uongozi kusafisha itakuwa vurugu!?
 
Sio hapo tu kampala university;kuna mauniversity kibao na taasisi yanatoza dola ukitaka kufanya malipo. SIJUI HII MIBUNGE VIJANA INAFANYA NN KULE BUNGENI?
 
Huu ni mjadala mrefu na mzuri sana, ni kweli suala hilo ni tatizo ila natumai humu kuna wachumi wengi tu, lakini chukua katika hali ya kawaida kabisa kama wewe ni mfanya biashara na unafanya importation ya product zako na kuja kuziuza Tanzania utakuwa ni kichaa kama utaendelea kungangania kutoza bei kwa Tshs ilhali thamani ya Tshs kila siku inaporomoka, huwezi ku set price ya faida hata siku moja, na vivyo vivyo watu wa maofisi dar hapo wanatoza kwa Dollar kuepuka kupata hasara, Tsh is not stable guys kwa hiyo laztima wafanya biashara wajaribu ku play in a safe side.
Sio kwamba natetea hali hii inayoendelea nchini ila nimesimama kama mfanya biashara na kutoa logic ya kawaida kabisa, kama Tsh ingekuwa stable usingeona watu wanasumbuka hata kidogo.

Kwa hili ilivyo sasa bado hatujafikia mahala pa kusema tuifute Tshs ila serikali irekebishe mambo kuna mambo mengi sana yanayosababisha Tshs kuendelea kushuka thamani kwa hiyo wahusika ni lazima wawajibike.

Kama tukiamua kuifanya dollar kuwa curency yetu kuna faida nyingi kuliko hasara, ila hii nikama Tshs itafutwa jambo ambalo siliteemei ila ukichukulia mfano wa Zimbabwe ambayo kwa sasa haina Currency yake yaani hawana tena Zimm Dolar na wanatumia US Dollar pamoja na South African Rand kwa sasa uchumi wao umeanza kuimarika sana, Zimbabwe ya sasa si ile tena ya miaka 5 ama 6 iliyopita.

Ni mambo mengi ningeweza kuyazungumza ila nisiwachoshe kwa maneno mengi, niwape nafasi wengine pia.

Am stand to be corrected.
 
Mi nakwambia nchi hii unaweza kutamani uhame.. Mi mwenyewe miaka mitano iliyopita ofisi niliyokuwapo tulikuwa tukiuza vifaa kwa dola. Tunaangalia rate ya siku hiyo mtu analipa madafu.
Kuna dada mmoja maarufu alinunua vitu vya dola 180,akatoa dola 200,tukaangalia rate,tukapiga hesabu,chenji tukamrudishia madafu. Akasema mi nimewapa mnyamwezi,nyie mnanirudishia hizi! Haya bwana!
 
Mwanakijiji, kuna pande tatu; serikali, mfanyabiashara na mnunuaji. Katika sheria za nchi, hutakiwi kushindwa kufanya malipo yoyote kwa kutumia shilingi ya tanzania, na hilo ndilo serikali inashindwa kulisimamia. Kwa mfano, kwenye shipping lines zote hapa tanzania kama CMA CGM, Maersk nk hawapokei TZS japo kwenye invoice huwa wanaonyesha usd equivalent. Hii ni kosa sana na serikali imelala hapo.

Upande wa pili ni Mfanyabiashara, huyu huwa ananunua bidhaa kwa USD wakati mwingi, sasa kutokana na inflation rate ya Tanzania ambayo nasikia imefika 19%, ni vigumu kuacha kuweka neno usd. ila pia anatakiwa aweze kutoa TZS equivalent kwani anafanya biashara ndani ya Tanzania.

Upande wa tatu ni wa Mwananchi, kwa sehemu kubwa anaonewa hasa serikali inaposhindwa kusimamia malipo ya TZS.


Kuna mambo mengi ambayo serikali inashindwa kusimamia hata ukiangalia bandari yetu pamoja na TICTS wote wanadai USD. Hii inasababisha demand ya USD kuwa kubwa.

