Idadi ya masheikh yapunguzwa katika mchakato wa kumpata kadhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Idadi ya masheikh yapunguzwa katika mchakato wa kumpata kadhi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Sep 13, 2009.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  September 12, 2009Idadi ya masheikh yapunguzwa katika mchakato wa kumpata kadhiNa Salim Said

  MASHEIKH walioteuliwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa bin Shaaban Simba kukutana na wataalamu wa serikali kujadili jinsi ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania bara watapungua kutoka 25 hadi watano, ili kuharakisha mazungumzo hayo.

  Habari za ndani ya kamati hiyo inayoanza mjadala kesho, zimelidokeza Mwananchi Jumapili kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kuonekana kuwa kamati hiyo ikiwa na wajumbe wengi kiasi hicho haitafikia maamuzi haraka


  “Kingine kilichojiri ni kwamba jopo la masheikh 25 kukaa na kujadili hoja ni kubwa mno na hatuwezi kufikia mwafaka, sasa ikaamuliwa jopo hilo livunjwe na iundwe kamati ndogo ya ufundi yenye wajumbe wasiozidi watano,” kilisema chanzo chetu.


  Chanzo hicho alisema kwamba, jukumu la kuamua nani apungue walikabidhiwa Waislamu wenyewe, isipokuwa walitakiwa kuwasilisha majina ya wajumbe wa kamati hiyo kesho kabla ya majadiliano kuanza.

  Habari zaidi zinaeleza kuwa wajumbe hao walikubaliana kuwa Mufti Simba ndiye ateue wahusika kama alivyofanya kwa wale 25 wa awali,” alidokeza mtoa habari wetu.


  Masheikh hao watano ndio watakutana na Kamati ya Serikali inayoongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe.

  Wazo la serikali kukutana na jopo hilo lilikuja Juni mwaka huu, baada ya Waziri Chikawe kutangaza bungeni kwamba, Mahakama ya Kadhi haitaanzishwa tena nchini, badala yake serikali itatafsiri Sheria za Kiislamu na kuzijumuisha katika sheria za nchi, ili zitumike katika mahakama za kawaida kama inavyofanyika maeneo mbalimbali, ikiwamo Afrika Kusini.


  Kauli hiyo iliibua hasira kali kwa Waislamu huku wengine wakiapa kutokipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM), iwapo Mahakama ya Kadhi haitoanzishwa kama kilivyoahidi kwenye ilani yake, jambo lililoishtua serikali na kuamua kukutana na viongozi wa dini hiyo kujadiliana juu ya suala hilo.


  Kikao cha kwanza cha majadiliano hayo kiliketi wiki iliyopita, lakini hakikujadili chochote kuhusu hoja hiyo, bali Waziri Mkuu Mizengo Pinda alizikutanisha kamati hizo na kutambuana, ili kuanza rasmi mjadala katika kikao cha kesho.


  “Baada ya kukutana Waziri Mkuu aliwatambulisha wajumbe na baadaye alituaga kwamba, anasafiri nje ya nchi na kututakia majadiliano mema. Tarehe ya kukutana ilitangazwa palepale kuwa ni Jumatatu ya Septemba 14, lakini hatujajua hawa wajumbe watano watakuwa ni nani,” alisema mtoa habari wetu.


  Alifafanua kuwa kingine kilichojiri hapo ni kutakiwa kujiandaa ikiwa ni pamoja na kuandaa hadidu za rejea zitakazotuongoza katika majadiliano hayo


  “Katika hilo pia sisi tulidai ripoti za tume za serikali zilizofanya utafiti kuhusu suala la Mahakama ya Kadhi nchini, ambazo ni ile ya Ntagazwa (Arcado) na Janguo (Athuman) ambapo Chikawe aliahidi kuwa hadi Jumatano iliyopita angekuwa ametupatia,” aliongeza.


  Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), ambaye pia ni Katibu wa Jopo la Masheikh 25, Suleiman Said Lolila alikataa kuzungumzia suala hilo kwa kile alichodai si msemaji.


  Alisema jopo hilo lilikuwa chini ya Mufti Simba na kwamba, ndiye anapaswa kuzungumzia mjadala huo kwa upande wa Waislamu na Waziri Chikawe kwa upande wa serikali.


  “Tumekubaliana kwamba wazungumzaji wa mambo haya ni Mufti Simba kwa upande wa Waislamu na Waziri Chikawe kwa upande wa serikali, chukua namba ya Mufti hii (tunayo) mpigie atakueleza,” alisema sheikh Lolila.


  Hata hivyo, Mufti Simba alisema hana taarifa ya kupunguzwa kwa jopo la masheikh 25, ila anachofahamu ni kwamba walitakiwa kuunda sekretarieti ambayo itakuwa na wajumbe watano kutoka katika jopo la masheikh 25 na watatu kutoka serikalini.
  “Sijaelezwa kwamba tunatakiwa tupunguze wajumbe wa jopo la masheikh, ila ninachofahamu ni kwamba tulitakiwa kuunda sekretarieti ya watu wanane, watano kutoka kwa masheikh na watatu serikalini, ili sasa wakae, kupanga na kuratibu ratiba ya mijadala yote,” alisema Mufti Simba.  Imetoka Mwananchi Gazeti
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Tusubiri tu, mapanga yameshaanzwa kunolewa.
   
Loading...