ICC-ICA Rules zinaruhusu review ya tuzo na mchakato? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ICC-ICA Rules zinaruhusu review ya tuzo na mchakato?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 23, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Sema kwa mfano baada ya hukumu na kabla ya malipo new facts zinatokea ambazo ni muhimu katika hukumu na zilifichwa kwa makusudi ili kunufaisha upande mmoja aliyedhuriwa ana recourse gani ya kisheria in light of 'no appeal clause'?
   
 2. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wanasheria vp? embu tufumbueni macho hapo
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu kuna information ambayo imeangukia kwa bahati Mbaya (kwa Dowans) na nzuri kwa (Tanesco) lakini sijui kushare information hiyo kutasaidia nini wakati serikali tayari imeshaamua kulipa? Tuwaache walipe ndio tushee hiyo?
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Toa hiyo information am sure katika kila kesi kama new evidence comes to light unaweza ukafungua kesi hata kama sio kupinga award ya ICC tunaweza kuifungulia kesi dowans na kuwadai pesa ambayo itakuwa plus fidia ya award na cost zote za kuendeshea kesi na kutuweka gizani for all this time
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,626
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, Ni mkataba wa Tanesco na ICC ndio ume relinguish haki zote za Tanesco kwa uamuzi wa ICC, japo mkataba umebainisha wazi, sheria za kutumika ni za Tanzania, vipengele vya mkataba huo vimeifanya ICC ndio final na supreme na kuiamuru High Court yetu kutekeleza maamuzi ya ICC bila kuyahoji. Hili ni kwenda kinyume cha katiba yetu!.

  Kwa vile mdaiwa kakubali kulipa kwa roho nyeupe, pesa ni za Tanesco na sio zenu!, nyie wengine unaopinga malipo nikiwemo mimi, swali mnaulizwa, " Pilipili iko shamba, nyie inawawashia nini?.

  Waziri wa Fedha wa keshasema, Hazina haina fedha, hilo ni zigo la Tanesco, sasa mnawasiwasi gani wakati fedha zitakazolipwa sio za hazina bali ni za Tanesco, tena Tanesco, imeshawatoa wasiwasi kuwa kupanda kwa umeme hakuna uhusiano na fidia ya Dowans, sasa wasiwasi wa nini?.

  Hivi hili suala bado mlipigia kelele mpaka leo, hivi hamjaelewa tuu kinachoendelea?. Wenyewe wanaodaiwa wamekubali kulipa, nyiemsio daiwa mnakatalia nini?.

  Wakati wa Rada, walioambiwa kila kitu mpaka Claire Short akaligomea huko Uingereza, wenyewe wanaitaka Rada walishakubali kuilipia na wakailipia, sasa leo mnashanga nini?.

  Bei ya Gulf Steam tuliambiwa ni bilioni 42, John Cheyo akaingia kwenye web site yao, akakuta bei ni Bilioni 18!.Akaiambia serikali bei ni nusu ya mliopewa, nunueni straight toka BAE, serikali ilikataa na ikalipa ile Bilioni 42!, sasa leo mnashangaa nini?.

  Na ile tenda ya ununuzi wa magari ya jeshi ni hivyo hiyo, tena naomba nisitoe siri ya ununuzi wa silaha za kivita zikiwemo helcopter bomu kwa bei mara mbili ya bei halisi na ajenti ni yule yule, serikali ni ile ile, hivi hamjaelewa tuu?.

  Hizo fedha ni zao, ama zenu?.Kama ni zao, wenyewe wamekubali kulipa, nyie kelele za nini?.

  Acheni walipe tuendelee na maisha ya kila siku, after all mwenye nyumba ameshasema hizi ni kele tuu za mlango, bado mnapiga kelele?.
   
 6. Shomoro

  Shomoro Senior Member

  #6
  Jan 23, 2011
  Joined: Aug 22, 2010
  Messages: 111
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wewe Pasco mimi sikuelewi kabisa. Unavyosema pesa sio zetu unamaanisha nini?
   
