Idadi ya wafanyakazi wa kigeni katika Hoteli za kitalii Tanzania - Ramada case

mwanangwa130

Member
Aug 25, 2013
22
8
Kumekuwa na idadi kubwa sana ya raia wa kigeni wakifanya kazi katika mahoteli hapa nchini , either pasipo kuwa na vibali halali au pasipo kuwa na sifa stahiki- kwa mfano unakuta raia wa kigeni eti anakuja nchini kuwa purchasing manager katika hotel wakati kuna wazawa wengi ambao wanamaliza masomo katika vyuo mbali mbali hapa nchini, au unaletewa raia toka mashariki y mbali kuja tu kufanya kazi ya kuonja wine halafu anavuta mshiko safi upatao dola 2000 kwa mwezi.

Naandika haya kwa uchungu sana sana ndugu zangu watanzani, wizara ya kazi na wizara ya mambo ya ndani mko wapi? sheria ya TIC kama sikosei inasema kuwa raia wakigeni wawe watano tuu katika hotel na sio zaidi!!! lakini hotel ya Ramada Resort Dar es salaam ina wafanyakazi wa kigeni wapatao kumi na nane!!!???

Halafu sasa hawa wote mwenye cheo sahihi na kibali chake cha kazi ni general manager tuu wengine wote ukiangalia picha zilizobandikwa katika management chart tofauti kabisa na address za email zao na business cards zao. Halafu wana mwanasheria wao huyu dada ndio anakuwa anawadanganya sana ili aendelee kuwalia pesa wateja wake wakati fika akijua sheria inasemaje.

Napenda kutoa wito kwa hizi wizara mbili tena kwa mara nyingine 'wizara ya kazi na ajira ya mama Jenister Muhagama na ya wizara ya ambo ya ndani ya bwana Charles Kitwanga' waangalie kwa jicho la tatu sana hili jambo, maana sector ya utalii hususani upande huu wa mahotel wametusahau sana huku.

Kama mtakumbuka, hivi juzi tuu hata muda haujapita raia mmoja aitwae Dennis Smith aliwatukana wafanyakazi wake kuwa ni manyani, wafanyakazi wakagoma na kumtaka GM amuondoe la sivyo watafanya watakachokijua, kweli GM akamwambia kuwa mambo magumu na usije kazini jamaa akaondoka nchini wakati shauri lake la kosa la kuwatukana raia wa Tanzania manyani likiwa kwa kamishna wa kazi- Huyu jamaa aliondoka nchini pasipo mtu kujua na hakutumia uwanja wa ndege huu wa dar.....! uhamiajia hawakujua hili na kwanini walimruhusu kupita huko alikopita mipakani?????????.

Leo ni siku ya tatu toka Human resource manager nae kufukuzwa kazi eti kafanya kosa kutoa comment kwenye gazeti wakati anaulizwa na mwandishi wa gazeti la Mwananchi katika kesi ya Manager wa food and beverage bwana Dennis Smith kuwaita staff wake manyani ndio kosa lilofanya bwana huyu HR Sebastian Nchimbi kufukuzwa kazi. Tumehudhunika sana kwa kweli kwa huyu HR wetu kufukuzwa kazi tunaomba wizara hizo nilizo zitaja hapo juu mumu mfuate huyu bwana na kujua mambo kwa undani kwani notice yake inaishia tarehe 29/4/2016.

Kingine cha kushangaza ni bwana fedha mkuu wa pale muhindi aneitwa Saleem Abdul Abonhi huyu ana watoto wake wawili wapo likizo wamekuja hapa dar na wanafanya kazi idara ya finance huku ,je hawa watoto nao wanavibali vya kazi? au ni sheria kweli inaruhusu kuwa hivi- wana week sasa tunakula nao chai canteen,lunch and dinner then jioni wanaondoka na baba yao.

Halafu huyu hapa tunamtambua kama director of finance lakini katika management chart kaandikwa system manager - director of sales and marketing yeye kaandikwa sales consultant- Cost controller yeye kaandikwa cost analyst- revenue manager yeye kaandikwa business analyst- Assistant food and beverage manage yeyeaandikwa Banquet manager -na wengine wengi wengi au chief engineer huyu anakibali kama cha training manager maajabu haya.

Yaani kila siku wanalalamika mapato hakuna lakini wanaletana kila uchao, na payroll ya hotel nzima hawa jamaa wanakula 90% iliyobaki ndio wanakula staff wazawa.

