Mimibaba
JF-Expert Member
- Jul 1, 2009
- 4,557
- 1,291
Shomoro, pesa zetu, ni zile pesa za kodi, hizi huwa haziruhusiwi kutumika mpaka wawakilishi wetu wakubali pale bungeni ndio maana zinapelekwa kuombwa kwa jina la bajeti na kupitishwa na ndipo hutumika.
Waziri wa fedha keshasema, bejeti ya kulipa fedha hizo, haitoki hazina, hivyo hilo ni zigo la Tanesco, na kwa Tanesco ninayoijua mimi, iko chapa lapa, haina uwezo wa kulipa bila kukopa. Kwa vile wenye nchi wameshasema tutalipa, na sio hazina ndiye atayelipa bali ni Tanesco, na bili ya umeme haipandi, sasa mna wasiwasi gani?.
Jamani nyie wenzangu mbona wagumu kuelewa tuu haka ka mchezo!. Anayedaiwa kasema analipa kwa roho nyeupe, bado hamuelewi tuu?.
Naomba ufafanuzi kwako.
Tanesco walisubiri maoni ya serikali kuhusu hukumu. Mwanasheria mkuu akaisoma hukumu na kuikubali. Waziri akatangaza kulipa kwa ushauri wa Mwanasheria mkuu. CC ya ccm imeamua deni lilipwe sijui kwa mandate ipi waliyonayo kikatiba.
Hayo yote hapo juu ongeza na kupanda bei ya umeme huoni sisi tunahusika moja kwa moja?