Ibara ya 30 (d): MwanaHalisi kufungiwa kwa kuvunja katiba ya Tanzania?

nafikiri wazir wa sheria atafiata taratibu za kulifungia gazeti hili

Mh! Yupi? Huyuhuyu tulie naye au mpya? Aanze na watuhumiwa wa ufisadi, tuhuma za Mwakyembe maana ziliorodheshwa na gazeti hili hili, tuhuma za Mengi maana zinachafua dola, ndo afuatilie la hii ya leo! Aanze na namba moja ndipo afuatilie yanayofuata hadi la leo.
 
Mwanahalisi ni gazeti la UDAKU wa siasa na wanasiasa wa Tanzania kama yalivyo magazeti ya Shigongo na celebrities wa Tanzania. Mwanahalisi wanauza kwelikweli kuliko hata Raia Mwema.
 
Wameweka ushahidi so wakiona hawajaridhika akina JK na mkapa waende mahakamani waache kumwagia watu kwa tindikali; limeenda chimbo kweli kweli leo si mchezo ila kulifungia ni kuonea maana lina uahsahidi kama vipi wakane ushahidi huo
 
Nkurukumbi, nkurukumbi, niyo yazaile mayenjeeeeeeeeeeeeeeeee, otalitela, otalijumaaaaaaaa, niyo yazaaile mayenjeeeeeeeeeeee......... aghhhhhhhh....... inabidi tuimbe kilugha. We Jeykey utakuwa kama Kombani na Werema. Walisema katiba ibaki kama ilivyo, president au boss wao akasema ifanyiwe mabadiriko sasa na wewe utachongaaaaaaaa alafu gazeti liaendelea kupeta.

Sijui hawaonagi aibu na unafiki wao?
 
Hamna kitu nisee tu story na kichea tofauti; kiapo cha Ben tayari na kinamlinda mshtakiwa Mahalu; swali je kesi itaendelea? sidhani kama kuna chochote naona wametoa habari iliyofichea kumbe hata Ben huwa anaapa kama raia kuthibitisha madai yake; halafu JK alishitaki vipi wakati wote walikuwa mambo ya nje na habari hiyo alishawahi kuithibitisha bungeni?
 
Leo gazeti la mwanahalisi limechapisha makala yenye kichwa cha " mkapa kutinga kortini"

Makala hii ya kubenea imeeleza jinsi mkapa na jakaya walivyoshiliki katika ununuzi wa nyumba ya ubarozi ROMa kwa kesi inayomkabili Pro Mahalu


Je Mwanahalisi haijaingilia uhuru wa mahakama


30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma

(d)kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine aumaisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashauri mahakamani, kuzuia kutoa habari za siri; kutunza heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama;

halafu likishafungiwa sisi watanzania tunanufaika vip na kufungiwa kwake?

kuna watu sijui mmelogwa? kuna mambo ya msingi kabisa ya kuongelea we unaleta mambo ya mwanahalisi au kwa kua una ubia na mafisadi? Kubenea hamtamuweza kamwe na ataendelea kuwalipua tu..
 
Msilizingatie gazeti hilo kwani linaongoza kwa kukiuka misingi ya uandishi wa habari. Mkitaka kuniamini someni cv ya mhariri wake. Pia, ili habari iwe habari kuna mambo ya msingi matatu ambayo yote mwanahalisi huwa linakiuka.

1. Ni lazima kuwe na 5 Ws + H.

2. Ni lazima maadili yote ya Newsworthiness yazingatiwe.

3. Ni lazima news elements zizingatiwe.

Hayo yote kwa mwanahalisi hayazingatiwi kabisa. Zamani uandishi wa aina hiyo ulikuwa unaitwa yellow Journalism na umewahi kusababisha vita ya nchi kwa nchi.

INASHANGAZA SANA KUONA GAZETI HILI BADO LINACHAPISHWA. NADHANI KUKIUKWA KWA MAADILI YA UONGOZI KATIKA NCHI KUNASABABISHA MAGAZETI KAMA HAYA KUDUMU.
Nitaweza fafanua kama sijaeleweka.

Kama CV ni muhimu sana naomba ibandike hapa CV yako ili niamini hiki ulichoandika, otherwise ulichoandika nakipuuzia pia
 
Gazeti limeingilia uhuru gani?wao wameonyesha jinsi mkapa alivyotoa ushahidi na wao hawajaongeza jambo lolote, kuingila uhuru wa mahakam ni kutoa hukumu na misimamo ya mahakama wakati mahakama haijafanya hivyo, acha ushabiki na propaganda
 
Mkuu kati ya uliyoeleza hii hesabu kwangu haipandi-ni nini hicho?


Mkuu huyo bwana,inaonesha ni mwandishi wa Habari au anajua mambo fulani ya taaluma hiyo lakini amesahau jambo moja kwamba mambo ya darasani ni vigumu sana kuyatumia yote katika field yahani copy and paste.

5Ws +H ni mojawapo ya somo wakati wa mwanzo kabisa wa kujifunza journalism ambapo utakiwa kujiuliza mambo matano kabla ya kuandika Habari na nilazima yawepo katika habari (kwa mjibu wa walimu wa enzi hizo) mimi nilifundishwa hii mwaka 2001
nayo ni
1;What happened,
2.When Happened,
3.Who involved ,
4.Where Happened Nk, +How happened
Lakini nikumbushe jambo moja ,kwamba journalism inakuwa kama ilivyo ICT,hivyo kwa miaka ya hivi karibuni hayo mambo ni ngumu kuyafuata kwani Magwiji wa journalism walishaongeza moja ambayo ni 'So what' kwamba tayari una habari iliyofuata 5Ws+H lakini Mwisho jiulize So what kwa kutoa hiyo habari.

Nafikiri kidogo nimetoa mwanga
 
Bwanawe lazima kuwe na uhuru wa vyombo vya habari mfano ni wazi kuwa mwanahalisi ni chombo cha propganda cha CDM,Tazama wao ni ccm japo si rasmi pia tanzania daima japo ni ya mbowe ni gazeti ambalo liko balanced kwa maana kwamba halisiti kusema mabaya au mazuri ya serikali.sasa kwa sisi wananchi twataka kusoma kila upande unasema nini.hivo suala la kufungiwa mwanahalisi itakua ni kuminya uhuru wa vyombo vya habari same applied to kiongozi,msemakweli,radia iman,al nur etc
 
Wakuu naona jeykey bado anatype hii habari.

Jisevieni wenyewe hii kitu ya Mwanahalisi
 

Attachments

  • kikwete adanganywa..pdf
    731.3 KB · Views: 114
Kwani limeandika uzushi au ukweli? Weka hadharan mapema mheshimiwa!. Najua tu ni ukweli. Kwani gazet hili huwa halikopeshi. Maana ndilo angalau limechangia kwa kias fulani watz kuanza kufunua blanket usoni.
 
Leo gazeti la mwanahalisi limechapisha makala yenye kichwa cha " mkapa kutinga kortini"

Makala hii ya kubenea imeeleza jinsi mkapa na jakaya walivyoshiliki katika ununuzi wa nyumba ya ubarozi ROMa kwa kesi inayomkabili Pro Mahalu


Je Mwanahalisi haijaingilia uhuru wa mahakama


30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma

(d)kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine aumaisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashauri mahakamani, kuzuia kutoa habari za siri; kutunza heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama;

... you need to convince us why the article is sub-judice. Tafadhali tueleweshe uhuru wa mahakama unaingiliwaje hapa, and I quote kama ulivyoandika, "haijaingilia uhuru wa mahakama"
 
Yapo magazeti ya Mwanahalisi yaliyopita yalikuwa na vichwa vya habari utahisi leo gazeti litafungiwa lakini
wapi,MWANAHALISI liko makini sana kuhakikisha halitiwi mikononi kirahisi CV ya Kubenea inahusu??leo ndio unauliza CV kalale unaboa.
 
kwa msaada!kama ni kufungiwa mhusika ni waziri wa habari na sio katiba,hukumbuki huko nyuma?
 
kwani kuna ushahidi uliotolewa?

Mhe kombani atafanya kazi yake kwa gazeti hili , hii itakuwa FUNDISHO KWA MAGAZETI MENGINE

Ninyi mnataka habari za "hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa alipokuwa..., sijui Rais ameyasema hayo.... yani kifupi hampendi habari za Kiuchunguzi. Karibuni katika gazeti la Uhuru, Mzalendo au habari Leo kwa habari unazopenda. Hupo Kwa Mwana wa Halisi waachie wana wa Asili ya Tz! {Mtazamo tu Kaka usikunje Ndita.}
 
Back
Top Bottom