Idadi ipi ya watoto inafaa kwa uzao wa zama hizi?

Mwatulole

Member
Oct 16, 2017
54
191
Habarini ya leo wana JamiiForums wenzangu,

Mimi ni kijana, niliekuwa na mtazamo wa kuwa na mtoto mmoja tu na tulikubaliana na mwenzangu tumeweza kumaintain hii hali kwa miaka tisa lakini juzi mke wangu hajaziona siku zake.

Kaenda kupima kakutwa anaujauzito kwa kweli hakuna namna nimezipokea taarifa hizo kwa mikono miwili japo mpango wangu ilikuwa ni mtoto mmoja.

Naomba kujua standard ya zama hizi ni watoto wangapi kwa uzao wa ambao hawawezi kukupa wakati mgumu wa malezi.
 
mfumo wa dunia unataka mtoto mmoja kwa familia, ila mfumo wa kiafrika ni si chini ya watoto 5 kwa familia. Kwa hiyo chagua mfumo mfumo unaokufaa
 
Habarini ya leo wana jamii forum wenzangu mimi ni kijana, niliekuwa na Mtazamo wa kuwa na mtoto mmoja tu na tulikubaliana na mwenzangu tumeweza kumaintain hii hali kwa miaka tisa lkn juzi mke wangu hajaziona siku Zake kaenda kupima kakutwa anaujauzito kwa kweli hakuna namna nimezipokea taarifa hizo kwa mikono miwili japo mpango wangu ilikuwa ni mtoto mmoja, naomba kujua standard ya zama hizi ni watoto wangapi kwa uzao wa ambao hawawezi kukupa wakati mgum wa malezi ?.
Hakunaga formula mkuu ktk suala hili,kama una uwezo wa kuwahudumia fresh piga hata 50 mana badae ndo watakuja kuwa wasaidizi wako pindi utakapokuwa hujiwezi (watoto wako ndio msaada pekee hapo baadae,ndugu sio wa kuwategemea sana zama hizi)
 
Back
Top Bottom