Nawasilisha
 
Mkuu hilo ni Tatizo kuubwa sana, nikiwa nje ya nchi nikatuma fedha Tanzania in terms of Dola mtu anayekwenda kuchukua anapewa exchange rate ya 1400, ila mtu akiniwekea fedha kwenye account huko Tanzania, mimi nikachukua huku kwa visa card exchange rate 1650. Nadhani hapo unapata Picha kwa nini watu wanapenda malipo kwa Dola. Can you imagine naibiwa Tshs 250/= kwa kila dola ninayotuma Nyumbani?
 
Sasa upinzani uko upande gani katika issue hii? Je mwananchi wa kawaida anaathirika vipi na dollarization of our economy.?
 
Niliuliza mwaka jana juu ya tatizo ka uchumi wetu hasa ni nini? Majuzi nimemwagiza ndugu yangu aniangalizie vibali na vitu fulani hapo dar. Amekuja na kunipa quotes jatika dola. Nikauliza kwa hela yetu ni kiasi gani hakuweza kukumbuka mara moja.

Nikawa nafuatilia malipo ya mwingine hapo Kampala University. Original quote was in Tanzanian Shillings but when the time came to make payments akatakiwa alipe kwa dola kiasi ambacho hakikulingana kabisa na ile hela ya madafu.

Kuna tatizo gani la kutumia shilingi? Kama dola inaakisi haki yetu ya kiuchumi why not peg our money to the dollar? Au tuamue tu kuwa dola ni legal tender kwa malipo yote nchini na mahali popote. Tunaweza hata kuamua kuita shilingi yetu "dola" kama itatufanya tujisikie vizuri.

Otherwise, are we screwed or what!?

I believe we are screaming while being screwed.
 
Toka lini dollar haijawa "legal tender"? au bado uko enzi zile?


Kwa kukusaidia tu a US dollar is a legal tender issued by the US government to be used kama pesa ya kubalishana katika soko la marekani. Tanzania legal tender currency is Tanzania Shillings. Sasa ni aibu tukawa tumebadilisha currency yetu kuwa us dollar wakati sisi watanzania. Kuna mdau mmoja hapo amesema kuna faida za kutumia US dollar nchini ila hajaoanisha au kutufafanulia zipi? Labda tumuulize supply ya US dollar itawafikia hadi wanavijiji kule chamwino au kwengineko?

Labda tuzungumzie hasara za dollar kwanza currency yetu itakufa na matokeo tutakuwa hatuna sarafu. Pili tutachangia kwa kiwango kikubwa mfumuko wa bei kwani us dollar thamani yake inategemeana na uimara wa uchumi marekani. Na kwa mazingira hayo marekani uchumi ukiyumba gharama za maisha tanzania zinapanda. Tatu value ya currency yetu inaunganishwa na East African Shillings je tutaiunganisha kama US dollar or what? Kuna kikwazo cha mfumo wa fedha.

Nitaendelea baadae.
 
Serikali isilifumbie macho suala la matumizi ya dola nchini mwetu. Nchi za wenzetu ukiwa na hela zako za kigeni mahali pekee pa kubadilishia ni benki tu, mfano dhahiri ni china, kule hakuna mzaha kila kitu ni mwendo wa fedha yao RMB.
 
Sasa upinzani uko upande gani katika issue hii?
Mwanakijiji, does it really matter Upinzani uko upande gani katika huu mfumo?
Je mwananchi wa kawaida anaathirika vipi na dollarization of our economy.?
Who really cares mwananchi anavyoathirika vipi katika huu mfumo tulio nao?

Mwanakijiji, ninao ndugu zangu na marafiki zangu wanaoniona kama mwendawazimu kwa msimamo wangu dhidi ya serikali hii ya CCM mapaka imefikia mahali wengine hata hatuongei. Yapo mambo yanayofanyika ndani ya taifa hili ambayo athari zake ni kubwa na za hatari lakini hao hao waathirika watakuona wewe unayelalamika kama mtu wa vurugu.

Kuhusiana na matumizi ya dollar ukweli ni kuwa tunaelekea pabaya na tusipoangalia utumwa unabisha hodi na sisi kama mazezeta tunaufungulia mlango bila wasi wasi. Kuna wajanja wanazidi kunufaika na muda si mrefu machungu ya hii hali yataanza kuchoma na by the time tunagutuka tutakuta tumepoteza hata kile kidogo tulichokuwa nacho.
 
