Idadi ya abiria kwenye meli iliyozama, nani anasema kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Idadi ya abiria kwenye meli iliyozama, nani anasema kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAMMAMIA, Jul 20, 2012.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Sumatra ilisema abiria walikuwa 288 (watu wazima 288+31+9 watoto na mabaharia)
  Ikulu Zanzibar ilitaja abiria 290 (sijui wawili walitoka wapi)
  Leo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM imebandika majina ya watu 340 (ziada ya watu 50, 52)
  Nani anasema ukweli?

  Haya ndio yale yale yaliyotokea mwaka jana katika ajali ya Spice Islanders - Idadi kamili haikupatikana hadi leo. Makosa yale yale yamekuwa yakijirejea siku hadi siku. Hivi viongozi wetu wana akili za mende kuwa wanasahau kila baada ya sekunde moja?

  Nimesoma kwenye gazeti moja Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi anajitetea kuwa "Asilaumiwe mtu kwa kazi ya Mungu". Kwa nini basi wanajazana mawizarani, wasimwache Mungu aongoze nchi? Abiria wametoa ushahidi kuwa tangu meli ilipozama hadi kufika chombo cha kwanza kuwaokoa yalipita masaa mawili kwa mahali pa masafa ya kutumia dakika 25. Mungu hauwi, yeye hupokea tu roho zaviumbe wake waliodhulumiwa maisha yao.
   
 2. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kwanza meli haina ofisi halafu ijulikane watu wangapi walipanda, hii haiwezekani kabisa. Suala la kazi ya Mungu kuua ni ushetani kabisa. Kutoka kwenye nafsi yangu iliyowazi kabisa, sikubaliani na maneno haya ya mashetani. Haiwezekani jeshi la maji lipo, kitengo cha maafa kipo, msalaba mwekundu ie akina kimbisa wapo lakini imeshindikana kuwasaidia watu waliokuwa wanaweza kuokolewa ndani ya dakika 45 mpaka kuwapelekea umauti. Haya ni maneno ya mashetani kabisa.
   
 3. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Mkuu ingekuwa vyema upige picha hayo majina, post hapa.
   
 4. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  kwa kweli hali hii inatilia mashaka sana utekelezaji na uwajibikaji wa viongozi wetu, kama ni nchi kujifunza kutokana na haya basi uwezekano wa watanzania kuona mabadiliko ni sufuri sababu wote tutaangamia kabla ya...
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kama ambavyo mafisadi hukimbilia kusema "amri hii imetoka juu" ili wasiulizwe, na hawa wachawi wakubwa wanakimbilia Mungu ili wasiulizwe, wakisahau kuwa Mungu hahitaji hata kuwauliza, atawasweka kwenye 1000000000ºC

  Mkuu, hiyo taarifa ya kubandikwa majina imetoka kwenye vyombo vya habari tu. Pengine ukienda huko Ofisi ya Mkuu wa Mkoa hakuna hata mlinzi.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,747
  Likes Received: 82,686
  Trophy Points: 280
  Kauli kama hiyo inaudhi sana kusema kweli. Vyombo vya usafiri havikaguliwi ili kuhakikisha kama vina hadhi ya kuruhusiwa kubeba abiria halafu ajali ikitokea wanakimbilia kutoa kauli ya "ajali hii/ile ni kazi ya Mungu." Hawajafanya hata uchunguzi tayari wameshaanza kutoa kauli zisizo na mshiko.
   
 7. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hahaha - Huo mshiko wanaupata baada ya kuunda tume ambazo hawazifanyii kazi. Soma: Ripoti ya ajali ya MV Spice Islanders 2011, kuanzia ukurasa wa 75, uone kama mapendekezo ya tume yamefanika kazi mpaka imetokea ajali nyengine. Sijui hawa huyo Mungu wao anaishi wapi niende kutata naye.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,747
  Likes Received: 82,686
  Trophy Points: 280

  Ndiyo yale yale ya Serikali DHAIFU kutokuwa na uwezo
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,747
  Likes Received: 82,686
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Ajali ya Zanzibar si upepo mkali

  na Datus Boniface
  Tanzania Daima  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema kuwa ajali ya meli iliyotokea Zanzibar haijasababishwa na upepo mkali kama inavyoelezwa.