Na kuna tetesi ambazo zimezagaa tunazisikia jengo zima kuwa watawala wanataka kumtimua mwenyekiti wetu wa chama cha wafanyakazi tawi la RAMADA RESORT 'chama chetu cha mahotelini na wafanyakazi wa majumbani kinaitwa CHODAWU. kisa eti alienda katika media kureport swala la boss wake kuwa amewatuka wao manyani mpaka kupelekea expert huyu kufukuzwa kazi (Dennis Smith).

Mwenyekiti wetu ndio kwanza juzi tuu kateuliwa/kachaguliwa na staff katika uchaguzi uliofanyika mbele ya usimamizi wa viongozi kutoka makao makuu ya CHODAWU. sasa anaonekana ni mtu mwenye msimamo sana ndio wanaona mbele itakuwa shida ni bola wakamtoa mapema.

Mweye hotel hii ni muhindi mwenye uraia wa Tanzania pia ni agent mkubwa sana wa bidhaa hizi za AMERICAN GARDEN hapa nchini maarufu kwa jina la MORTY lakini jina la Kuzaliwa ni Murtaza Fadhali mtu poa sana anahela mbayaa, lakini amekosa management ya kumuongozea hotel yake sasa imebakia kuharibu na kuweka mtafaruku na wafanyakazi, hotel haina muda sana toka ifunguliwe yapata kama mwaka mmoja na ni bonge la five star hotel na ina sifa nzuri kwa huduma mbali mbali za ndani mjengo kwa ujumla kwa kweli tatizo ni MANAGEMENT.

Namalizia kwa kusema Muheshimiwa Jenister Muhagama na Muheshimiwa Charles Kitwanga anglieni sana sana hii sector ya hotel kwa kweli, waangalieni sana wasaidizi wenu wa idara ya kutoa vibari vya kazi, angalieni sana uhamiaji hawa wa wilaya ya kinondoni kila siku wanakuja wanapewa mshiko, wanauliza passport, wanapewa chakula wanakula vingine wanafungiwa take away basi na jamaa wanarudi kufanaya kazi kama kawaida- Maana jamaa wakija wa uhamiaji hawa wageni wote wasiokuwa na vibali wanakimbilia katika apartment yao pale Jangwani seabreae kama una unaelekea Africana ukitokea Ramada mkono wa kulia unakata kwa mbele kulia ndioa kuna villas kibao wanaishi hapo.

Au uhamiaji wakija wanaishia mapokezi halafu jamaa wanafichwa vyumbani au vyooni kwani baadhi ya wenzetu huwa sio waaminifu wanawashtua hawa jamaa wa kigeni wakimbie/wakijifiche kupeka uhamiaji.

COPY kwa wakuu wetu wa nchi Magufuli na Majaaliwa (labda mnafichwa kuhusu ukweli, haya ndio yanayofanyika huku katika sector ya matotel/utalii)

Bwana yesu asifiwe/wabilah tawfiq
 
Mkuu asante sana kwa kutumbua jipu kwa upande wako huo.

Kuhusu Waziri Charles Kitwanga ambaye ni boss wa idara ya uhamiaji nchini, usitegemee kabisa kupata msaada wowote kutoka kwa mtu huyu.

Naomba nikurudishe nyuma kidogo ili uweke kumbukumbu zako sawa.

Si unakumbuka kipindiki cha miezi ya mwanzo ya utawala wa Magufuli, liliibuka swala ili ili la wahamiaji haramu, wageni kufanya kazi bila vibali na wageni kufanya kazi ambazo watanzania ndio wanatakiwa kuzifanya.

Balozi wa China nchini aliandaa chakula cha jioni, na mgeni rasmi alikuwa huyu Charles Kitwanga.

Baada ya icho chakula cha jioni, hakuna tena mchina aliyekamatwa, ilhali wamejazana pale karikoo wakiendelea na shughuli zao za umachinga kama kawaida.

Kwa kumalizia, huyu waziri Charles Kitwanga amekuwa na atendelea kuwa sio mtu wa msaada kwa watanzania. Kwa kifupi yupo pale kwa ajili ya kulindana na Magufuli analijua hilo.
 
Aisee bora uwaeleze wakina Mh. Jenisteer Mhagama na Mh. Charles Kitwanga waelewe kuna wahamiaji haramu wengi sana apa Tanzania. Kila kona wamejazana.

Mimi napendelea ktk sehemu zenye mikusanyiko ya watu. Police officer wangepewa Mamlaka ya kukuoji vitambulisho vyako kwa mtu yoyote akiisi kwamba wewe sio MTANZANIA.

Kama hapa maeneo ya Ubungo Mataa Kuna wageni wengi wanaokuja Kuchukua mizigo na Magari yao bandarini. Wanakuwa wakifika Mataa awaerewi bandarini kuelekea waende na njia ipi sasa apo nashindwa kuelewa wanapitaje uko barabarani bila kujua wanapoelekea wengi Kuna Wamarawi, wazambia, Zimbabwe, wakongo, waganda, wakenya, wasomali na mataifa mengi.

Alafu wanigeria wamekuwa wengi sana hapa Dar es salaam, sasa sjui wanafanya biashara gani.

Wangeweka sheria hata ktk izi guest house na motel. Sheria kuhusu wageni wengi wanalala awana pasi wala documents zozote.

Tanzania tunatakiwa ktk migration wajaribu kufanyia kazi hii kitu. Au hata watu wa magazeti wafanye utafiti apa Ubungo Kuna hotel nyingi wanalala wageni wasiokuwa na vibali hata kidogo
 
Punguza fitina fanya kazi shukuru mwekezaji amekupa ajira. Kama vipi fungua biashara yako weka watoto wako wakusaidie.
 
Labda umesahau kuwa nchi hii mgeni ni bora kuliko mtz safari ni ndefu.Kitwanga kwa sasa yupo anahangaikia jinsi kusave tuhuma Lugumi mtoto wa nyumbani.
 
Hao maofisa wa immigration ndio wabaya zaidi,wanazungukia mahoteli na makampuni mbalimbali ambayo wanajua fika kuna wageni na kuvuta rushwa,juzi juzi waliingia kampuni fulani mikocheni kuna wakenya wakavuta halafu wakaingia kwa wachina wakavuta pia.tena wanavuta mkwanja mrefu.
 
Hayo wafanyakazi walicho eleza yote ni ya kweli maana kazi ambayo watanzania wanaweza kufanya lakini expert wanafanya cha ajabu hawana ubora wowote lakini kama rangi yao na lugha sawa labda nasi tujikoboe
 
Hao maofisa wa immigration ndio wabaya zaidi,wanazungukia mahoteli na makampuni mbalimbali ambayo wanajua fika kuna wageni na kuvuta rushwa,juzi juzi waliingia kampuni fulani mikocheni kuna wakenya wakavuta halafu wakaingia kwa wachina wakavuta pia.tena wanavuta mkwanja mrefu.
Acha uoga wataje kama mwenzio hapo juu alivyofanya
 
Watu wa MIGRATION pale maeneo ya Godown za pale Ubungo. Kuna waindi, wachina na waarabu kibao awana vibari. Wakisikia police wamepita wanajificha awatoki awana documents zote zozote za kuishi apa Tanzania.
 
Kumekuwa na idadi kubwa sana ya raia wa kigeni wakifanya kazi katika mahoteli hapa nchini , either pasipo kuwa na vibali halali au pasipo kuwa na sifa stahiki- kwa mfano unakuta raia wa kigeni eti anakuja nchini kuwa purchasing manager katika hotel wakati kuna wazawa wengi ambao wanamaliza masomo katika vyuo mbali mbali hapa nchini, au unaletewa raia toka mashariki y mbali kuja tu kufanya kazi ya kuonja wine halafu anavuta mshiko safi upatao dola 2000 kwa mwezi.

Naandika haya kwa uchungu sana sana ndugu zangu watanzani, wizara ya kazi na wizara ya mambo ya ndani mko wapi? sheria ya TIC kama sikosei inasema kuwa raia wakigeni wawe watano tuu katika hotel na sio zaidi!!! lakini hotel ya Ramada Resort Dar es salaam ina wafanyakazi wa kigeni wapatao kumi na nane!!!???

Halafu sasa hawa wote mwenye cheo sahihi na kibali chake cha kazi ni general manager tuu wengine wote ukiangalia picha zilizobandikwa katika management chart tofauti kabisa na address za email zao na business cards zao. Halafu wana mwanasheria wao huyu dada ndio anakuwa anawadanganya sana ili aendelee kuwalia pesa wateja wake wakati fika akijua sheria inasemaje.

