Idadi ya vifo kutokana na virusi vya Corona ndani ya siku moja yafikia viwango vipya nchini Brazil

Sam Gidori

Verified Member
Sep 7, 2020
96
150
Brazil imerekodi idadi kubwa zaidi ya vifo ndani ya siku moja vinavyotokana na virusi vya corona tangu kuanza kwa mlipuko.

Jumla ya watu 2,286 walifariki dunia ndani ya saa 24 pekee siku ya Jumatano na kufanya idadi ya vifo kufikia 268,370, kwa mujibu wa takwimu za Chuo Kikuu cha John Hopkins. Visa vya maambukizi vilivyorekodiwa ndani ya siku moja vilifikia 79,876. Brazil ni nchi ya pili kuathiriwa zaidi na virusi vya corona baada ya Marekani.

Wataalamu wanaonya kasi kubwa ya maambukizi na aina mpya ya virusi vinavyoonesha kuwa na nguvu zaidi huku miundombinu ya afya nchini humo inaonekana kuzidiwa. Vyumba vya kuhudumia wagonjwa mahututi vimejaa kwa asilimia 90 katika miji ya Rio de Jeneiro na São Paulo, katika Mji Mkuu, Brasilia ICU zimejaa kabisa huku miji ya Porto Alegre na Campo Grande ikiwa na wagonjwa wengi katika vyumba vya kuhudumia wagonjwa mahututi kuliko idadi inayoweza kuhudumiwa.

Rais wa Brazil analaumiwa kwa kuonesha uzembe kudhibiti maambukizi ya corona. Rais wa zamani wa nchi hiyo, Luis Inacio Lula da Silva ametaja maamuzi ya rais Jair Bolsonaro kuwa ni ya 'kijinga' na kuwataka wananchi kupatiwa chanjo. Bolsonaro amewataka wananchi wa Brazil kuacha kulalama kuhusu corona, akipinga uvaaji wa barakoa na kukaa karantini.

Chanzo: KBC
 

BlackPanther

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
7,648
2,000
Mutamlaumu Raisi buree, nchi yenyewe imejaa ufuska, uchafu wote uko pale copa cabana n.k....unategemea corona itawaacha salama! Marekani pia hivyo hivyo unategemea itawaacha salama!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom