Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,691
- 149,915
Ibara ya 90-(2) inazungumzia sababu ambazo zinaweza kumfanya Raisi kulivunja Bunge wakati wowote.
Moja ya sababu inayotajwa katika Ibara ya 90-(2)(e) inasema:
endapo,kutokana na uwiano wa uwakilishi wa Vyama vya Siasa katika Bunge,Raisi anaona kwamba hakuna uhalali kwa serikali iliyopo kuendelea kuwepo na wala haiwezekani kuunda serikali mpya.
Pia ibara hiyo ya 90-(2)(b) inampa Raisi mamlaka ya kulivunja Bunge iwapo Bunge likataa kupitisha Bajeti inayopendekezwa na Raisi.
Kwa mtazamo wangu, iwapo hatutakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na serikali hii ikaendelea na mwenendo wake wa sasa,kuna uwezekano wa CCM kupoteza idadi kubwa ya wabunge lakini Raisi akasalia na hivyo anaweza kuona hana uhalali wa kuunda serikali au akajikuta anashindwa kuunda serikali na kulazimika kulivunja Bunge kwa kutumia Ibara hiyo niliyoitaja hapo juu.
Tukumbuke sehemu ya kipengele hicho kinasema wazi kuwa ni kutokana na Raisi atakavyoona bila shaka hii inamanisha ni kutokana na utashi wake na sijui kama kuna mashariti kawekewa(wataalamu wa sheria mtatusaidia hapa).
Mimi kama mwananchi wa kawaida, nashauri tuwe na kipengele katika katiba yetu kinachoruhusu kuundwa kwa serikali ya mseto(Raisi aruhusiwe kuunda serikali ya mseto) iwapo hali ya aina hiyo itajitokeza maana uchaguzi ni gharama na nchi yetu bado ni masikini sana licha ya rasilimali zote tulizonazo.
Msisahau idadi ya wabunge wa upinzani imekuwa inaongezeka katika kila mwaka wa uchaguzi na 2020 wapinzani wanaweza kabisa kutawala Bunge kutokana na hali hii tunayoendana nayo sasa.
Sidhani hata Katiba inayopendekezwa kama imetazama jambo hili.
Ni ushauri tu.