Idadi ya vifo vilivyotokana na mgomo wa madaktari

mtendaji wa kijiji

JF-Expert Member
Jul 3, 2012
533
114
Ndugu wanajamvi kufuatia mgomo wa madaktari unaoendelea watu wengi wamepoteza maisha wakiwa hospitalini, njiani kupelekwa Private hospitals na kurudishwa majumbani kutokana na Mgomo. Kulingana na Tathmini niliyoifanya mimi katika hospitali ya rufaa mhimbili na baadhi ya mitaa katika jiji la Dar na Mbeya watu 698 wamepoteza maisha katika wiki hz za mgomo. JK na utawala wako mna kesi ya kujibu na Ifike hatua sasa mshughulikie matatizo kwa dhati na sio kushutumu CHADEMA wakati ninyi ndo vyanzo vya matatizo na vifo hivi kwa utendaji wenu dhaifu. Swalahili la mgoo tusilihusishe kabisa na siasa
 
idadi hiyo ni kubwa sanaaaaa.sidhani kama ina ualisia lakini asante kwa taarifa
 
mmhh, mbona wengi hivyo!?? umefanya research kweli!!

Polen wafiwa, mungu awape faraja
 
Dah inatia hasira sana kwa upuuzi wa migomo isiyo na kichwa wala miguu.
 
waulize madaktari ni watu wangapi wanakufa kwa kukosa matibabu ya kawaida sababu ya upungufu wa vitendea kazi. Nasikia katika wodi ya watoto muhibili hufa watoto 10 kila siku , piga idadi hiyo kwa mwezi uone balaa lake
naona ni vizuri madaktari mtuwekee data za vifo hata kabla ya mgomo ambavyo vingeweza kuzuilika kama mazingira yenu yangeboreshwa
 
Unaweza ukapoteza watu 100 kwenye mgomo lakini ukaokoa 1000 baada ya mgomo kama huduma zitaboreshwa
 
Mnatupa pole ili iweje?. Waswahili wanasema "Msiba usikie kwa mwenzio". Acheni zenu kutoa pole za kinafiki huku mkihalalisha vitendo vilivyosababisha. Wakati mwingine ni busara kukaa kimyaa utawafariki vizuri zaidi.
 
ndugu wanajamvi kufuatia mgomo wa madaktari unaoendelea watu wengi wamepoteza maisha wakiwa hospitalini, njiani kupelekwa private hospitals na kurudishwa majumbani kutokana na mgomo. Kulingana na tathmini niliyoifanya mimi katika hospitali ya rufaa mhimbili na baadhi ya mitaa katika jiji la dar na mbeya watu 698 wamepoteza maisha katika wiki hz za mgomo. jk na utawala wako mna kesi ya kujibu

huu ni upuuzi - kwa nini madaktari wasipelekwe court mashall kujibu tuhuma hizi na wakipatikana na hatia wacharazwe risasi jangwani.
 
Hata Wamarekani, Waingereza na nchi nyingi zilizoendelea walikufa watu wengi mpaka wakafika hapa walipo kimaendeleo.
 
Hakuna maendeleo bila kusacrify, madk mue na msimamo ili jambo sio la kujirudia kila sku,. Kieleweke
 
Jk na Liwalo na Liwe ndo wanaostahli kunyongwa kwa hivi vifo kwani wameendelea kufanya ubabe tangu february bila kuwa sikiliza madaktari. Ukichukua taarifa ya kamati ya bunge huduma zajamii ilipo kaka kuchunguza mgomo huu utagundua serikali lazima ishtakiwe na hii ndo mana wanaizuia kujadiliwa Bungeni
huu ni upuuzi - kwa nini madaktari wasipelekwe court mashall kujibu tuhuma hizi na wakipatikana na hatia wacharazwe risasi jangwani.
 
Tupunguze madaraka ya Rais kwenye katiba na kumwondolea kinga ili 2016 tumswage Jk mahakama ya kimataifa, ili watakao fuata wajifunze
Hata Wamarekani, Waingereza na nchi nyingi zilizoendelea walikufa watu wengi mpaka wakafika hapa walipo kimaendeleo.
 
Back
Top Bottom