Biashara ya kutengeneza na kuuza "Askrimu" (Ice Lollies)

Habari za kwenu wana jamvi,

Nimeona fursa na ninataka niitumie katika mji jirani na hapa nilipo, ni biashara ya Ice cream/koni. Naombeni wajuzi mnifahamishe upatikanaji wa mashine za kutengenezea kwa urahisi, kitu gani kina hitajika ikiwemo leseni na mengineyo,pia ningependa pia nifahamishwe jinsi ya kupata zile fridge za Azam au kampuni nyingne zozote ambazo zinauza Ice cream ili kama nikifanikisha biashara hyo niwe pia wakala wa kuuza Ice cream za Azam/kampun nyingne pia.

Asanteni
 
Koroga uji wa ngano ukianza kuiva iva changanya unga wa ubuyu vichemke kwa pamoja mpaka viive. Ila uwe unapitisha mwiko mara kwa mara ili visiungue. Nilishafanya hii biashara na inalipa vibaya
Hawatakwenda msala mkuu
 
Unapika uji wa ngano kwenye sufuria ila uwe mwepesi halafu unachukua uji unachanganya kwenye ubuyu uliouloweka na maji ya moto then unakoroga baada ya hapo unafikisha kutoa mbegu then inakuwa tayari
Nsemwas naomba uniandikie vipimo mfano kupata ice cream mia unatumia kiasi gani cha ubuyu,ngano sukari maji n.k
 
Koroga uji wa ngano ukianza kuiva iva changanya unga wa ubuyu vichemke kwa pamoja mpaka viive. Ila uwe unapitisha mwiko mara kwa mara ili visiungue. Nilishafanya hii biashara na inalipa vibaya
Hapo ratio ya unga sijui inakuaje babe!
 
Kumbe wauza lamba lamba mpo wengi humu,hii biashara inalipa ukipata lokesheni nzuri za kuuzia.
Wengi wenu mnafeli kwenye vifungashio,igeni mfano wa azam hata kama unatumia vifuko tafuteni vipakti vizuri vinavyovutia
Tupe mfano wa ivo vimfuko plse
 
Nsemwas Junior,

Mahitaji
(kwa mahitaji haya utatoa zaidi ya pisi 200 za barafu ukitumia vifuko vya size 1¼ X 10)
Maji lita 7
Maziwa ya unga 1 cup (brand yoyote)
Unga wa wanga (corn starch) 2 cups uchanganye na maji lita 1.5 (unga wa wanga unauzwa supermarket) au sokoni unga wa ubuyu
Sukari kilo 1¾ (waweza punguza)
Chumvi ½tsp (ukipenda)
Utaweka ladha uipendayo (vanilla, mango, chocolate, pineapple, nk) Mifuko 300 ya kufungia ice candy (mifuko ya barafu)

HATUA:
1. Weka maji lita 7 kwenye sufuria kubwa na weka jikon yachemke, ongeza sukari na chumvi(ukipenda), kisha changanya vizuri hadi viyeyukie humo .
2. Ongeza ile corn starch na maziwa ya unga kwenye hayo maji yanayochemka, koroga vzr ili kusitokee mabujabuja, chemsha kwa dk 8, kisha zima jiko, acha ipoe kwa saa kadhaa kisha ongeza ladha uipendayo.
3. Funga kwenye vile vifuko na gandisha hadi ziwe barafu.

Kwa hisani ya Numbisa Jinsi ya kutengeneza barafu za kula, ice crem
 
Ni vyema kufungia vifuko vya karanga. Mfuko upo kwenye rola haina usumbufu katika kujaza. Unafunga kwa mashine zinauzwa 50,000 zinatumia umeme. Hizi ni za kuchomea tu.
 
Ni vyema kufungia vifuko vya karanga. Mfuko upo kwenye rola haina usumbufu katika kujaza. Unafunga kwa mashine zinauzwa 50,000 zinatumia umeme. Hizi ni za kuchomea tu

Those days tulitumiaga Kibatari. challange ya hiyo mashine ni ngumu kupack tight than kufunga na mkono.
 
kwahiyo tofauti na ubuyu au ukwaju,kuna ice cream gani nyngine mtu anaweza kutengeneza?na je unga wa ngano unahusika kotekote?

Corn starch, cornstarch, cornflour or maize starch or maize is the starchderived from the corn (maize) grain. The starch is obtained from the endosperm of the kernel. Corn starch is a popular food ingredient used in thickening sauces or soups, and is used in making corn syrup and other sugars.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom