Idadi kubwa ya Waislam (99%) inaweza kuwa kikwazo cha Uturuki kutokuwa mwanachama rasmi wa EU?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari za muda huu ndugu zangu wa JamiiForums

Je, idadi kubwa ya waumini wa dini ya kiislam (99%) inaweza kuwa ndio kikwazo kikuu cha nchi ya Uturuki kutokuwa mwanachama kamili/rasmi wa E.U mpaka sasa?

Walikubaliwa haraka kujiunga NATO kwa maslahi ya kijeshi kama daraja la Wazungu kuingia Middle East? Uturuki kama mwanachama wa NATO aliruhusu jeshi la Marekani kutumia anga lake wakati wa vita vya kumpiga Saddam Hussein mwaka 2003.

turkey.jpg


Waliruhusu anga lao kutumika kupitisha ndege vita za Marekani lakini wakakataa Marekani kuweka kambi katika ardhi yao kwa lengo la vita ile.

Muungano wa umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi yaaani NATO ulianzishwa baada ya Vita vya pili vya dunia. Kusudi lake lilikuwa kupata amani huko Ulaya, kukuza ushirikiano kati ya nchi wanachama wake na kulinda uhuru wao - yote haya ilikuwa katika hali ya kukabiliana na tishio lililokuwapo kwa wakati huo kutoka kwa Umoja za Kisovieti (USSR).

Mkataba wa uanzishaji wa Muungano huo ulisainiwa jijini Washington nchini Marekani mnamo mwaka wa 1949 na nchi kadhaa za Ulaya pamoja na Amerika Kaskazini. NATO inawapa Washirika wake uhakika wa kuwa na serikali za kidemokrasia, uhuru wa mtu binafsi na utawala wa sheria, na vile vile utatuzi wa mizozo kwa njia za amani. Muhimu zaidi ni kwamba, mkataba huo unaweka wazi wazo la ulinzi wa pamoja, ikimaanisha ya kwamba "kuwa shambulio dhidi ya mshirika mmoja linachukuliwa kama shambulio dhidi ya Washirika wote".

Kwa sasa, NATO ina wanachama wapatao 30. Mnamo mwaka 1949, kulikuwa na wanachama 12 waanzilishi wa umoja huu yaaani Ubelgiji, Canada, Denmark, Ufaransa, Iceland, Italia, Luxemburg, Uholanzi, Norway, Ureno, Uingereza pamoja na Marekani. Nchi nyingine wanachama ni Uturuki (1952), Ujerumani (1955), Uhispania (1982), Jamhuri ya Czech, Hungary na Poland (1999), Bulgaria, Estonia, Latvia, Lithuania, Romania, Slovakia na Slovenia (2004), Albania na Croatia (2009), Montenegro (2017) na Macedonia Kaskazini (2020).

Jamhuri ya Uturuki iko kwenye peninsula moja maarufu sana ya Anatolia magharibi mwa Asia na mkoa mdogo wa Kusini Mashariki mwa Ulaya. Jirani kabisa ya Uturuki kwa upande wa kaskazini magharibi ni nchi ya Bulgaria; Ugiriki ikiwa magharibi; Armenia, Azabajani na Iran upande wa mashariki; Georgia upande wa kaskazini mashariki; Syria upande wa kusini; na Iraq upande wa kusini mashariki.

Uislamu ndio dini kubwa zaidi nchini Uturuki kulingana na takwimu za serikali, na 99.8% ya watu hapo awali walitambuliwa na serikali kama Waislamu na asilimia iliyobaki ya 0.2 ni Wakristo au wafuasi wa dini zingine zilizotambuliwa rasmi kama Uyahudi.

Uturuki ni mmoja wa washirika wakuu wa EU (kumbuka kuwa mshirika sio mwanachama) na wote ni wanachama wa Umoja wa Forodha (European Union–Turkey Customs Union). Uturuki ilisaini makubaliano ya Jumuiya ya Forodha na EU mnamo mwaka 1995 na ilitambuliwa rasmi kama mgombea wa uanachama kamili mnamo tarehe 12 mwezi Desemba mwaka 1999, katika mkutano wa huko Helsinki wa Baraza kuu la Ulaya.

Mazungumzo ya uanachama kamili yalianza tarehe 3 mwezi Oktoba mwaka 2005. Nchi zingine zinazotafuta kuwa wanachama wa EU ni zile zilizo katika mchakato wa 'kubadilisha' (au kujumuisha) sheria za umoja huo wa Ulaya (EU) kuwa sheria ya kitaifa ndani ya nchi zao. Nchi hizi ni pamoja na:

(1) Turkey
(2) Albania
(3) Montenegro
(4) North Macedonia
(5) Serbia

Tangu mwaka 2016 hadi leo hii 2021, mazungumzo ya kutanganzwa kuwa mwanachama kamili/rasmi yamekwama. Kwanini Umoja wa Ulaya (EU) unasita kuipa uanachama kamili/rasmi nchi ya Uturuki? Je, sababu kuu inaweza kuwa ni idadi yake kubwa ya waumini wa dini ya kiislam?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya wadau;
==========
Kwa Marekani kama superpower, kwake malengo ya NATO hayakuwa hayo uliyoainisha hapo juu. Hayo malengo hapo juu Marekani aliyatumia kuzirubuni nchi za ulaya zikubaliane na kuanzishwa kwa NATO.

Marekani aliweka msukumo kuanzishwa kwa NATO ili kui-control Eurasia militarily kwa kutumia remote control inaitwa NATO. Kwa zama za vita baridi, ili kui-control Eurasia, ilikuwa ni lazima udhibiti Ujerumani isiamke tena kijeshi baada ya mtiti wa WW2 na vilevile kuzuia kuenea kwa nguvu za Usovieti(baadae Russia)ndani ya Eurasia. Kwahiyo, kwa kiingereza wanasema The US NATO Objective were to keep the Germans down and Russians out!
==========
Ukweli ni kwamba kijiografia eneo la Uturuki lipo katika mabara mawili, kuna eneo lipo Ulaya na kuna eneo lipo Asia.

Tukija kwenye hoja ya kujiunga katika Umoja wa Ulaya, ni wazi kuwa umoja huu umejengwa chini ya mikataba ya haki za binadamu zinazotambua usawa kwa kila binadamu. Uturuki ina waislam wengi, ndani ya uislam hakuna usawa wa mwanamke na mwanaume.

Kwa muda mrefu Uturuki imekuwa ikitaka kujiunga na huu umoja ila sharti lilikuwa ni kurekebisha sheria zake ili ziendane na zile za umoja wa Ulaya.

Ila kuna hoja iko hapa, members wa EU wana uhuru wa free movement kwa wananchi wa nchi husika, ukimruhusu Turkey kuwa mwanachama, waarabu wanavyopenda Ulaya watakuwa wamepata daraja, hivyo lazima ipigwe spana kwanza.
==========
 
Ila naona kama Erdogan ameanza kushtuka flank hivi kuanza relation na Russia.

Pia kipnd cha COLD WAR USA ILIPELEKA MILLITARY BASSES ZAKE TURKEY ILI KUMUOGOPESHA. USSR

HADI USSR NAYO IKA REVENGE KWA KUPELEKA MILLITARY BASES
CUBA

SO TURKEY AMEANZA KUTUMIKA KITAMBO SANA
 
Back
Top Bottom