Idadi ya watoto wanaozaliwa kwenye kambi za wakimbizi yahatarisha usalama wa nchi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Picha
ZAIDI ya watoto 600 wanazaliwa kila mwezi kwenye makambi ya wakimbizi wa Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) yaliyopo mkoani Kigoma.

Hali hiyo imetia hofu wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa Kigoma, ambao wameeleza kutishwa na kasi kubwa ya kuzaliana kwa wakimbizi hao. Hivyo, wameitaka serikali kuchukua hatua kukabiliana na hali hiyo.

Wajumbe hao walitoa kauli hiyo kwenye kikao cha siku moja cha kawaida cha halmashauri hiyo. Walisema kuwa kuendelea kuzaliana holela kwa wakimbizi hao, kutakuwa na madhara makubwa siku zijazo kwa nchi, ikiwemo baadhi ya wakimbizi hao kudai taifa lao ndani ya Tanzania.

Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwanko alisema ametembelea baadhi ya kambi za wakimbizi mkoani Kigoma na takwimu ya watoto 600 wanaozaliwa kila mwezi kwenye makambi hayo ni kubwa sana. Nsanzugwanko alisema kama kambi moja, inaweza kuwa na watoto 600 wanaozaliwa, inakuwaje ukijumlisha kambi zote na kwa mwaka mmoja.

Alisema idadi hiyo ni kubwa na isipowekwa mkakati sasa hivi, athari za baadaye ni kubwa.

Alitaja athari ya baadaye ni sehemu kubwa ya watoto hao waliozaliwa, kujichanganya mtaani na kuishi kama raia wengine, ambayo italeta hatari ya usalama wa nchi.

Katika mapendekezo yake, alisema kuwa ni vizuri serikali ichukue jukumu la kuhakikisha wakimbizi hao, wanarudishwa kwao haraka au wanapewa uraia kwa masharti maalum, ili uwezekano wa kuzuka mambo yasiyo kwenye taratibu, usiweze kutokea.

Katibu wa CCM wilaya ya Kibondo, Stanley Mkandawile alisema ongezeko kubwa la wakimbizi na idadi kubwa ya wakimbizi wanaotoroka kambini na kuishi mtaani, linaongeza matatizo ya utata wa uraia wa wananchi wa mkoa Kigoma ikiwemo nyakati za uchaguzi, jambo ambalo linaweza kuwafanya baadhi ya wakimbizi kupata nafasi za uongozi.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Kirumbe Ng’enda alilalamikia ongezeko hilo kubwa la kuzaliana kwa wakimbizi.

Pia, alilalamikia manyanyaso wanayopata wananchi wa mkoa Kigoma, kuhusu utata wa uraia na kuwafanya wananchi wa mkoa huo kuwa raia wa daraja la tatu.

Katika kuondoa hilo, Ng’enda aliunga mkono kurudishwa kwao wakimbizi wote wanaoishi kwenye makambi mbalimbali mkoani Kigoma, sambamba na serikali kuhakiki uraia wa wananchi wa mkoa huo.

Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, Amandus Nzamba alisema azimio la wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa Kigoma, ni kuitaka serikali kuangalia upya suala la kushughulikia utata wa uraia wa wananchi wa mkoa huo, sambamba na kuangalia ongezeko kubwa la kuzaliana kwa wakimbizi hao.
 
Nimewahi kufanya kazi Kambi za mtendeli na nduta Hali Ni Mbaya Sana ... Watu wanazaliana Kama njugu ... Nilipewa hizi Takwimu katika kituo Cha afya Cha red Cross sikuamini...

Na wakimbizi wengi wanaingia mitaani na kuhatarisha maisha ya watanzania.. Sema waziri akienda kule wanamzuga kwa maneno matamu ... Kuna Siri kubwa nyuma ya wakimbizi kuzaliana Kama serikali ipo humu ijue KUNA SIRI KUBWA ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyo katibu mwenyewe anaitwa Mkandawile, Malawi hawataki waCongo! Maajabu ya dunia!
Ni kweli jina "Mkandawile" hutumika sana Malawi na Zambia! Iweje mtu kama huyu kwenye nafasi ya kitaifa awaone watu wa mkoa wa Kigoma kama wakimbizi?. Basi tukubaliane kuwa mikoa na wilaya za mipakani upande wa magharibi mwa Tanzania, ziwe sehemu ya zile nchi mbili ndogo za Rwanda na Burundi.

sssssehemu
 
Picha
ZAIDI ya watoto 600 wanazaliwa kila mwezi kwenye makambi ya wakimbizi wa Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) yaliyopo mkoani Kigoma.

Hali hiyo imetia hofu wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa Kigoma, ambao wameeleza kutishwa na kasi kubwa ya kuzaliana kwa wakimbizi hao. Hivyo, wameitaka serikali kuchukua hatua kukabiliana na hali hiyo.