Napenda kutoa wito kwa hizi wizara mbili tena kwa mara nyingine 'wizara ya kazi na ajira ya mama Jenister Muhagama na ya wizara ya ambo ya ndani ya bwana Charles Kitwanga' waangalie kwa jicho la tatu sana hili jambo, maana sector ya utalii hususani upande huu wa mahotel wametusahau sana huku.

Kama mtakumbuka, hivi juzi tuu hata muda haujapita raia mmoja aitwae Dennis Smith aliwatukana wafanyakazi wake kuwa ni manyani, wafanyakazi wakagoma na kumtaka GM amuondoe la sivyo watafanya watakachokijua, kweli GM akamwambia kuwa mambo magumu na usije kazini jamaa akaondoka nchini wakati shauri lake la kosa la kuwatukana raia wa Tanzania manyani likiwa kwa kamishna wa kazi- Huyu jamaa aliondoka nchini pasipo mtu kujua na hakutumia uwanja wa ndege huu wa dar.....! uhamiajia hawakujua hili na kwanini walimruhusu kupita huko alikopita mipakani?????????.

Leo ni siku ya tatu toka Human resource manager nae kufukuzwa kazi eti kafanya kosa kutoa comment kwenye gazeti wakati anaulizwa na mwandishi wa gazeti la Mwananchi katika kesi ya Manager wa food and beverage bwana Dennis Smith kuwaita staff wake manyani ndio kosa lilofanya bwana huyu HR Sebastian Nchimbi kufukuzwa kazi. Tumehudhunika sana kwa kweli kwa huyu HR wetu kufukuzwa kazi tunaomba wizara hizo nilizo zitaja hapo juu mumu mfuate huyu bwana na kujua mambo kwa undani kwani notice yake inaishia tarehe 29/4/2016.

Kingine cha kushangaza ni bwana fedha mkuu wa pale muhindi aneitwa Saleem Abdul Abonhi huyu ana watoto wake wawili wapo likizo wamekuja hapa dar na wanafanya kazi idara ya finance huku ,je hawa watoto nao wanavibali vya kazi? au ni sheria kweli inaruhusu kuwa hivi- wana week sasa tunakula nao chai canteen,lunch and dinner then jioni wanaondoka na baba yao.

Halafu huyu hapa tunamtambua kama director of finance lakini katika management chart kaandikwa system manager - director of sales and marketing yeye kaandikwa sales consultant- Cost controller yeye kaandikwa cost analyst- revenue manager yeye kaandikwa business analyst- Assistant food and beverage manage yeyeaandikwa Banquet manager -na wengine wengi wengi au chief engineer huyu anakibali kama cha training manager maajabu haya.

Yaani kila siku wanalalamika mapato hakuna lakini wanaletana kila uchao, na payroll ya hotel nzima hawa jamaa wanakula 90% iliyobaki ndio wanakula staff wazawa.

Na kuna tetesi ambazo zimezagaa tunazisikia jengo zima kuwa watawala wanataka kumtimua mwenyekiti wetu wa chama cha wafanyakazi tawi la RAMADA RESORT 'chama chetu cha mahotelini na wafanyakazi wa majumbani kinaitwa CHODAWU. kisa eti alienda katika media kureport swala la boss wake kuwa amewatuka wao manyani mpaka kupelekea expert huyu kufukuzwa kazi (Dennis Smith).

Mwenyekiti wetu ndio kwanza juzi tuu kateuliwa/kachaguliwa na staff katika uchaguzi uliofanyika mbele ya usimamizi wa viongozi kutoka makao makuu ya CHODAWU. sasa anaonekana ni mtu mwenye msimamo sana ndio wanaona mbele itakuwa shida ni bola wakamtoa mapema.

Mweye hotel hii ni muhindi mwenye uraia wa Tanzania pia ni agent mkubwa sana wa bidhaa hizi za AMERICAN GARDEN hapa nchini maarufu kwa jina la MORTY lakini jina la Kuzaliwa ni Murtaza Fadhali mtu poa sana anahela mbayaa, lakini amekosa management ya kumuongozea hotel yake sasa imebakia kuharibu na kuweka mtafaruku na wafanyakazi, hotel haina muda sana toka ifunguliwe yapata kama mwaka mmoja na ni bonge la five star hotel na ina sifa nzuri kwa huduma mbali mbali za ndani mjengo kwa ujumla kwa kweli tatizo ni MANAGEMENT.