Wana JF
Nimekwisha sema tuanzishe occupy Magogoni kuanzia tarehe 1.2.2012. Marehemu Nyerere aliwahi kusema " Serikali ambayo ni Corrupt haiwezi kukusanya kodi". Huo ndio ukweli huu uholela wa kuifanya Usd kuwa legal tender hapa Tanzania ni matokeo ya kutokuwepo kwa Serikali. Waliosema kwamba Ikulu ilikwisha binafsishwa kwa Rostam wako sahihi. Bila kuwepo na Benki kuu thabiti inayosimamia vizuri maswala ya fedha then hatuna haja ya kuendelea kutumia Tshs. Kama sarafu. Nyumba zilizojengwa na pesa chafu na hata na mifuko ya akiba Kama PPF, NSSF na kadhalika yanatoza kodi kwa kutumia Usd. For your information the lowest going Market rate is Usd 10 per square metre. Serikali ya CCM ilifuta Rent Restriction Act ya mwaka 1974 Kama nimekosea nisahihishwe. Kama Serikali ikikomaa na kukusanya hata 10% ya hizo kodi za ajabu wanazolipa wapangaji Leo hii tusingekuwa tunasena kila siku Serikali ni masikini this country is damply rich. Ukipanua tax base na kukapcha Watz wote hakuna haja ya Jakaya Kikwete(nampatia jina jipya: Juha Kalulu) kusafiri mara 300 kuuza sura ughaibuni akiomba. El Bashir Rais wa Sudan hutoka nje ya nchi yake mara moja au mbili kwa mwaka na Sudan sio ombaomba. Tumellogwa na aliyetuloga kafa. Kuvaa mapete makubwa na hirizi haitutoi .
 
US$ ni legal tender duniani na si US pekee.

Bado mnaishi dunia ya kale. Dunia nzima watu wana trade na fedha za kigeni, nyie mnaona ajabu? soko huria kwa maana ikiwa unahisi fedha inashuka thamani unawekeza kwenye ambayo una uhakika haishuki thamani.

Huwa mnatafuta vya kusema na kukosoa lakini hamvipati.

FF Nadhani kuna mambo mengi hapa unamiss na kama ungekuwa Banker ungekuwa unaelewa watu wanazungumzia kitu gani!

Suala hapa siyo kuipinga bali hatuna utaratibu mzuri katika hii mbio ya shilingi yetu na na dola na hakuna udhibiti madhubuti ambao umefanywa na serikali kwa nia makini ya kuilinda shilingi na matokeo yake tunaburuzwa na fedha nyingi za kigeni na siyo dola tu ni kwamba shilingi ya yetu haina thamani na kama hauamini nakupa mpaka mwezi wa nane dola itakuwa imefikia 2200 na hata zaidi na nina hakika na hili maana hakuna longterm plan za kuidhibiti dola dhidi ya shilingi bali wafanya short term plan ambayo tunaona kama dola imeshuka vile lakini siyo kweli.
 
US$ ni legal tender duniani na si US pekee.

Bado mnaishi dunia ya kale. Dunia nzima watu wana trade na fedha za kigeni, nyie mnaona ajabu? soko huria kwa maana ikiwa unahisi fedha inashuka thamani unawekeza kwenye ambayo una uhakika haishuki thamani.

Huwa mnatafuta vya kusema na kukosoa lakini hamvipati.

huna hoja point yako ipo kwenye red, hivyo ndio vitu ulivyonavyo kichwani
na jinsi nyie mlivyo huwezi kuiona hoja inayojadiliwa tayari unanegativity so just keep quite sio lazima uchangie uwaonyeshe watu ufinyu wako wa kufikiri
 
Nafikiri tunaendeshana kwa utaalamu wa siasa kuliko utaalamu wa kitu kingine chochote. Sheria zipo ila hazisimamiwi wala kufuatwa. Wale wenye kuzisimamia wako busy na kukua kisiasa kuliko kufanya kazi za kitaalamu.
Tunatumia dola kwa matumizi ya ndani kwani Tanzania imekuwa USA au Zimbabwe???
 
Back
Top Bottom