Idadi ya Watanzania waliotoa maoni muswada wa katiba hii hapa!

Msouth

Member
Apr 21, 2011
15
0
Waziri Kombani na spika wanasema watanzania wote wamewakilishwa ipasavyo kutoa maoni! Binafsi najiuliza ni wangapi hao? Kama ni Dodoma yalipigwa Mabomu na wengi hawakushiriki. Kule zanzibar alienda mzee sita wakachanachana ule muswada mbele yake. Dar kwenyewe ziliibuka fujo,zomea zomea n.k. Asubuhi leo kwenye kipindi cha star tv waziri kadai anamakabrasha kibao ya maoni ya wananchi!

Nilishangaa alipoulizwa na mh. lisu ni maoni ya mswada mpya au wa awali alibaki kucheka cheka!
Tuwaunge mkono wabunge wetu waliofikisha ujumbe kwa kuugomea mswada! Magamba wanagonga meza na kushambulia lisu badala ya hoja iliyoko mbele.
Nawasilisha!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom