"Ibrahim Class" the most decorated boxer in Tanzania,bingwa mpya wa WBF

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
"IBRAHIM CLASS" THE MOST DECORATED BOXER IN TANZANIA,BINGWA MPYA WA WBF.

Leo 16:45hrs 30/01/2021

Ibrahim Class ndiye bingwa mpya wa Mabara,World Boxing Federation (WBF) super featherweight intercontinental, Champion Ibrahim Class usiku wa Jana amempiga Mmalawi Dennis "The Menace" Mwale katika ukumbi wa ngumi wa kimataifa,Next Door Arena,Masaki jijini Dar es Salaam,mchezo huo ulihudhuliwa na Bondia wa Dunia Kubrat Pulev ambaye mwezi uliopita alipambana na Bingwa wa Dunia,Antony Joshua,mchezo huo pia ulihudhuliwa na Rais wa WBF,Howard Goldberg.

Ibrahim Class,shujaa wa ulingoni mwenye ujuzi mkubwa na mbinu za kuvutia,tekniki na ubora wa hali ya juu,timamu wa akili ya ngumi,mwepesi wa mwili mwenye kipaji cha kuzaliwa cha masumbwi,si mpiganaji mjanja bali mpiganaji mwenye skills zilizokwenda mbele zaidi kwenye makabiliano,alitwaa ubingwa huo wa mabara baada ya kumpiga Dennis "The Menace"Mwale kwa point,huku majaji wote watatu wakimpa Ushindi Champion Ibrahim Class.

Ibrahim Class ni Bondia mwenye kutupa ngumi tano kwa wakati mmoja,mzuri wa kukwepa na kurudi ambae ni vigumu kummaliza baada ya kukushambulia,utawakumbuka mabondia wazuri wa dunia kama Michael Spinks,James Buster Douglas,Joe Frazier,George Foreman,Mohamad Ali,Mike Tyson wote walikuwa na mapigo ya ushindi,uwezo wa kupiga ngumi na kukwepa,sifa kubwa zikiwa ni spidi,kusimama kidete kwa uvumilivu,kuruka ruka huku na kule kumtafuta mpinzani kichwani,

Ibrahim Class mwenye makonde ya vita vya kijeshi akipiga kwa stahili ya silaha za maangamizi ya halaiki, uwa hatetereki hata ukimshambuliaje,anarudi nyuma hatua mbili kana kwamba anakuogopa kisha ghafla kutoka upande aliopo anakusukumia makonde yanaulenga usoni huku akiandaa upper cut amalize mchezo,atakusogezea uso lakini fahamu kuwa Ibrahim Class ni mwenye uwezo mkubwa wa kukwepa,stahili hii itamsumbua mpinzani mwenye kudhani kapata kumbe kapatikana,hivi ndivyo akivyopigwa Mwala "The Menace" Denis baada ya kuachiwa kichwa akipiga ngumi zake mbili lakini baada ya konde la pili,Ibrahim Class alimuadhibu kwa makonde ya vita vya kijeshi,kwa stahili ya silaha za maangamizi ya halaiki,

-Ubora wa Championi Ibrahim Class.

Focus,timing nzuri,skills,stamina na technicni haya ni maeneo anayostahili sifa bondia wetu Ibrahim Class kwa sababu ana makonde mazuri,anaweza kukwepa na kumzunguka mpinzani,Championi Ibrahim Class ana ngumi za ana kwa ana anazimudu na anao ufundi,Championi Ibrahim Class anapiga ngumi za kiufundi zaidi,uzuri wa Champion Class,haangaiki kupigana ngumi za mitaani kama mabondia wengi wasio wataalam wanavyofanya,

Kupiga ngumi kimahesabu ndiko kunakotakiwa,anafanya ‘timing’ nzuri kwa kumchapa makonde katikati ya uso wa mpinzani na kichwani, Shukrani kwa Waalimu wake Kocha mkongwe Habib Kinyogoli,na Rajab Mhamila "Super D" wamemfundisha ujuzi na ufundi mkubwa wa ngumi za kimataifa,waendelee kumwongezea maarifa kwa vile ameonesha uwezo mkubwa sana.

Tunaweza kumsifia Ibrahim Class kwa uwezo wake mzuri wa kukwepa makonde, na mojawapo ni yale ya ‘Upper cut’ ambayo anayakwepa vizuri,huku nae akipeleka makonde ya kiufundi mkubwa kwa mpinzani wake,Hiyo ni ishara kuwa bondia anatakiwa kuwa na ‘focus’ya eneo au mbinu fulani ili kummaliza mpinzani wake,hata kwenye ,mpira wa miguu iko hivyo,ukiona udhaifu kwa mabeki wa pembeni basi unatakiwa kutumia mianya hiyo kupitia maeneo hayo na kuwachapa mabao wapinzani,

Nimalizie kwa kutoa kongole kwa mabondia wote wa Tanzania ambao kwa sasa wameifanya Tanzania kuwa kama Marekani na Uingereza kwenye medani ya masumbwi,Bondia Dulla Mbabe,Bondia Cosmas Cheka,Ninapoona mashabiki wa Twaha Kiduku wakimtaka Hassan Mwakinyo,nakumbuka mashabiki wa Antony Joshua wanavyomtaka Tyson Fury,pongezi pia kwa Ukumbi bora kabisa wa Next Door Arena,Masaki jijini Dar es Salaam,hapa unapata uhakika wa kushuhudia mapambano bora ya ngumi yenye hadhi ya kidunia kila mwezi,naamini siku moja pia tutamshuhudia Man Pacquiao akipigana na Mtanzania katika Ukumbi huo wa Next Door Arena,Masaki jijini Dar es Salaam.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Sifa zote hizo.... Ila kiuhalisia wabongo katika ngumi bado sana.... Labda tupate makocha kutoka ulaya na america.... Ama mabondia wetu waende huko nje kujifunza zaidi ...
 
Ngumi hatutaki mambo ya siasa
Ngumi mpaka hapa ilipo inasimamiwa na watu wanaojua boxing hata kuucheza
Siyo soka inaongozwa na watu ambao hata kupiga danadana hawawezi
Ngumi ikipatikana wadhamini wa nguvu basi tz itatoa wakina myweather kama 100

Kama mtu wa ngumi jumatano tukutane kwenye gym ya mzazi respect muone vijana wanavyojifua na kupiga vitasa+ shadow boxing

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Nimemkubali sana Ibra yuko vizuri sana mshkaji na nimempima kwa kumuangalia mmalawi
Mmalawi yuko vizuri pia lakini hajaamini alichokutana nacho pambano la jana nimelikubali lakini siyo mapambano kama alilowahi kupambana Mfaume na akashinda kimagumashi akina mfaume inabidi wafanye kazi nyingine kwa sasa waachane na ngumi

Pambano lingine nililolikubali lilikuwa la jamaa anaitwa mchumia tumbo na mwingine wa bagamoyo sikumbuki jina lake
Walipigana vizuri sana na ni uzito wa juu

Pia majaji inabidi watoe haki kwa mabondi wageni siyo lazima kuwabeba wageni ikitokea wamepigwa wanaharibu mchezo
 
Nimemkubali sana Ibra yuko vizuri sana mshkaji na nimempima kwa kumuangalia mmalawi
Mmalawi yuko vizuri pia lakini hajaamini alichokutana nacho
Pia majaji inabidi watoe haki kwa mabondi wageni siyo lazima kuwabeba wageni ikitokea wamepigwa wanaharibu mchezo
wenyeji wanabebwa sana mpaka aibu
ngoja watakapoitwa huko mje kutetea mikanda km hawakuiacha yote huko
Tanzania kwa Boxing bado hawa Malawi, Botswana DRC zimbabwe kote tunapoteza muda, mbona Olympic tunashindwa,
 
Ngumi hatutaki mambo ya siasa
Ngumi mpaka hapa ilipo inasimamiwa na watu wanaojua boxing hata kuucheza
Siyo soka inaongozwa na watu ambao hata kupiga danadana hawawezi
Ngumi ikipatikana wadhamini wa nguvu basi tz itatoa wakina myweather kama 100

Kama mtu wa ngumi jumatano tukutane kwenye gym ya mzazi respect muone vijana wanavyojifua na kupiga vitasa+ shadow boxing

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Kwel aisee ; hiv Barbara Gonzalez anaweza kupiga hata danadana 2 kweli!😂
 
Ngumi hatutaki mambo ya siasa
Ngumi mpaka hapa ilipo inasimamiwa na watu wanaojua boxing hata kuucheza
Siyo soka inaongozwa na watu ambao hata kupiga danadana hawawezi
Ngumi ikipatikana wadhamini wa nguvu basi tz itatoa wakina myweather kama 100

Kama mtu wa ngumi jumatano tukutane kwenye gym ya mzazi respect muone vijana wanavyojifua na kupiga vitasa+ shadow boxing

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Nataka kujifunza seld defence, nije hapo?
 
Ibra classic yuko vizuri sana atafika mbali ....ila we mleta mada inaonekana hata kwenye uchambuzi wa boxing hujui lolote,umeandika ili mradi uonekane umeandika.
 
Back
Top Bottom