Namalizia kwa kusema Muheshimiwa Jenister Muhagama na Muheshimiwa Charles Kitwanga anglieni sana sana hii sector ya hotel kwa kweli, waangalieni sana wasaidizi wenu wa idara ya kutoa vibari vya kazi, angalieni sana uhamiaji hawa wa wilaya ya kinondoni kila siku wanakuja wanapewa mshiko, wanauliza passport, wanapewa chakula wanakula vingine wanafungiwa take away basi na jamaa wanarudi kufanaya kazi kama kawaida- Maana jamaa wakija wa uhamiaji hawa wageni wote wasiokuwa na vibali wanakimbilia katika apartment yao pale Jangwani seabreae kama una unaelekea Africana ukitokea Ramada mkono wa kulia unakata kwa mbele kulia ndioa kuna villas kibao wanaishi hapo.

Au uhamiaji wakija wanaishia mapokezi halafu jamaa wanafichwa vyumbani au vyooni kwani baadhi ya wenzetu huwa sio waaminifu wanawashtua hawa jamaa wa kigeni wakimbie/wakijifiche kupeka uhamiaji.

COPY kwa wakuu wetu wa nchi Magufuli na Majaaliwa (labda mnafichwa kuhusu ukweli, haya ndio yanayofanyika huku katika sector ya matotel/utalii)

Bwana yesu asifiwe/wabilah tawfiq
Hao mawazirii xjuagi kazi wanayofanyaa kwakweli Mungu Atusaidie Watanzaniaa,,,
 
Uhamiaji ni walarushwa wakubwa katika idala inayotakiwa kuwa makini ni uhamiaji na haya mambo ya ugaidini hatari sana idara kama uhamiaji wanakuwani watu wakwenda katika mahotel nakukunja pesa... Juzi nimeona watu wa uhamiaji wamekuja Ramada kama 8 hivi waliwashtukizia menejiment hivyo hawakuwakimbiza wafanyamazi haramu wakaenda kwa GM kwa kirefu sana ilammoja naonakakatiwa ticket kaondoka kwao, uhamihaji wanachukua rushwa sasa nawataadharisha siku wakirudi napiga picha mwenyewe kwa ngazi husika nyinyi ndo mnaosababisha wahamihaji haramu wawepo wenzetu kitengo cha uhamiaji ni sekta nyeti sana...... Uhamiaji kaeni chonjo!!
 
Hivi idara ya Uhamiaji inafanya kazi yake kweli?
Huwa wanaenda kuchukua hela na kutokomea. Ukiisoma ile sheria inayowapa vibali wageni kufanya kazi nchini iko poa sana, tatizo watekelezaji ni majipu. Mtu hata kama ana qualify sheria inamwambia afanye kazi huku akitengeneza succession plan ya wazawa. Utashangaa kuna mzungu namfahamu anapiga kazi bongo toka 1990 ana renew vibali tu sa sijui anaowafundisha hawafundishiki
 
TATIZO LETU UVIVU NA WIZI MARA TUKIPATIWA KAZI HASA ZA HOTEL.... MATZ LAZIMA TUBADILIKE TUACHE KULIA LIA....

MTOA POST UNADHAMIRA YA KUUWA HAYA MAHOTEL.
UNAUFAHAMU UFANYAJI KAZI WA HOTELIAR WA KITANZANIA?
Uvivu, wizi umekuwepo ktk kila idara hapa TZ na hii imejengeka haswa ktk miaka kama 20 iliyopita.

Ni mfumo ambao tumetengenezewa ukaingia mpaka kwenye damu kiasi kwamba tunajiona kazi ni kuiba tu bila hivyo no life

Inatia uvivu sana na inaongeza niwe mwizi mno pale unapoona analetwa muhindi kutoka India asiyejua chochote anakuja kufanya kazi kama ninayofanya mimi anapewa nyumba, usafiri, matibabu na mshahara $3000 usiokatwa kodi mimi nabaki napewa laki 6 inayokatwa kodi, NSSF,... no house, no transport, no what na mimi ndiyo nam-train huyu muhindi baadae anakuja kuwa boss wangu anavuta $6000 per month.

Hivi niache kukuibia si nitakuwa kichaa
 
Kuna watanzania kibao wabeba box mpaka wengine wanajiita Rais wa wabeba box. Acha lawama fanya kazi mgeni hazibi riziki yako jitume upate chako tu.
 
Back
Top Bottom