ICC inailindaje jamii pana isiyo na hatia dhidi ya madhara ya utapeli wa kimataifa??

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,856
401
Ndugu zangu wanaJF na watanzania kwa ujumla,

Wakati wote nimekuwa nikitafakari kuhusu madhara ya kuilipa kampuni ya kitapeli ya Dowans kwa fedha zetu sisi wananchi maskini. Mwanzoni, nilijipa moyo kwamba kelele zinazoendelea mitaani za kupinga malipo kwa Downs zinaweza zikasaidia kuzuia serikali yetu ya kifisadi isiilipe Dowans. Lakini ndani ya jamvi letu hili nimesoma THREAD moja inayoeleza na kufafanua kuhusu kwa nini MALIPO KWA DOWANS NI LAZIMA. Wachangiaji wengi wanaonekana kushawishika na mtazamo wa mwandishi wa thread. Sina hakika, lakini kuna uwezekano kuwa baadhi yetu humu jamvini ama ni wahusika wa utapeli moja kwa moja au ni maajenti wa matapeli.

Kutokana na maelezo hayo, nimejikuta nafika mbali zaidi katika tafakuri yangu kuhusu Dowans. Nimetafakari kwamba hivi vyombo vya kisheria iwe ni ndani ya nchi au viwe vya kimataifa vimewekwa au vimeundwa kwa maslahi ya nani? Kwa uelewa wangu mdogo nilijishawishi kuwa sheria zozote duniani (kama zimeundwa kwa namna ya kawaida) lazima ziwe na mwelekeo ambao mwisho wa siku maslahi ya jamii kubwa yatalindwa ili kuleta na kudumisha amani na utulivu miongoni mwa wananchi husika. Kwa mtazamo wangu hiyo ndiyo inayoitwa PUBLIC INTEREST. Vivyo hivyo, kwa mtizamo huo, naamini kuwa hata vyombo vinavyoundwa kutafsiri sheria hizo lazima viwe na mwelekeo wa kuhakikisha kuwa MASLAHI PANA YA JAMII yanalindwa zaidi ikilinganishwa na MASLAHI YA KIKUNDI KIDOGO.

Sasa ninachojiuliza ni je, kama serikali inayoongozwa na jk inawajali na kuwaonea huruma wananchi wake, kwa nini isikate rufaa na kupeleka kwa ICC ushahidi unaothibitisha kuwa Dowans ni kampuni ya kitapeli na kwamba endapo serikali italazimika kulipa kiasi hicho kikubwa cha fedha, mamilioni ya wananchi wasio na hatia watateseka kwa kipindi kirefu na hata kusababisha baadhi ya kufariki? Ni mazingira gani au sababu gani ya msingi kisheria inayoizuia serikali isifanye hivyo?

Lakini vilevile, ninajiuliza pia kwamba je, ICC inatambua uwepo wa utapeli wa kimataifa unaoweza kufanywa na kikundi kidogo cha watu kutoka ndani au nje ya nchi kwa kushirikiana na viongozi wa nchi husika? Kama inatambua hivyo, ICC inawalindaje wananchi wa kawaida mamilioni kwa mamilioni wanaoteseka kwa utapeli wa kimataifa hata kama umewashirikisha viongozi waliowachaguliwa na wananchi hao hao? Na kama haitambui hivyo, je, ni nini faida ya ICC katika mustakabali mzima wa kulinda maslahi ya umma katika jamii pana ya kimataifa?

Conclusion:
Kama majibu ya maswali hayo yatadhihirisha uhalali wa Dowans kulipwa, basi binafsi sioni umuhimu wa kuwa na ICC na kama kulikuwa na uhiari wa nchi yetu kujiunga na ICC, kwa nini tusijiulize upya maslahi ya uanachama wetu kwa ICC? Na kama ICC inahusika na nchi yoyote duniani ikiwemo Tanzania, je, hatuoni sasa ni muhimu sheria husika zipitiwe upya ili kuondokana na uwezekano wa kulinda maslahi ya kikundi kidogo cha watu badala ya jamii nzima?
 
Post yako ni nzuri...tena sana....usichojua (ama unajua ila ulitaka changamoto) ni dhahiri kua DOWANS ni mradi wa wakubwa...kwamba Kikwete ni mwanahisa haina shaka,hiyo ICC itapata wapi nguvu....matapeli wa nchi hii si wakimataifa km ulivyowaita bali ni wakitaifa wenye majina ya kimataifa na wasio na chembe ya haya...nafsi itawasuta kwani siku ya kiama chao ii karibu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom