Ibara ya 35...Haki za wafanyakazi na waajiri

che wa Tz

JF-Expert Member
Jul 14, 2011
277
71
Ibara hii inazungumza kuhusu haki za mfanyakazi pamoja na muajiri wake pamoja na wajibu wa vyama vya wafanyakazi.....nadhani ibara hii ingeongeza wigo mpana zaidi wa haki za wafanyakazi na iwe wazi zaidi. Kwa Mfano nadhani ingetamka bayana juu ya haki ya msingi ya mfanyakazi kujiunga na chama cha wafanyakazi yakiwa ni maamuzi yake binafsi pasipo kushurutishwa au kulazimisha au kuamuliwa na muajiri wake juu ya ama kujiunga na chama cha wafanyakazi au kutojiunga na aina ya chama anachotaka kujiunga bora tu kiendane na aina ya kazi yake anayoifanya, na pia itamke bayana juu ya maamuzi binafsi ya mwanachama kujitoa au kuendelea na uanachama wake. Hii nadhani itaweka uhuru zaidi kwa mfanyakazi kutokushurutishwa juu ya kuwa na uanachama wa chama ambacho anaona hakikidhi mahitaji yake, mfano halisi ni CWT, wengi wa wanachama wake ambao ni walimu wamepewa uanachama sio kwa ridhaa yao bali kwa kulazimishwa na muajiri wao ambae kwa sasa ni wakurugenzi wa halmashauri wanazofanyia kazi na wengi wao wanatamani kutoka lakini hawajui nini cha kufanya na mbaya zaidi wanakatwa ada za uanachama ambazo hawajui zinaenda wapi, wala taarifa za mapato na matumizi ya chama chao hawajui mbele wala nyuma. Nawasilisha wadau
 
Back
Top Bottom