Idadi Kubwa ya wanafunzi wa Form vi wakataliwa kufanya mitihani yao.

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1]
NECTA(10).jpg
[/h]Written by Ashakh (Kiongozi) // 25/11/2012 // Habari // 10 Comments


Kwa mujibu wa taarifa zilizoandikwa katika gazeti la Zanzibar leo la siku ya leo limekuwa na taarifa hii kwamba kuna idadi kubwa ya wanafunzi wa form six kutoka Zanzibar hawatoruhusiwa kufanya mitihani yao hapo mwezi wa February mwaka 2013 kwa sababu hawana sifa za kufanya mtihani huo.
Imeelezwa kwamba ili uweze kufanya mtihani wa form six inatakiwa mtihinawa awe na pass tano ikiwa ni pamoja na credit tatu.
Miongoni mwa wanafunzi kutoka skuli za Kiembe samaki, Hile, na hamamni ni miongoni mwa waliokumbwa na mkasa huo.
tayari barua rasmi kutoka NECTA wameshapelekewa wazee wa watotot hao kuthibitisha hilo. Mmoja wa wazee wa wanafunzi waliofikwa na mkasa huo amesema hakubaliani na hoja hiyo kwani mtoto wake aametimiza sifa zote na ndio alijiunga na form form iv, huku akiwa na B ya Kiswahili, B ya Dini na B ya Kiarabu.
Sakata bado linaendelea


[h=4]Related Posts[/h][h=3]KAMWE HAWATAACHA[/h]
[h=3]Govt to introduce anti cyber crime law[/h]

[h=3]Barua ya Wazanzibari kwa Amnesty[/h]


[h=3]Wapendekeza nafasi ya Makamu wa Rais ifutwe wakazi wa Dar[/h]

[h=3]Msaada unahitajika[/h]





[h=3]10 Comments on "Idadi Kubwa ya wanafunzi wa Form vi wakataliwa kufanya mitihani yao."[/h]


  1. pambanua 25/11/2012 kwa 11:27 mu · Ingia kujibu
    mi nataka wazuiwe kufanya mitihani wote si walijidai UAMSHO umewasababishia fujo hawawezi kufanya mitihani vizuri hao wazuiwe wote ndipo wazee wao watakapojua nini maana ya muungano.




  2. pambanua 25/11/2012 kwa 11:30 mu · Ingia kujibu
    halafu smz/wizaraya wizi elimu hiyo combination ya kiswahili, dini, kiarabu wazifute manake mwisho wa masomo watoto wanakosa pa kuelekea au kama wanahitaji ziwepo wawape uhakika watoto wa masomo ya juu yaani UNIVERSITY kwa kuwatafutia scholarship katika nchi zinazofundisha dini na kiarabu vyenginevyo tutakuwa na watoto wengi form four na six wa kombi hizo ambao hawana kwa kuelekea.




  3. Said-Said 25/11/2012 kwa 12:35 um · Ingia kujibu
    Assalam Alaykum,
    @ Ashakh na wazalendo.
    Binafsi nimeipokea taarifa hii kwa maskitiko makubwa sana, kwa hali halisi ilivyo na kwa jinsi NECTA kila mwaka inavyochakachua matokeo Wazanzibari wengi huambulia “C” tatu na kuendelea form V, kwahiyo mkasa huu utawakumba wengi katika wanafunzi wetu na kwa kweli hizi ni njama maalumu kutuzuia wazanzibari tukwame kielimu inasikitisha sana sana sana kuona kwamba wazazi tayari washatumia fedha zao na wanafunzi juhudi zao kwa ajili ya masomo, mtihani upo FEBRUARY 2013 hii ni NOVEMBER au NISEME DECEMBER TENA, (MIEZI MITATU KABLA YA KUFANYA MTIHANI) wanafunzi wanazuiliwa kufanya mitihani.
    Kwa ninavyoelewa mimi sheria hii imepita mwaka huu, na kama ni hivyo sio haki kuanza kuwabana wanafunzi ambao wao tayari waliingia form 5 kwa sheria iliyokuwepo ya inayowaruhusu wanafunzi wenye credit tatu kuingia form 5, binafsi hili nalipinga na si haki kabisa si kwa wazanzibari tu bali hata huko bara wanafunzi ambao wana credit tatu hawapaswi kuzuiliwa kufanya mitihani kwakua sheria hii imetungwa ilhali wao tayari wameshaanza masomo yao kidato cha tano.
    USHAURI.
    Nawaomba walimu wote wa form 6 kwa kushikiana na wazee na wanafunzi, na kwa kupitia wizara ya elimu ya ZANZIBAR kulipinga hili na kufuata utaratibu ili kuiambia NECTA kwamba sheria hii haipaswi kuwabana wanafunzi ambao tayari walishaanza masomo yao ADVANCE. na pia viongozi wakuu wa Nchi walitetee hili.
    Kila la kheri ndugu zangu, M/Mungu atatupa njia inshaallah, huo ndio MUUNGANO, hayo ndio MAPINDUZI DAIMA yaliyokuja kutangaza ELIMU BURE (Kwa maana hata ukisoma ni bure kama huna jamaa serikalini) leo tunajitutumua tunasoma hivyo hivyo wenzetu (watawala wetu) hawataki tufike vyuo vikuu tutaelimika na kuyasema wanayotufanyia.
    ZANZIBAR KWANZA.




  4. kingjokery 25/11/2012 kwa 12:52 um · Ingia kujibu
    mambo mengine tunawalaumu vichogo bure tu, nina uhakika hiyo mipango yote wahafidhina wa wizara ya elimu zanzibar wanafahamu vyema. ila kwa ushenzi wao waliamua kunyamaza kimya na ndio maana hawataweza kusema lolote kuwaambia lolote NECTA, kama hamusaidiki mpigieni simu abdalla mzee muone.




  5. Bosco 25/11/2012 kwa 1:10 um · Ingia kujibu
    Kwa kweli hizi taarifa mie nliziskia miezi kama 6 iliyopita ila sikuweza kuzithibitisha. Na kama ni za kweli mie pia naona ni bora mana hao wanafunzi hawana kheri hata moja. Kipindi kile cha fojo walihojiwa wanafunzi wa skuli ya kwerekwe wakasema eti uamsho inaleta fujo wao hawapati kusoma. Yule mwanafunzi akizungumza lafudhi ya kimakunduchi.
    Sasa wacha wakose sifa ndipo watakapo jua nini maana ya ukoloni kudadeki zao.
    Na wale wanaotegemea wizara ya elimu ya znz kupinga jambo hili wanajidanganya. Pale wema kuna watendaji wachoyo sana na wangependa wazanzibari wote wafeli.
    Nawashauri wanafunzi mujiunge na uamsho kudai uhuru nyie wapumbavu.




  6. Abdul 25/11/2012 kwa 1:33 um · Ingia kujibu
    tujitokeze kwa wingi kutoa maoni ya serekali mbili kwenda mojaaaaa mapinduzi daimaa




  7. mwanafunzi 25/11/2012 kwa 1:59 um · Ingia kujibu
    Kwanza poleni sana kwa hilo lakini hili ni viongozi wetu wanalisababisha. Hili suala lipo muda sasa na Wizara inafahamu kwamba sifa zinazotakiwa sasa ni kuwa na credits tano kwa kuanzia (C tatu na D mbili); na UAMSHO TAYARI WALILISEMA ZAMANI LAKINI KIONGOZI GANI ATAKAEWASIKILIZA.
    Pili Suala la elimu ya Sekondari si la Muungano lakini viongozi wetu kwa vile hawataki kujituma wanang’ang’ania tu libaki Tanganyika. Wawakilishi walipiga kelele sana mpaka jussa akakauka kifua angalau tuunde baraza letu la mitihani lakini WAziri gani wa CCM atakaekubali, sasa matokeo yake hayo.
    Binadamu hatakiwi kuingia katika shimo lile lile mara mbili, mwaka jana yaliyowapata wazanzibari tunayajua mwaka huu mambo ndio hayo, sasa hao wahusika nawatowe majibu ya msingi au watasema ni UAMSHO HAO NDIO WALIOSABABISHA?
    ALLAH TUNAMUOMBA ATUPE NUSRA.
    Wabillahi Tawfiq.




  8. mwanafunzi 25/11/2012 kwa 2:05 um · Ingia kujibu
    Ndugu Bosco nakuunga mkono kwa upande mmoja, kwani Wizara inayosimamia hili ingesimama kidete kabla jambo hili halijatokeza lakini kwa kuwa ni wachoyo wanaomba Muungu wanafunzi wote wafeli ili nafasi walizonazo wasijekuzikosa, sasa tuwaulize watakapozeeka nani ataendesha hii nchi.
    Sisi wengine ndio tulibahatika na ALLAH akatuongoza kipindi hicho mambo yalikuwa hayajakuwa mabaya kama leo, walimu wa sayansi walikuwa wanaonekana mashuleni. Leo walimu wote ni Dini NA kIARABU tutaelekea wapi? na ukijiunga na UAMSHO ndio mambo kama hayo mnaambiwa eti wachochezi, kwani niulize uchochezi unaokusudiwa maana yake mbona hawaisemi?




  9. pambanua 25/11/2012 kwa 2:51 um · Ingia kujibu bosco
    sawa sawa ndugu yangu mi nataka wazuiwe wote maadam nafanya shahada ya pili na karibuni namaliza potelea mbali, sisemi haya kwa kupenda sababu wanangu ndio kwanza na kama yataendelea yatawakumba pia lakini liwalo naliwe tulishasema haya siku nyingi lakini wapumbavu wanang’ang’ana na muungano utadhani wamepewa na ALLAH, binafsi mwaka 2009 nilipita sehemu kibao Unguja kuelezea ubaya wa muungano na katiba iliyopo siku moja nilihutubia madiwani na masheha halmashauri ya wilaya mkokotoni pale.
    diwani mmoja wa ccm anaitwa BABLA akaniuliza masuali kuhusi katiba na muungani nikafafanua vizuri hadi baadhi ya masheha akiwepo wa BUMBWINI akaja akanipongeza mwishi Babla alisema haizuru lakini muungano udumishwe hivyo hivyo,,sasa wazee kama hawa watoto wao ni kupigwa ziro tu watajifunza baadae, binafsi nimefanya kazi hata siku moja bado kidogo tu nipigwe na ffu na mgambo kisiwa cha tumbatu,,lakini ukiona watu hawaelewi waambiwalo waache wataona baadae.
    smz na harou ali sleimani waliharibu mfumo mzima wa elimu kwa kuanzisha form one zero ili watu wapelekwe tu hata kama hawana sifa waende wakafeli form four sasa ndio matokeo hayo,,ZAmzni ilikuwa kama hukupasi majaribio ya darasani hupelekwi darasa la juu leo watoto wanakwenda tu kama kuna beni la borafia silima. unafikiria nini matokeo hapo? waache wazuiwe watajijua.
    M/Mungu aliniamboa mimi kuwa kafiri hawezi mpendelea mema muislamu hata kama ni baba ako lakini kuna watu hapo akina stonetown kiongozi wanaona ccm na muungano kama dini,,WALLAHI naandika haya kwa uchungu mkubwa lakini acha liwe liwalo watoto wazuiwe wote pumbavu wakubwa,,ASOFUNZWA NA BABAYE NA MAMAYE HUFUNZWA NA ULIMWENGU ACHA ULIMWENGU UTUFUNZE….




  10. kingjokery 25/11/2012 kwa 4:13 um · Ingia kujibu
    tusiwalaumu watu tatizo ni letu wenyewe
    kwa miaka mini sana wazanzibari tumekuwa tukiwalaumu watu kwa matatizo yetu wenyewe. nakumbka hata ile siku ya uzinduzi wa kitabu cha maalimu seif na ali sultani bin issa dr. salim ahmed alieleza mambo ya msingi sana na kubwa zaidi akasisitiza matatizo mengi yanayotokea ni matokeo yetu sisi wenyewe wazanzibar na kwa hivyo tusiwalamu watu. kutokuwajibika kwa vioingozi wetu na kutoeleza wananchi juu ya mambo ya msingi yanayotokea huko kwenye vikao vyao ndio msingi mkuu wa matatizo yanayoibuka zanzibar. hili la ongezeko la qualification halikuibuka tu kama dondo wanaanguka wakati wa masika bali ni mpango mzima ambao viongozi wa wizara ya elimu wanalifahamu vyema lakini kwa ukorofi wao waliamua knyamaza kimya utadhani hawalipwi kutokana na jasho la wananchi. wizara ya elimu imeoza tena ndo wizara inayonuka kwa kila aina ya uvundo na kama shein hakuwang’oa wale wazee hakuna mageuzi ya elimu yatapatikana pale. abdala mzee ni hafidhina tena amechoka kabisa, katibu mkuu bi mwanaidi alishastaafu karejeshwa tena sasa vizee kama hawa unatarajia utendaji wa aina gani hapo kama si uozo! nyie mtazameni shamuhuna alivyochoka! eti ndo waziri wa elimu ha! jamani ivi hakuna vijana hapa mbona shein unatuzingua ili tuwaone NECTA wabaya bure kumbe nyie ndo wabaya! kuna yule load Kombo ambaye ameshastaafu lakini karejeshwa tena kuwa mwenyekiti wa bodi ya mikopo zanzibar, yaani mtu anajulikana na kila mtu kwa ukorofi na rorho mbaya hata omari mapuri alimshinda akamrejesha elimu alipokuwa naibu waziri kiongozi! lol! hao ndio viongozi wenyewe wa elimu. yagujuuu hamna cha elimu wala nini bila kwangoa hao.
    Moved by admin

 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom