Landson Tz
JF-Expert Member
- May 8, 2011
- 295
- 221
Idadi ya watu maskini nchini inaongezeka mwaka hadi mwaka. Takwimu zinazotolewa na wataalamu wetu zinaonyesha wazi kuwa idadi ya watu maskini inaongezeka japokuwa ukijikita kwenye asilimia utaona kama umaskini unapungua.
Kutokana ukuaji mkubwa wa idadi ya watu (hadi 3% kwa mwaka) ambao hauendani na sera madhubuti za kuondoa na kudhibiti umaskini, idadi ya watu wanasota kwenye dimbwi la umaskini iaongezeka badala ya kupungua.
Utafiti unaofanywa na serikali kupitia NBS kila baada ya miaka mitano kwa kutumia asilimia unanyesha kuwa umaskini unapungua japo kwa spidi ndogo sana. Kwa mfano: 1991/92 (39%), 2000/01 (36%), 2007 (34.4%), 2011/12 (28.2%) na 2017/18 (26.4%)
Ukitumia tafiti hizo hizo ila ukaangalia idadi ya watu wanaoishi chini msitari wa umaskini (poverty line)
utagundua kuwa idadi ya watu maskini inaongezeka hivyo kwenda kinyume na asilimia ambazo mara nyingi wataalam wetu hupenda kuzitumia. Angalia table hii hapa chini
Tanzania ilikuwa na watu maskini 10,514,867 mwaka 1992, ila mwaka 2018 watu maskini waliongezeka na kufikia 14,866,748.
Kwa takwimu hizi, takwimu zinatudanganya au tunajidanga?
Landson Tanzania

MWAKA | POPULATION | % YA WATU MASKINI | IDADI YA WATU MASKINI |
1991/92 | 26,961,197 | 39.00% | 10,514,867 |
2000/01 | 35,334,788 | 36.00% | 12,720,524 |
2007 | 40,681,404 | 34.40% | 13,994,403 |
2011/12 | 47,053,030 | 28.20% | 13,268,954 |
2017/18 | 56,313,438 | 26.40% | 14,866,748 |