Ice cream zitokanazo na maziwa ya mama zauzwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ice cream zitokanazo na maziwa ya mama zauzwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanaweja, Feb 26, 2011.

 1. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ice Cream zitokanazo na maziwa ya Mama zauzwa 25/02/2011

  Mgahawa mmoja mjini London nchini Uingereza kwa jina, Convent Garden, umeanza kuuza 'ice cream' zilizotengenezwa kwa maziwa ya binadamu.

  Ice cream hizo zilizopewa jina la "Baby Gaga" zimetengenezwa kwa mara ya kwanza kutokana na maziwa ya Mama mmoja wa mjini London, Victoria Hiley, 35.

  Zoezi la kukamua na kujitolea maziwa Mama Hiley lilifanyika katika mgahawa huo na kupitishwa kwa viwango vinavyokubalika kabla ya kuwekewa vikorombwezo kama vile Madagascan vanilla pods na ladha ya limao.

  Mwenyewe, Mama Vicroria Hiley anasema kuwa ikiwa maziwa ya mama ni mazuri kwa watoto, basi ni mazuri pia kwa kila mtu, ingawaje wapo watakaosikia kuhusu hilo na kung'aka, 'yuck', lakini wafahamu kuwa ni maziwa asilia, yanapatikana bwerere na yasiyokuwa na virutubisho vya kimaabara.

  Kwa sasa, ice cream ya Baby Gaga inauzwa kwa pauni za Uingereza £14 (sawa na dola za Marekani $23) kwa kipimo na Bi. Hiley anajipatia kitita cha £14 kila wakia 10 za maziwa anayotoa (wakia ni tafsiri ya neno la kiingereza "ounce" linalotumika kwa vipimo vya uzito). Mwenyewe Hiley anauliza, 'upo ubaya gani kutumia mali zangu kujiongezea kipato?' Anaongeza kusema kuwa, 'Endapo watu wangefahamu thamani ya ladha ya maziwa ya mama, basi akina mama wengi wasionyonyesha wangehamasika kunyonyesha watoto wao'.

  Mvumbuzi wa ice cream Matt O'Connor aliweka tangazo katika tovuti ya wakina mama, Mumsnet, akiwasihi wakina mama wajitolee maziwa yao kwa ajili ya kutengenezea ice cream. Watu 15 walijitolea. O'Connor anayo imani kubwa kuwa 'recipe' yake hii itapata mafanikio makubwa. Anadai kuwa hakuna mtu yeyote amejitahidi kuweka 'masham sham' kwenye ice cream kwa kipindi cha miaka mia moja iliyopita. Anasema Baby Gaga ni ladha moja, watu watarajie ladha zaidi...

  Ipo video ya watu waliohojiwa kuhusiana na 'ice cream' hiyo ya aina yake. Bofya hapa kuitizama katika tovuti ya BBC.

  Unaweza pia kusoma zaidi juu ya hili na mengine mengi kupitia tovuti ya Baby-Gaga.
  from: - Habari
   
Loading...