kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,301
- 12,600
Matokeo ya Sensa 2022 inaonyesha kuwa idadi ya watu wa Zanzibar ni 3.06% tu ya watu wote wa Tanzania. Idadi hii ni ndogo sana kulinganisha na idadi ya watu kwenye baadhi ya mikoa ya bara.
Takwimu hizi zinaonyesha namna muundo wa serikali yetu unavyotakiwa kubadilika kuwa wa kimajimbo ili kuharakisha maendeleo ya watu wote wa tanzania kwa usawa. Zanzibar ina watu wachache lakini maendeleo yake yanatiliwa mkazo sana kwasababu wa serikali inayoweza kuzichokonoa rasilimali zote zilizomo ndani ya Zanzibar na kuzitumia kikamilifu kwa manufaa ya wakazi wake.
Kama nchi yote itaendeshwa kwa majimbo idadi ya watu katika kila jimbo itazingatiwa kwa usawa na rasilimali zote zilizomo kwenye jimbo zitatumika kikamilifu kwakuwa zitahitajika sana kuendesha jimbo pamoja na serikali kuu.
Tuingawanye nchi kwenye majimbo ambayo yatazingatia idadi ya watu, mchanganyiko wa makabila, dini na rasilimali zitakazokuwemo ndani ya jimbo. Faida yake kuu ni kuwa kutakuwemo na uwajibikaji mkubwa wa watu ndani ya jimbo, serikali itakuwa karibu zaidi na watu wake, mila na desturi kwenye jimbo zitakaribiana kama sio kufanana, majimbo yataendelezwa, viongozi watatokana na watu wenyewe ndani ya jimbo na majimbo kushindana kwa maendeleo.
Hasara zake ni pamoja na majimbo kuweza kuingiwa na ulevi wa kutaka kujitenda kama ilivyo kwa Tigrae kule Ethiopia, lakini hii ni ndogo sana.