  Mkurugenzi wa taarifa za utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa, aliliambia gazeti hili jana kuwa huenda ajali hiyo imetokana na sababu zingine, kwani kama ungekuwa upepo ni wazi kuwa meli, boti na mitumbwi iliyopo kwenye Bahari ya Hindi vingezama au kupeperushwa.

  "Siwezi kuitaja sababu ya ajali ya juzi, isipokuwa naweza kusema kuwa upepo ulikuwa wa kasi ya kilometa 30 hadi 40 kwa saa," alisema.
  Kwa mujibu wa maelezo yake, upepo wa juzi ulikuwa mkali kwenye ukanda wa Bahari ya Hindi na kusababisha vumbi na mawimbi juu ya bahari hiyo.
  Alisema kwa jana walitarajia upepo mwingine wenye kasi ya kilometa 20 hadi 30 kwa saa kwenye ukanda wa Bahari ya Hindi, lakini hali ikawa tofauti.
  Hata hivyo, aliongeza kuwa kutokana na hali ya hewa kwa siku mbili hizo kuwa tete hali sasa ni shwari.
  Kutokana na maafa ya Zanzibar, TMA ilitoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri wa majini kupata taarifa za mara kwa mara za mwenendo wa hali ya hewa.
  Alisema hatua ya kupata taarifa za mara kwa mara zitasaidia kwa kiasi kikubwa kufahamu hali ya hewa na mwenendo wa upepo kwa siku husika kabla ya safari zao.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 10. s

  sawabho JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Mungu asisingiziwe hata katika makosa ambayo ni uzembe wa binadamu mwenyewe. Kama Mungu kampatia binadamu akili, ni kwa nini huyu binadamu ambaye anahusika na hali ya hewa hakutoa tahadhari ya meli kutoanza safari, maana amepewa akili na Mamlaka ya kutabiri wa hali ya hewa ? Aidha, ni kwa nini huyo binadamu anayehusika na maafa na uokoaji hakufika mapema eneo la tukio kwa kutumia teknolojia ya kisasa ?
   
 11. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Harakisheni kuchangia na mtoe mawazo yenu yasikike leo kwani kesho hamtaruhusiwa tena maana kesi itakuwa imefunguliwa mahakamani
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,747
  Likes Received: 82,686
  Trophy Points: 280
  Kuzama Mv Skagit, ziri nzito yafichuka *Yadaiwa usalama wake ulikuwa mdogo *Serikali Z'bar yabebeshwa lawama *Maiti 58 zaopolewa, 128 wanasakwa *Bunge laomboleza, bendera nusu mlingoti siku 3


  Na Benedict Kaguo, Dodoma
  Majira

  MBUNGE wa Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Bw. Haji Khatib Kai (CUF), amefichua siri nzito ya kuzama meli ya Mv Skagit na kudai kuwa, tayari ilifungiwa isifanye kazi ya kubeba abiria kutokana na ubovu uliokithiri lakini wamiliki wake wameihonga fedha Serikali ili iendelee na kazi.


  Akizungumza na Majira jana, Bw. Kai alisema katika ripoti ya uchunguzi wa ajali ya Meli ya Mv Spice Islander I, ambayo ilizama miezi 10 iliyopita, tume iliyoundwa ilitoa mapendekezo kadhaa likiwemo la kuzuia meli zinazomilikiwa na Kampuni ya Seagul ikiwemo Mv Skagit (iliyozama) na kusababisha vifo.


  Alisema inasikitisha kuona meli hiyo imeachwa ifanye kazi ya kubeba abiria wakati uchunguzi tume ilishaagiza meli za kampuni hiyo zifungiwe kwa sababu zimekuwa zikizima na kupoteza uelekeo baharini.

  "Inavyoonekana, wamiliki wa kampuni hii wametoa hongo ili meli zao ziruhusiwe kubeba abiria hata kama hazifai hivyo ajali hii ilitegemewa kabisa kwa siku za usoni na kuua watu wasio na hatia.

  "Tukio hili si la bahati mbaya kwani tayari Mamlaka ya Hali ya Hewa ilishatoa tahadhari juu ya kuchafuka kwa bahari, iweje meli hii iruhusiwe kuondoka kwenda Zanzibar kwa sababu ya kutaka fedha na kusababisha maafa kama haya," alihoji Bw. Kai.

