Ibara ya 35 ya Sheria ya Uchaguzi ilifutwa lini - ingeweza kulisaidia TAIFA sasa hivi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,747
Likes
7,616
Points
280

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,747 7,616 280
Sheria hii ya Uchaguzi ya 1984 Sehemu ya Kipengele chake ilikuwa inasema:

(2) The Electoral Commission may, for any reason which appears
to be sufficient, require that the votes in the constituencies, or in any
particular constituency, shall be recounted.
(3) Subject to sub-section (2), the Commission shall, after adding
together all the respective totals certified to it in accordance with subsection
(1), declare the result of Presidential election.
Sijapata muda wa kufuatilia kwa karibu maana najua kuna mabadiliko kadhaa ya Katiba yalifanyika, sijui kama sheria ya Uchaguzi ilivyo sasa inasomeka ikiwa na vifungu hivyo.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
79,380
Likes
43,056
Points
280
Age
28

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
79,380 43,056 280
Mwanakijiji, tanzania, kwa ujumla si taifa lenye kufuata utawala wa kisheria hasa pale maslahi ya watu fulani yanapokuwa hatarini
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,747
Likes
7,616
Points
280

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,747 7,616 280
Maana nikikumbuka Katiba inakataza tu kuyapinga matokeo baada ya Rais kutangazwa, kabla ya hapo haikatazwi. Na kwa vile sheria inatoa a wide room ya argument "for any reason".. nadhani kesi ya Geita na sehemu nyingine inatosha kusababisha kutaka a court injunction ya kuwazuia tume kumtangaza mshindi hadi hoja za Chadema kuhusu uchaguzi. Mimi naamini tatizo kubwa liko ndani ya Tume.
 
GeniusBrain

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
4,321
Likes
19
Points
135

GeniusBrain

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
4,321 19 135
Maana nikikumbuka Katiba inakataza tu kuyapinga matokeo baada ya Rais kutangazwa, kabla ya hapo haikatazwi. Na kwa vile sheria inatoa a wide room ya argument "for any reason".. nadhani kesi ya Geita na sehemu nyingine inatosha kusababisha kutaka a court injunction ya kuwazuia tume kumtangaza mshindi hadi hoja za Chadema kuhusu uchaguzi. Mimi naamini tatizo kubwa liko ndani ya Tume.

Katiba inasema hivi , na nukuu ' Iwapo Mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa RAIS , basi hakuna mahakama yoyote itakayo kuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake'.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,613
Likes
610,862
Points
280

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,613 610,862 280
Re: Ibara ya 35 ya Sheria ya Uchaguzi ilifutwa lini - ingeweza kulisaidia TAIFA sasa

Maana nikikumbuka Katiba inakataza tu kuyapinga matokeo baada ya Rais kutangazwa, kabla ya hapo haikatazwi. Na kwa vile sheria inatoa a wide room ya argument "for any reason".. nadhani kesi ya Geita na sehemu nyingine inatosha kusababisha kutaka a court injunction ya kuwazuia tume kumtangaza mshindi hadi hoja za Chadema kuhusu uchaguzi. Mimi naamini tatizo kubwa liko ndani ya Tume.​
Dawa ni hiyo kuizuia Tume kutangaza mshindi wa uraisi ingawaje huko nyuma kwenye kesi za utata wa Uraisi Mahakama kuu ilikwisha kuweka msimamo kuwa kama kuna ushahidi wa mazingira ya kumtangaza mgombea uraisi haykuwatendea haki wagombea wengine Mahakama Kuu inayo mamlaka ya kuingilia kwa kuchunguza na kusawazisha dosari kama zipo.........

Hata hivyo kifungu cha kikatiba cha kukataza Matokeo ya Uraisi yaliyokwisha kutangzwa na NEC kinahojiwa hivi sasa Mahakama Kuu na kesi ya kupinga matokeo ya Uraisi bado yaweza kufunguliwa na aidha kuunganishwa na ile au kuiomba Mahakama kuu kukifuta kile kipengele cha kikatiba na kusikiliza hilo shauri.......................Zipo njia mbadala kibao za kuipa nafasi Mahakama kuona kama JK kweli ni Raisi halali wa nchi hii.........
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,747
Likes
7,616
Points
280

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,747 7,616 280
Kwanini Dr. Slaa asitake tume iagize wasimamizi wote wa uchaguzi wa majimbo kuweka hadharani mara moja fomu zote za matokeo ya Ubunge na Urais ili ziweze kupitiwa hata baada ya kuapishwa Rais ili kuweka historia na rekodi sawasawa?
 
Tata

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2009
Messages
5,171
Likes
1,004
Points
280

Tata

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2009
5,171 1,004 280
Sheria hii ya Uchaguzi ya 1984 Sehemu ya Kipengele chake ilikuwa inasema:Sijapata muda wa kufuatilia kwa karibu maana najua kuna mabadiliko kadhaa ya Katiba yalifanyika, sijui kama sheria ya Uchaguzi ilivyo sasa inasomeka ikiwa na vifungu hivyo.
Mheshimiwa hata kama kipengele hicho kingekuwepo bado hakiwezi kuziba mianya ya kuchakachua kwa sababu kwa mfumo ulivyo sasa kama kuna kuhesabu upya basi maboksi yote ya kura hukusanywa na kupelekwa kwenye kituo kimoja (kwa msimamizi wa uchaguzi) kwa ajili ya kuhesabiwa. Uhamishaji wa maboksi unasimamiwa na polisi na jeshi kwa kutumia magari yao na hakuna wakala anayeruhusiwa kufuatana nao wakati wa zoezi hilo.

Suala ni kwamba hakuna jinsi ya kuhakiki kama kweli maboksi yanayochukuliwa vituoni ndiyo yanayofikishwa kwenye kituo cha kuhesabia kura. Kwa kuwa wahamishaji ndio walewale waliosema kuwa lazima watu wakubali matokeo na wote wanaripoti kwa amiri jeshi mkuu ambaye anakuwa ni mmoja wa wagombea basi lolote linaweza kutokea. Udhaifu huu umetumiwa vilivyo na wagombea wezi ambao walikuwa wanadai kura zihesabiwe upya baada ya kuwa wameshaingiza kura zao zilizochakachuliwa.

Dawa ni matokeo yote (uraisi, udiwani na ubunge) kutangazwa palepale kwenye vituo vya kuhesabia kura nakala za matangazo hayo yenye matokeo kubandikwa kituoni na nakala kupewa wawakilishi wa vyama, vyombo vya habari na wasimamizi wa uchaguzi. Baada ya hapo vyombo vya habari viruhusiwe kuyatangaza. Huu utaratibu wa kusubiri mpaka Msimamizi wa uchaguzi ayajumlishe na kisha wazee wa NEC wayahakiki unatoa mianya ya wizi wa kura.

Kama mtu ana wasiwasi na matokeo basi aende mahakamani aeleza ni vituo gani anataka matokeo yahesabiwe upya. Mahakama ndiyo itakuwa na maamuzi ya kutoa kibali cha kuhesabu upya matokeo hayo chini ya uangalizi wa wanasheria (mawakili) wa pande zote mbili. Asiruhusiwe mgombea kudai tu kuwa matokeo yote yahesabiwe upya wakati yalihesabiwa mbele ya wawakilishi wake na watu wengine.

Cha muhimu hapa inabidi unangalizi wa maboksi ya kupigia kura uwe ni wa makini kuondoa uwezekano wa watu kuingiza maboksi yenye kura zilizochakachuliwa. Hii inaweza kufanikiwa kwa maboksi hayo kuwekewa lakiri vituoni huku wawakilishi wa vyama vyote wakiwepo na lakiri hizo zitaondolewa pale tu kutakapokuwa na uamuzi wa mahakama wa kuhesabu upya.

Lakini sheria iwe wazi kuwa tukimpata mtu ana maboksi yenye kura za kuchakachua ama amechakachua tunamshitaki kama mhaini na anahukumiwa kunyongwa ama kufungwa maisha.
 
Tata

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2009
Messages
5,171
Likes
1,004
Points
280

Tata

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2009
5,171 1,004 280
Maana nikikumbuka Katiba inakataza tu kuyapinga matokeo baada ya Rais kutangazwa, kabla ya hapo haikatazwi. Na kwa vile sheria inatoa a wide room ya argument "for any reason".. nadhani kesi ya Geita na sehemu nyingine inatosha kusababisha kutaka a court injunction ya kuwazuia tume kumtangaza mshindi hadi hoja za Chadema kuhusu uchaguzi. Mimi naamini tatizo kubwa liko ndani ya Tume.
Hizi mahakama kiwete za Tanzania haziwezi kufanya hilo. Kumbuka kesi ya mgombea binafsi ambapo mahakama ya rufaa iliamua, bila aibu, kujivua madaraka na kuyakabidhi kwa bunge wakidai kuwa ni suala la kisiasa. Sioni ni jinsi gani mahakama hii kiwete inaweza kufanya uamuzi dhidi ya Tume ya uchaguzi.
 
PAS

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2010
Messages
452
Likes
3
Points
35

PAS

JF-Expert Member
Joined May 3, 2010
452 3 35
sheria hii ya uchaguzi ya 1984 sehemu ya kipengele chake ilikuwa inasema:Sijapata muda wa kufuatilia kwa karibu maana najua kuna mabadiliko kadhaa ya katiba yalifanyika, sijui kama sheria ya uchaguzi ilivyo sasa inasomeka ikiwa na vifungu hivyo.
andika kwa lugha aliyotuachia mwl nyerere ndo ntaelewa vizuri ili nichangie fasta
 
Jatropha

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2009
Messages
1,152
Likes
144
Points
160

Jatropha

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2009
1,152 144 160
Sheria hii ya Uchaguzi ya 1984 Sehemu ya Kipengele chake ilikuwa inasema:Sijapata muda wa kufuatilia kwa karibu maana najua kuna mabadiliko kadhaa ya Katiba yalifanyika, sijui kama sheria ya Uchaguzi ilivyo sasa inasomeka ikiwa na vifungu hivyo.
Vifungu hivyo visingeweza kusaidia katika mazingira ya sasa, kwani uchakachuaji wa kura ni pamoja na kubadili kura oroginal katika masanduku ya kura na kuweka zile zilizochakachuliwa. Kumbuka baada ya masanduku hayo kutoka makao makuu ya Kata hadi NEC Taifa hayasindikizwi na mawakala wa vyama, hivyo chochote kinaweza kutokea.
 
Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
4,482
Likes
363
Points
180

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
4,482 363 180
Kwanini Dr. Slaa asitake tume iagize wasimamizi wote wa uchaguzi wa majimbo kuweka hadharani mara moja fomu zote za matokeo ya Ubunge na Urais ili ziweze kupitiwa hata baada ya kuapishwa Rais ili kuweka historia na rekodi sawasawa?
Wewe unataka anzisha ugomvi, yaani unataka JK aonekane Lofa zaidi maana hiyo 61 itabomoka kiaina na mtashangaa. Kaza moyo twende mbele, mwache ajivunie kaushindi kake ka kubahatisha!

Kuna moja limeonekana, yawezekana watu walichagua wabunge wa CCM, lakini hawakumchagua yeye kama Rais!
 
Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2009
Messages
3,230
Likes
162
Points
160

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2009
3,230 162 160
Maana nikikumbuka Katiba inakataza tu kuyapinga matokeo baada ya Rais kutangazwa, kabla ya hapo haikatazwi. Na kwa vile sheria inatoa a wide room ya argument "for any reason".. nadhani kesi ya Geita na sehemu nyingine inatosha kusababisha kutaka a court injunction ya kuwazuia tume kumtangaza mshindi hadi hoja za Chadema kuhusu uchaguzi. Mimi naamini tatizo kubwa liko ndani ya Tume.
Mahakama za Tanzania, no way, watakuambia mambo ya uchaguzi peleka kwa wapiga kura. Mawakili wa serikali wetu ni bure kabisa, wanaweka mapigamizi ya kisheria kwenye vitu ambavyo ni very very obvious. Ona jamaa mmoja alifungua kesi kupinga kifungu cha kukataza watu kupinga matokeo ya uraisi, the case was handled in a supersonic speed and was finally determined on Friday at 21.00 hrs, to beat the deadline of the election date.

I wish the industry, vigour speed and commitment exhibited by the judges in that case proceed in other cases too. Justice delayed is justice denied, they say, but on the other hand justice hurried is justice buried. ile kesi ilivyoharakishwa justice was buried. Wajitokeze watu wasaidie kupeleka hiyo kesi mahakama ya rufaa.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2008
Messages
7,787
Likes
4,433
Points
280

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2008
7,787 4,433 280
Sheria hii ya Uchaguzi ya 1984 Sehemu ya Kipengele chake ilikuwa inasema:Sijapata muda wa kufuatilia kwa karibu maana najua kuna mabadiliko kadhaa ya Katiba yalifanyika, sijui kama sheria ya Uchaguzi ilivyo sasa inasomeka ikiwa na vifungu hivyo.
Juzi juzi ulikuwa unaapa kwa mbingu na nchi kuwa 'hakuna uwezekano wa kuiba kura' ... leo umebadilika?
 
Forum statistics

Threads 1,203,712
Members 456,928
Posts 28,125,963