Idadi ya safari wakati wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China yaashiria uhai na ufunguaji mlango

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,116
1,121
1737509170699.png


Msimu wa safari za Mwaka Mpya wa Jadi wa China umeanza hivi karibuni. Msimu huu ni wa kwanza wa safari za Mwaka Mpya wa Jadi wa China tangu kutangazwa kwa mapumziko ya siku nane ya sikukuu hii, kupanuliwa kwa sera za kutohitaji visa, na kuongezwa rasmi kwa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwenye orodha ya UNESCO ya Urithi wa Kitamaduni Usioshikika wa Binadamu.
Kwa mujibu wa Tume ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi, inatarajiwa kuwa, safari karibu bilioni 9 za ndani ya nchi zitafanyika katika kipindi cha siku 40 za safari, huku idadi ya abiria kwa safari za anga na reli pia zikitarajiwa kufikia rekodi mpya.
Wimbi la safari wakati wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa jadi wa China linadhihirisha maendeleo ya kasi ya kiuchumi na kijamii nchini China. Mtazamo huu unatokana na msingi wa ukuaji endelevu wa uchumi wa China, maendeleo ya kasi ya miundombinu, na kuongezeka kwa kiwango cha maisha.
Kwa mujibu wa Sun Jiashan, mtafiti mshiriki kutoka Idara ya Akademia ya Utamaduni na Utalii, muunganiko wa utamaduni, utalii na usafiri vinawezesha sikukuu za jadi, kama Mwaka Mpya wa jadi wa China, kuchukua sura mpya. Siku hizi, sikukuu hii sio tu watu wanakimbilia kurudi kwenye maskani yao, bali imekuwa taswira ya maingiliano ya desturi na utalii. Kusafiri wakati wa Mwaka Mpya wa jadi wa China kumeibuka kuwa mwelekeo mpya, ukionyesha mageuzi ya ubunifu na maendeleo ya uvumbuzi wa utamaduni mpya wa kisasa wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.
Mwaka huu, huenda Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ikachukua zaidi sura ya kimataifa kuliko miaka iliyopita. Takwimu zilizotolewa na tovuti ya huduma za safari ya nchini China, Ctrip zinaonyesha kuwa, idadi ya maagizo ya safari kutoka kwa watalii wa kigeni kutembelea China wakati wa mapumziko ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China mwaka huu imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 200 ikilinganishwa na mwaka jana, huku Singapore, Japan na Marekani zikiwa na ongezeko la idadi ya watalii wa kigeni wanaotembelea China.
Hatua hii inahusishwa kwa karibu na upanuzi wa sera ya kutohitaji visa kutoka baadhi ya nchi iliyotangazwa mwaka jana. Kwa sasa, watumiaji wa hati za kawaida za kusafiria kutoka nchi 38 hawahitajiki kuomba visa ili kuingia China, na wanaweza kukaa kwa siku chini ya 30. Pia, wageni sio tu wanaweza kutembelea miji ya ngazi ya kwanza na ya pili, bali pia wanaweza kutembelea miji ya ngazi ya tatu na ya nne ili kujifunza zaidi kuhusu China. Msimu wa safari wakati wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa jadi wa China sio tu ni maingiliano ya hisia kwa Wachina, bali unaonyesha nguvu tulivu ya utamaduni wa China na ushawishi wa kimataifa, pia unatumika kama daraja la kipekee linalounganisha China na dunia, na kuonyesha mvuto wa utamaduni wa Kichina.
 
Back
Top Bottom