ICC yamzuia Gbagbo kuondoka nchini Uholanzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279

Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai Icc, iliyoko huko The Hague, Uholanzi imemzuia rais wa zamani wa Ivory Coast,Laurent Gbagbo, kuondoka nchini humo licha ya kuachiwa huru.

ICC imemzuia Gbagbo kuondoka Uholanzi, akiwa anajiandaa kurejea nchini mwake, baada ya waendesha mashtaka katika mahakama hiyo kukata rufaa dhidi ya kesi inayomkabili ya kuhusika na makosa ya uhalifu wa kivita nchini mwake.

Gbagbo anatuhumiwa kutenda kosa hilo miaka minane iliyopita, mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Ivory Coast uliompatia ushindi mpinzani wake mkuu Alsane Outtarra, na yeye kukataa kuondoka madarakani.

Askari waliokuwa wakimuunga mkono mwanasiasa huyo walipita nyumba kwa nyumba kuwasaka wapinzani wake na kuwaua pamoja na raia wa kigeni, hali iliyosababisha watu wapatao elfu tatu kupoteza maisha nchini Ivory Coast.

Wafuasi wa Gbagbo walionekana kushangilia, baada ya Icc kutangaza kuwa imemwachia huru mwanasiasa huyo, baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.

Hata hivyo baadhi ya watu ambao ndugu za walikufa wakati wa mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe nchini Ivory coast walionekana kukosa amani.

TBC
 
Stupid, ICC a failed mission!
 
Well, Gbagbo hata akitoka, it's worth it, kwani kuna kitu amejifunza na ni darasa tosha kwa wengine sampuli kama yake wanaojidanganya kuwa wao wako juu ya sheria.

Kutumia madaraka kunyanyasa watu ktk dunia ya leo ni kitu ambacho dunia ya wastaarabu haiwezi kuubali lazima uongoze watu kwa kufuata misingi ya haki na sheria.

Impunity has no justification and must be punished in the best possible manner. Mr. Gbagbo, there is something you've leant and we hope other dictators will borrow a leaf from your experience. Dictatorship never pays.
 
Ulishawahi kuona Bush ameshitakiwa huko baada ya kuivamia Iraq kwa mabavu akidai inavinu vya kurutubisha uranium ilhali hakuna, roho ngapi kapoteza zawatu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kutokukamatwa kwa bush kuna halalisha vipi mauaji aliyokuwa anafanya huyu raisi wa ivory coast ??

Unataka kuniambia mtu akiua na asipokamatwa ni Ishara ya wewe pia uue na hutashtakiwa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom