Idadi ya madarasa vs idadi ya walimu

Okwaaa

JF-Expert Member
Dec 3, 2020
1,316
2,917
Itifaki imezingatiwa!

Moja kwa moja kwenye maada. Nimekutana na nyuzi nyingi humu jamii forum zikionyesha juhudi za Mama yaani raisi SSH juu ya uagizaji wa kujengwa kwa madarasa manne manne kila shule. Hizi ni juhudi za makusudi kabisa anazozifanya rais wetu mpendwa ili kutatua changamoto ya ukosefu wa miundo mbinu mizuri ya usomeaji kwa wanafunzi wa sekondari hususani wanaoanza kitato cha kwanza.

My point/suggestions
Kuongezeka kwa madarasa kunatakuwa kuendane pia na idadi ya walimu kwani shule nyingi zina idadi ya walimu wachache saana hususani vijijini. Hii ina maana kuwa kama mwalimu wa hesabu alikuwa anafundisha form one A na B kipindi wanafunzi ni wengi lakini baada ya madarasa kuongezwa kuwa A, B,C, D ,E na F: huyu mwalimu hawezi tena kufundisha hayo madarasa yote bila kuathiri ratiba za kufundisha madarasa mengine.

Hivyo ili kuendana na idadi ya wanafunzi katika kila darasa na idadi ya mikondo iliyopo ni vyema sasa Raisi SSH aweze kuachia ajira za walimu wapya wa kutosha ili sasa suala la ufaulu mbovu wa wanafunzi shule za serikali walaumiwe walimu na wasimamizi wa elimu na siyo serikali.

Kutokuajiri walimu wa kutosha serikali itakuwa imeamua kumtesa mwalimu na kumfanya mwalimu asiwe na muda wa kupumnzika ili aweze kufundisha madarasa yote sita. Wakati hapo kabla alikuwa anafundisha madarasa matatu.

Na walimu nao hujiongeza kwa kuwaunganisha wanafunzi wa mikondo yote ili wawafundishe kwa pa1 kuepuka kujichosha, suala linalopunguza uelewa kwa mwanafunzi na ufanisi wa ufundishaji. Na hivyo tatizo litakuwa halijatatuliwa kabisa.

Wizara ya elimu ombeni vibali vya ajira kwa walimu vya kutosha ili kuwapunguzia kazi kubwa waliyonayo walimu.

Nawasilisha.
 
Enrolment ya watoto tanzania darasa la kwaza kila mwaka ni 1.1m pupils na recommended ratio ya wizara mualimu kwa wanafuzi ni 1-30 kwa gawanya idadi ya wanafunzi kwa ratio ya darasa, ni waalimu laki 340,000 wanao hitajika kwa darasa la kwanza tu kwa ufupi ni kwamba elimu ya tzania ni usani na siasa ilaa sio kusaidia watzania.
 
Enrolment ya watoto tanzania darasa la kwaza kila mwaka ni 1.1m pupils na recommended ratio ya wizara mualimu kwa wanafuzi ni 1-30 kwa gawanya idadi ya wanafunzi kwa ratio ya darasa, ni waalimu laki 340,000 wanao hitajika kwa darasa la kwanza tu.........kwa ufupi ni kwamba elimu ya tzania ni usani na siasa ilaa sio kusaidia watzania.
Sure kabisa, alafu linapifika suala la ufaulu ndo wa kwanza kulaumu walimu. Hivi hakuna study research zozote walizozifanya ili kuweza kujua kinachosababisha utofauti wa ufaulu gvt schools na private schools??

Alafu kuna muda nawaza kama je agizo hilo utekelezeaji wake utafanikiwa 100%??? Naona jinsi watu wanavyoenda kuzibutua hizo hela za ujenzi!
 
Back
Top Bottom