  Kwa Upande wake, Mbunge wa Konde, Bw. Khatib Said Haji (CUF), alisema ajali hiyo ni matokeo ya Serikali kushindwa kuchukua hatua stahiki za kulinda maisha ya raia wake.

  Alisema Zanzibar ni visiwa hivyo kwa vyovyote Serikali ilipaswa kuweka mfumo mzuri wa vyombo vya usafiri majini lakini imekuwa ikifumbia macho hali hiyo kwa kisingizio cha ufinyu wa bajeti.

  "Ni takriban mwaka mmoja tangu janga kama hili litokee, ilikuwa fundisho kwa Serikali ambayo ilipaswa kuchukua hatua stahiki za kuokoa maisha ya watu...hii ni makusudi ya Serikali kutochukua hatua ili kulinda maisha ya raia wake," alisema.

  Aliongeza kuwa, kitendo cha Serikali kutolinda raia wake kwa kisingio cha ufinyu wa bajeti, umefika wakati wa Baraza la Wawakilishi liiwajibishe Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

  "Majanga kama haya yanawafanya wananchi wapoteze imani na Serikali yao kwani tunakumbusha makovu ya ajali ya mwaja jana ambayo watu hawajaisahau," alisema.

  Mbunge wa Kisarawe, Bw. Suleiman Jaffo (CCM), alisema wanaohusika na vyombo vya majini wawajibike kwa kashfa hiyo kabla ya kusubiri wananchi kuwanyooshea vidole.

  Alisema uzembe wa usimamizi wa vyombo vya majini unaonekana kuota mizizi ambapo Serikali bado haijaweza kuweka mkakati wa kukabiliana na majanga.

  Mbunge wa Viti Maalumu Bi. Magdalena Sakaya (CUF), alimtaka Rais Jakaya Kikwete kuivunja Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), kwani imeonesha kushindwa kusimamia vyombo vya majini hivyo kusababisha maafa.

  Alisema viongozi wa SUMATRA, wameshindwa kazi na kutilia shaka uteuzi wao kuwa huenda haukizingatia sifa ila masuala ya kisiasa ndio maana wanashindwa kutekeleza majukumu yao.

  "Watu wanasafirishwa kama magogo, hakuna usimamizi makini, Serikali imekuwa ikichukulia mambo kirahisi tu…ajali za Mv Bukoka, Mv Spice Islander I, zilitosha kabisa kuwa fundisho," alisema Bi. Sakaya.

  Mbunge mwingine wa Viti Maalumu Bi. Christowaja Mtinda (CHADEMA), alisema ajali hiyo imechangiwa na Serikali kutosikiliza ushauri wa wabunge.

  "Kwa muda mrefu wabunge wamekuwa wakilalamikia vyombo vya usafiri kama ndege na meli lakini Serikali bado inarudusu kuingizwa mitumba, wakati tunapitisha Sheria ya Manunuzi, tulikataa vyombo vya mitumba visinunuliwe kwani haya ndio madhara yake iwe kwa watu binafsi au serikalini, tununue meli mpya sio mitumba," alisema.

  Alisema meli hiyo inapandwa na wananchi wa kipato cha chini kutokana na ubovu wake ambapo Serikali imekuwa ikiona na kushindwa kuchukua hatua.

  Spika Makinda aahirisha Bunge

  Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda, jana ameahirisha kikao cha bunge na kueleza kuwa, posho za wabunge wote zitapelekwa kwa waathirika wa ajali ya Meli ya Mv Skagit, iliyozama juzi eneo la Chumbe Zanzibar, kama rambirambi.

  Bi. Makinda alitangaza uamuzi huo baada ya wabunge kuingia ukumbini, kusomwa dua ya kuliombea Bunge na kumwita Waziri wa Nchi, Sera Uratibu na Bunge, Bw. William Lukuvi, ambaye alitoa taarifa ya Serikali kuhusu tukio la kuzama kwa meli hiyo.

  Alisema taarifa za awali hadi kufikia juzi jioni, zinasema meli hiyo ilibeba abiria 290 ambapo kati ya hao, watu wazima walikuwa 250, watoto 31 na wafanyakazi tisa wa meli hiyo.

  Aliongeza kuwa, hadi jana asubuhi watu waliokuwa wameokolewa wakiwa hai ni 146 ambapo jumla ya maiti 31, ziliopolewa na zote zimetambuliwa na ndugu zao.

