Uchaguzi 2020 Idadi ya Wagombea Wanawake katika nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
UCHAGUZI 2020: WAGOMBEA WANAWAKE KATIKA NAFASI YA URAIS, UDIWANI NA UBUNGE

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Kaijage amesema Wagombea wanawake katika kiti cha Rais ni 2 kati ya 15 sawa na asilimia 13 na kwa Makamu wa Rais wanawake ni 5 kati ya 15 sawa na asilimia 33.

Amesema kwa mujibu wa takwimu kuna jumla ya Wagombea 1,257 katika nafasi ya ubunge na kuna Wagombea 9,237 katika nafasi ya Udiwani.

Wagombea wanawake kwa nafasi ya Ubunge walioteuliwa ni 294 sawa na asilimia 23 ambako kwa upande wa Madiwani, wanawake walioteuliwa ni 669 sawa na asilimia 7.2 ya Wagombea wote.
 
Back
Top Bottom