Idadi ya wanaonunia koridoni na kuchekea ukumbini itaongezeka ndani ya CCM

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Zipo habari za mtandaoni zinazosema kuwa wale "wageni maalum wa jinsia ya kike" wa waheshimiwa wabunge ambao ni wa jinsia ya kiume, wamepungua huko Dodoma.

Pia kuna habari nyingine zinasema kwamba hata wale wageni wasio na ulazima wanaotambulishwa na mheshimiwa spika au naibu wake, wakiwa wamekaa kwenye sehemu ya wageni, na wenyewe wamepungua. Hii ni kutokana na zoezi halisi la wabunge kulazimika kufunga mikanda.

Ninaiona CCM ambayo ilizoea kubeba kila mtu kuanzia wacha Mungu mpaka wafanyabiashara "wapigaji", ikiwa na muonekano mpya ndani ya miezi michache ijayo.

Ulikuwepo utamaduni wa watu wenye nafasi zao nzito ndani ya CCM kujirahisisha kwa wenye fedha, na matokeo yake akakosekana aliye msafi mwenye kuweza kumnyooshea kidole mwenzake.

Kwa mtindo huu mpya wa taasisi kulazimika kuishi ndani ya pato lililo halali, naiona CCM ikilazimika kurudi kwenye misingi ya kijamaa, hakuna tena nafasi ya mtu kutumia kile ambacho hajakitokea jasho.

Nilikuwa namshangaa rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa na nafasi ya "kupiga fedha" lakini akiishi kwa kutegemea mshahara wake, nilikuwa namwambia mbona marafiki zako wote wamejenga mahekalu wewe vipi?. Akawa ananiambia yeye ana malengo ya mbali. Mheshimiwa mkuu wa nchi amempa cheo kikubwa na sasa nimeelewa ni kwanini jamaa yangu huyu anaweza kupeta sana kwenye awamu ya tano. Yeye na wengine waadilifu wanayo nafasi ya kuacha legacy itakayodumu.

Kwa hali hii naona ongezeko la watu ambao wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano watakuwa wakicheka na kuonyesha sura za bashasha lakini wakiwa koridoni wananuna na kuendelea kuomboleza baada ya mianya yao ya fedha nyepesi nyepesi kuwa imeshakatwa au ikiendelea kukatwa.
 
Nafikiria hi style ya Magu kwanza itapunguza hata idadi ya watoto wenye walezi wa jinsia 1 tu, nadhani pia itazifanya ndoa za watu zidumu hasa za waheshimiwa, style hi pia itawafanya hata wasiojua uchumi wa ujue kwasababu sasa kila mtu ataishi kwa bajeti yake halisi lakini pia nadhani itapunguza maambukizi ya UKIMWI ingawa style hi pia itaua biashara za bar and hence uchumi kuathirika kidogo.
 
Back
Top Bottom