Wajumbe hao walitoa kauli hiyo kwenye kikao cha siku moja cha kawaida cha halmashauri hiyo. Walisema kuwa kuendelea kuzaliana holela kwa wakimbizi hao, kutakuwa na madhara makubwa siku zijazo kwa nchi, ikiwemo baadhi ya wakimbizi hao kudai taifa lao ndani ya Tanzania.

Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwanko alisema ametembelea baadhi ya kambi za wakimbizi mkoani Kigoma na takwimu ya watoto 600 wanaozaliwa kila mwezi kwenye makambi hayo ni kubwa sana. Nsanzugwanko alisema kama kambi moja, inaweza kuwa na watoto 600 wanaozaliwa, inakuwaje ukijumlisha kambi zote na kwa mwaka mmoja.

Alisema idadi hiyo ni kubwa na isipowekwa mkakati sasa hivi, athari za baadaye ni kubwa.

Alitaja athari ya baadaye ni sehemu kubwa ya watoto hao waliozaliwa, kujichanganya mtaani na kuishi kama raia wengine, ambayo italeta hatari ya usalama wa nchi.

Katika mapendekezo yake, alisema kuwa ni vizuri serikali ichukue jukumu la kuhakikisha wakimbizi hao, wanarudishwa kwao haraka au wanapewa uraia kwa masharti maalum, ili uwezekano wa kuzuka mambo yasiyo kwenye taratibu, usiweze kutokea.

Katibu wa CCM wilaya ya Kibondo, Stanley Mkandawile alisema ongezeko kubwa la wakimbizi na idadi kubwa ya wakimbizi wanaotoroka kambini na kuishi mtaani, linaongeza matatizo ya utata wa uraia wa wananchi wa mkoa Kigoma ikiwemo nyakati za uchaguzi, jambo ambalo linaweza kuwafanya baadhi ya wakimbizi kupata nafasi za uongozi.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Kirumbe Ng’enda alilalamikia ongezeko hilo kubwa la kuzaliana kwa wakimbizi.

Pia, alilalamikia manyanyaso wanayopata wananchi wa mkoa Kigoma, kuhusu utata wa uraia na kuwafanya wananchi wa mkoa huo kuwa raia wa daraja la tatu.

Katika kuondoa hilo, Ng’enda aliunga mkono kurudishwa kwao wakimbizi wote wanaoishi kwenye makambi mbalimbali mkoani Kigoma, sambamba na serikali kuhakiki uraia wa wananchi wa mkoa huo.

Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, Amandus Nzamba alisema azimio la wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa Kigoma, ni kuitaka serikali kuangalia upya suala la kushughulikia utata wa uraia wa wananchi wa mkoa huo, sambamba na kuangalia ongezeko kubwa la kuzaliana kwa wakimbizi hao.
Acheni ubaguzi ndugu zetu hao tuwahudumie na tuwapende
 
Warundi na wakongoman kwa kuzaa nawapigia saluti sijui siku warundi wote wakirudi kwao kama patawatosha na hivyo hawako smart kichwani kama wanyarwanda
 
Nimewahi kufanya kazi Kambi za mtendeli na nduta Hali Ni Mbaya Sana ... Watu wanazaliana Kama njugu ... Nilipewa hizi Takwimu katika kituo Cha afya Cha red Cross sikuamini...

Na wakimbizi wengi wanaingia mitaani na kuhatarisha maisha ya watanzania.. Sema waziri akienda kule wanamzuga kwa maneno matamu ... Kuna Siri kubwa nyuma ya wakimbizi kuzaliana Kama serikali ipo humu ijue KUNA SIRI KUBWA ...

Sent using Jamii Forums mobile app
Hamna siri yoyote. Binadamu wanakaa bila shughuli yoyote maalumu huku wanalishwa na kuvishwa unategemea nini kitafuata? Ni uzinzi tu. Dawa walirudishwe kwao wakafanye kazi.
 
Mkuu ukweli ni kwamba wanapewa vyakula vilivyoongezewa virutubisho vinavyohamasisha kugegedana, hiyo ndo Siri!
 
Nimewahi kufanya kazi Kambi za mtendeli na nduta Hali Ni Mbaya Sana ... Watu wanazaliana Kama njugu ... Nilipewa hizi Takwimu katika kituo Cha afya Cha red Cross sikuamini...

Na wakimbizi wengi wanaingia mitaani na kuhatarisha maisha ya watanzania.. Sema waziri akienda kule wanamzuga kwa maneno matamu ... Kuna Siri kubwa nyuma ya wakimbizi kuzaliana Kama serikali ipo humu ijue KUNA SIRI KUBWA ...

Sent using Jamii Forums mobile app
Vyakula wanavyopewa mkuu, Kuna kitu kinaongezwa na ni makusudi!
 
Shida ni kwamba hawana kazi za kufanya yaani hawako bise na ubize wao mkubwa ni kupigana miti tu
 
Hatua za haraka inabidi zichukuliwe ama sivyo baadae tutajuta,Jamaa wana ukabila balaa,Wakiendelea kuzalisna namna hiyo wanaweza wakatengeneza nchi yao ndani ya Tz.
 
Back
Top Bottom