ICC na kesi za vurugu: Waafrica waandame kupinga viongozi wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ICC na kesi za vurugu: Waafrica waandame kupinga viongozi wao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shiefl, Feb 5, 2011.

 1. S

  Shiefl Senior Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hii imenisikitisha sana kusikia eti viongozi wa Africa wanakubali eti hawa jamaa wa kenya hata kama hawajahusika wadifikishwe The Hague.
  Huu kwa mtazamo ni ule ule uzandiki wa viongozi wa Africa kutotaka kutenda haki daima na kuendelea kuwakandamiza wananchi wao na democrasia ya kweli. Imeonesha ni jinsi gani viongozi wa Africa wanalindana hata katika mambo ya kishenzi kama ya uchaguzi wa Kenya ambapo watu kwa makusudi kabisa walifanya uhalifu wakakataa kuunda mahakama yao mpaka Mremo Ocampo alipoingilia kati.

  Kuna haja gani ya watu kusababisha mauaji na kuwalinda kwa nguvu zote? Kwani ICC inahukumu kwa hila? Kama ndio si iwe hoja na si kutetea wahalifu? Ukiangalia utagundua kuwa akili za viongozi wetu zinawaza kwingine tu kuwa wazungu wanatuonea. Nakubali wanafanya hivyo lakini ICC imefanya vizuri katika nchi za mabara mengine kabla ya Africa kuwafikisha mbele ya haki madikteta.

  Nitafurahi nikisikia NGOs kote Africa na Wanaharakati wakiwauliza viongozi wao kwanini waliwatetewa wahalifu wa uchaguzi Africa?

  Aheri basi wakakataa ICC wakaunda mahakama yao serious ikawashughulikia hawa wahalifu ambao kila mwaka wanaongezeka Africa.
  :A S crown-1:
   
Loading...