  Bw. Lukuvi alisema, miongoni mwa waliookolewa wako watalii 16 ambapo mmoja aliopolewa akiwa amekufa na watu wengine 113 wanaendelea kutafutwa ambapo shughuli za uokoaji zilisimama
  jana kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa baharini.

  Kutokana na tukio hilo, Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo na bendera zote zitapepea nusu mlingoti na kuwataka wakazi wa Bara, wafike Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kupata taarifa za ndugu zao waliokuwa katika meli hiyo.

  Baada ya taarifa hiyo, Bi. Makinda alisemama na kueleza kuwa tangu kutokea kwa ajali hiyo juzi, wabunge 18 walisafirishwa kwenda Zanzibar kuungana na wananchi na kundi jingine la wabunge limeondoka jana.

  "Tulidhani kutakuwa na mazishi ya halaiki lakini Serikali ya Zanzibar imesema bado kwani maiti nyingi zimetambuliwa na ndugu zao na idadi ya watu ambao bado hawajapatikana ni kubwa.

  "Kwa hali hiyo, hatuwezi kukwepa kuwepo kwenye mazishi ya
  halaiki...sasa naahirisha bunge hadi kesho saa tatu asubuhi," alisema.

  Nje ya ukumbi wa Bunge, Bw.Lukuvi alikutana na waandishi wa habari na kuwasilisha taarifa ya Rais Jakaya Kikwete ambaye ametoa salamu za rambirambi na kuwataka wananchi wawe na subira wakati huu ambao kazi ya uokoaji inaendelea.

  Alisema uchunguzi wa kina wa tukio hilo unafanyika ili ifahamike nini kilichangia ajali hiyo ambapo kazi ya uokoaji bado inaendelea kufanywa na kwa ushirikiano wa Vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), KMKM, Polisi na wananchi.

  Alisema taarifa za watalii hao zinaendelea kufuatiliwa kwani hadi sasa haijafahamika ni raia wa nchi gani.

  Maiti zaidi zapatikana

  Hadi jana jioni, miili ya watu 58 ilipatikana baada ya kuopolewa katika eneo la tukio kukiwa na matumaini ya kupatikana wengine 124, ambao hadi sasa hawajulikani walipo.

  Juhudi za kuokoa abiria waliozama, jana ziliingia siku ya pili. Mwandishi wetu aliyepo Zanzibar, alisema kazi ya uokoaji bado inaendelea ingawa hadi jana jioni hakuna aliyepatikana akiwa hai.

  Mganga Msaidizi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Dkt. Abdurahaman Khalfan Said, alisema juzi walipokea majeruhi 145, wa ajali hiyo kati hao, 22 ndio wanaoendelea na matibabu ambapo wengine walitibiwa na kuondoka.

  Alisema kati ya watu walioruhusiwa baada ya kupata matibabu, sita hawana ndugu Zanzibar, hivyo wanaendelea kubaki hospitalini hapo wakati taratibu zingine zikiendelea.

  Dkt. Said alisema walipokea miili ya watu 20, mmoja alikuwa raia wa Israel, wawili Tanzania Bara na mmoja Mwera, Unguja.

  Katika hatua nyingine, yalitokea malalamiko ya wapigambizi wa kujitolea wakidai kuwa wameshindwa kwenda eneo la tukio kutoa msaada kutokana na kukosa mafuta.

  Kwa upande wa wananchi, baadhi yao wameilalamikia Serikali kwa kuchelewa kupeleka waokoaji eneo la tukio kwa sababu ya kuchelewa kupatikana kwa mafuta.

  Walitoa mwito kwa Serikali kuhakikisha matukio ya ajali za aina hiyo hayatokei tena.

  SUMATRA yatoa taarifa

  Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), jana imetoa ufafanuzi wa ajali hiyo.

  Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Ofisa Uhusiano wa SUMATRA, Bw. Devid Mziray, alisema meli hiyo inamilikiwa na Kampuni ya Seagul Transport.

  Alisema usajili wa meli hiyo ulifanyika katika Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) na ina uzito wa (GRT) 96.

  Aliongeza kuwa, cheti cha ubora wa meli hiyo kimepatikana Agosti 24, 2011, kinamalizika Agosti 23, 2012 na ina uwezo wa kubeba abiria 300 wakati mizigo ni tani 26

  "SUMATRA kupitia Kituo cha Utafutaji na Uokoaji-MRCC, ilipata taarifa kuwa meli hii ambayo ilikuwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar, inazama kwenye karibu na Kisiwa cha Chumbe, Zanzibar, eneo ambalo lipo umbali wa kilomita za bahari 13.8 kutoka Bandari ya Zanzibar," alisema Bw. Mziray.

  Alisema baada ya kupata taarifa hizo, kituo cha MRCC kilitoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama na vyombo vya usafiri majini ambavyo vilikuwa karibu na eneo la tukio.

  Bw. Mziray alisema meli hiyo iliondoka bandari ya Dar es Salaam saa 06.05 mchana ikiwa na abiria 248, watoto 31 na mabaharia tisa kwa mujibu wa orodha ya abiria.

  Taarifa za ajali hiyo zilisambazwa kwa wadau mbalimbali wakiwamo Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Kikosi cha Polisi cha Maji, Kikosi cha Wanamaji, Vituo vya Ishara Zanzibar (Signal Station) na Shirika la Bandari Zanzibar.

  "Kazi ya uokoaji inaendelea katika eneo la tukio kwa msaada wa vyombo mbalimbali zikiwamo boti za Mv Flying Horse, Mv Kilimanjaro III, Tug Bandari ya Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar I, Polisi, boti za doria, Kikosi cha Wanamaji na Kituo cha MRCC ambacho kinaendelea kufuatilia na kutoa taarifa ya uokoaji.

   
 13. B

  BULOLE BUKOMBE JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwa jibu Mkuu wa Mkoa yuko sahihi kwa sababu uzoefu unaonesha kwamba yanapotokea majanga makubwa kama hilo system huficha idadi ya waliokufa na idadi kamili ya wahanga wa tukio lakini kwa sasa inaonekana system haiko well coordinated kila upande unatoa data zake bila kuwasiliana na upande mwingine hata hivo ukisikia watu kumi na wawili wamekufa kama ilivyotokea Geita hivi karibuni ongeza watano watakao kuwa wamefichwa kwa sababu za wakubwa na RC DAR alitumia kanuni hiyohiyo kwani anajua utaratibu wao huwa wanafanyaje!! Hapo pekundu umegusa kwenye focal point watu wengi wamekuwa wakimsingizia Mungu kila jambo baya linapotokea hasa vifo kuwa ni kazi ya Mungu, Mungu akuumbe wewe tena Mungu huyohuyo akuue wewe hivi angekuwa hataki uwepo hata hiyo mimba yako isingetungwa, Tusihalalishe uzembe kwa kumsingizia Mungu kila jambo na ndiyo maana tumepewa akili ya kupambanua mazuri na mabaya. Ununue meli mbovu na hauweki standby kikosi cha uokoaji leo maafa yakitokea utasema kazi ya Mungu?
   
 14. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ukos sahihi Mkuu. Mwaka mmoja haujatimka tangu ilipokua ajali kama hii, badala ya kujifunza kwa makosa hatufanyi lolote kwa sababu Mungu yupo. Siku Watanzania tukiamua tutawaondosha hawa katika viti vyao vya usungizi.
   
 15. B

  BULOLE BUKOMBE JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu MAMMAMI Ninakushukuru kwa kuniunga mkono jitahidi kuwaelimisha na wenzetu wasiaminishwe mambo ya uwongo kuhalalisha uzembe.
   
 16. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #16
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  kwa maelezo yaliyo na rangi ya BLUE moja kwa moja serikali zote mbili zinahitajika kuwajibika kwa uzembe huu uliopoteza maisha kwa hawa wapendwa wetu,na kila upende uwajibike katika nafasi yake
  Tukianzia na:-
  1. IKULU (USALAMA WA TAIFA)
  2. TAKUKURU
  3. SUMATRA
  4. WIZARA YA USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI
  Pia tungeomba ushirikiana kutoka kwa wabunge na kamati iliyoshiriki katika uchunguzi wa awali wa MV Spice watoe taarifa hiyo hadharani ili wananchi tupate kujua jinsi serikali hii isivyo jali kutekeleza taarifa mbali mbali za kamati zinazoundwa na kutumia fedha nyingi za serikali lakini mapendekezo yake huwekwa kapuni bila kufanyiwa kazi.
   
 17. The Eagle2012

  The Eagle2012 Senior Member

  #17
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  Naunga Mkono Hoja yako 100%
   
Loading...