 7. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Since leo ni weekend na ninajua mambo ya weekend ninakusamehe ila naomba kesho ukiwa sawa urudi tuongelee hii issue vizuri..., By the way fedha ni zetu thats why tunalalamika.
   
 8. k

  kayumba JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni bora ku-ishare labda inaweza kusaidia!
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,626
  Trophy Points: 280
  Shomoro, pesa zetu, ni zile pesa za kodi, hizi huwa haziruhusiwi kutumika mpaka wawakilishi wetu wakubali pale bungeni ndio maana zinapelekwa kuombwa kwa jina la bajeti na kupitishwa na ndipo hutumika.

  Waziri wa fedha keshasema, bejeti ya kulipa fedha hizo, haitoki hazina, hivyo hilo ni zigo la Tanesco, na kwa Tanesco ninayoijua mimi, iko chapa lapa, haina uwezo wa kulipa bila kukopa. Kwa vile wenye nchi wameshasema tutalipa, na sio hazina ndiye atayelipa bali ni Tanesco, na bili ya umeme haipandi, sasa mna wasiwasi gani?.

  Jamani nyie wenzangu mbona wagumu kuelewa tuu haka ka mchezo!. Anayedaiwa kasema analipa kwa roho nyeupe, bado hamuelewi tuu?.
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Pasco I can read and understand your frustrations lakini bado hii haituondolei haki ya kufuatilia na kufahamu hizi shoddy deals za serikali yetu. If that would have been the case watu kama Mandela, MLK na hata X would have just been busy running their lives na familia zao. Simply kwa sababu the opressor alihalalisha mpaka kwenye katiba kwamba mambo waliyokuwa wakifanya ni sahihi na halali.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,626
  Trophy Points: 280
  VoiceOfReason, ni kweli unavyosema, hapa Cava inaishia ishia,ila mimi ni kama Prof. Shaba!, the more i get the better I perform!.

  Hii "By the way fedha ni zetu thats why tunalalamika", kama zingekuwa zenu, basi wangefikisha cabinet na wangerudi bungeni kutuomba!. Kwa vile wametangaza kulipa straight forward, bila kuiambia cabinet na bila kusubiri, bunge, basi usiwe na shaka, Tanesco watalipa kwa fedha watakazozipata wanakojua waona sio zetu, msiwe na wasiwasi!.

  Hi common sense logic haijakutuma kujua kwa nini tumekubali kulipa haraka haraka?. Masikini Valambia, Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, anadai madai genuine, ya kugharimia vita ya Kagera, serikali imekataa kumlipa kwa zaidi ya miaka 20!, tena kesi zote kashinda na kila siku serikali inakata rufaa dhidi ya rufaa mpaka bada wa watu kajifia!.

  Wastaafu wa Afrika Mashariki, wanadai madai very genuine, serikali ya Uingereza iliwalipa na kuzileta fedha zao zote na kuikabidhi Hazina, serikali ilikuwa na ukata ikazitumia kwa matumaini ya kuzirudisha, haikuzirudisha na haikuwalipa. Wakafungua kesi, wakashinda. Mkapa akaahidi kulipa, mpaka leo wanajifia mmoja baada ya mwingine bila kulipwa!, lakini hili la Dowans, kampuni hewa, wamiliki fictitious lakini serikali mbio mbio imesema italipa!, what a double standard, hivi mpaka hapa hamjaelewa tuu?!.
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,626
  Trophy Points: 280
  Nyambala, mimi nilitaka watu kama Mzee Mwanakijiji, wasipige kelele, bali wawaambie Watanzania, what is "the name of the game",wanajidai watalipa simplt because, watajilipa!, mpaka watu mnaowaamini mkifikiri wako nanyi, ni viongozi wenu mliowaamini na kuwachagua tena kwenye kiti cha mbele, lakini kumbe ndio hao hao!. Kikulacho siku zote ki nguoni mwako!. Sasa kuna ubaya gani kama wakijilipa kwa fedha za mkopo,ambao haitaulipa wewe, labda watoto wako na watoto wa watoto wako?.
   
 13. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #13
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Ndio sababu nasema hii nchi haitakuwa sawa mpaka hao watu "cancer" watakapongolewa madarakani na kufilisiwa ili iwe mfano kwa vizazi vijavyo....? Mimi ndio maana nasema hata wasipolipa sitafurahia, I will be happy the day ambapo nyumba za baadhi ya hawa watu zitakapotaifishwa na kufanywa museums, maktaba, e.t.c.
   
 14. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  The Time is Running Out...., We need to Strike When the Irons Still Hot!!!!, Please do the neadful
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,626
  Trophy Points: 280
  VoiceOfReason, kwa mujibu wa ule mkataba niliouona humu, tumefungwa mikona, front, back, left and right, hatuna pa kutokea, the only way ni kudeclare, to hell with ICC, hatulipi!, lakini wenye uwezo wa kusema hatulipi ndio hao hao benefisiaries wa malipo hayo!, sasa wakate tawi walilokalia?.
   
 16. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mimi kwenye kuwalipa nimesha - surrender..., kilichobaki ni kuona hizo proof hata kama kuna chembe ya kuhujumu uchumi wa hawa waheshimiwa basi tuwaambie wananchi wote ukweli ili wajue kwamba kuna "The Enemy Within"..., hopefully tunaweza kurudisha pesa zetu kutoka kwenye mali za hawa waheshimiwa. What is 95 Billion if it helps us to get rid of huu uozo?, am sure tukitaifisha kampuni zao tunaweza kupata mara kumi ya hizo...., mmoja wao alisema yeye kampuni zake zinapata fedha kama hizo kwa miezi minne tu..!!!
   
 17. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mkuu mwanakijiji we tuwekee tu hizo document hapa mkuu ili siku tukiingia bara barani hata wakileta vifaru tusiogope.
  Nadhani Tanzania kunahitajika vikundi vya kijesus kwa ajili ya kuisimamia serikali kama vile ilivyo mafia mob ya italy, izibola ya lebanoni na vinginevyo....maana naona democrasia ishatushinda.
   
 18. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu tuwekee hizo latest news even a small leak (You and Others) can sink big SHIP (DOWANS)
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,626
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, nimerudia hii hoja yako, kisheria, ukiweza kuthibitisha kuna facts zilifichwa kwa makusudi ili kuusaidia upande fulani, facts hizo zinawasilishwa Mahakamu Kuu, Mahakama Kuu inagoma kuthibitisha hukumu, ikiirudisha ICC for review kwa kuzingatia facts hizo mpya zilizoibuka. Kama ICC ikizitupilia kwa hoja za kisheria au za kimaslahi na kushikilia hukuku ya awali, Mahakama Kuu yetu hapa imefanywa ni joka la Mdimu, haina meno na imefungwa mikono yote kwa nyuma, na kulazimika kuisajili hukumu.

  Sasa kama hivi facts zipo, hapo ilipofika ndio mahali pake stahili, Mzee Mwanakijiji, ziwahishe.

  Kuna wakati niliamini kale Kainzi kamekufa!, tuthibitishie kuwa bado kapo and still going strong!.
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Kisheria, technically speaking - WEWE, NA MIMI SIYO PARTY TO THE CASE.Lakini inapokuja kulipa na wenye kesi wakakubali na kuingia
  ' mifukoni mwao" hatuna jinsi bali kusikia maumivu. Ndiyo ukweli anaouweka Pasco hapa.Wakati wanafanya haya makubaliano, wewe na mimi hatukuhusishwa na kama waliokuwa wana negotiate hawakuweka maslahi yetu mbele kwa maana ya kuingia ndani na kuchambua kwa marefu na mapana yake basi kama madhara yatatokea hatuna jinsi bali kudhurika.Wenyewe watakuambia kama faida au nafuu ingetokea, leo hii huu mjadala usingekuwepo. Kwamba kuna haya madhara basi ndio mchezo wa kula uliwe!
   
Loading...