FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,416
- 7,828
Idadi kubwa ya wahamiaji wakamatwa katika mji wa Mississippi Marekani
Katika harakati za kupambana na uhamiaji haramu maafisa wa uhamiaji wa Marekani wamewakamata karibu wahamiaji 700 wasiokuwa na vibali halali katika mji wa kusini wa nchi hiyo wa Mississippi.
Mwendesha mashtaka wa umma amesema watu hao 680 wamekamatwa baada ya uvamizi uliofanywa katika viwanda vinavyotengeza chakula.
Kiasi kikubwa cha waliokamatwa ni raia wa Amerika ya Kusini. Maafisa wa uhamiaji nchini humo wanasema huenda ikawa hiyo ndiyo idadi kubwa zaidi ya wahamiaji kukamatwa katika jimbo moja la Marekani.
Mapambano dhidi ya wahamiaji haramu ni mojawapo ya ahadi kuu alizotoa Rais Donald Trump wakati alipokuwa anachukua mamlaka.
DW | CNN | Los Angeles Times