Ibara ya 24:3 ya Sheria ya Utumishi wa Umma ina maana gani? Rais anaweza kumlazimsha jaji kustaafu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ibara ya 24:3 ya Sheria ya Utumishi wa Umma ina maana gani? Rais anaweza kumlazimsha jaji kustaafu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 24, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa katika kujisomeasomea na kutafiti kitu fulani lakini nimekutana na hiki kipengele sijakielewa hasa. Ibara ya 24 ya sheria hiyo ya 2002 inazungumza kuondolewa kwa watumishi wa umma na inaanza kwa kusema kuwa


  Na sehemu ya 3 inasema kuwa:

  Sasa najiuliza; ina maana kuwa Rais anaweza kumlazimisha Jaji wa Mahakama Kuu au wa Rufaa kustaafu? Inaposema "save that where" maana yake ni "isipokuwa pale ambapo" .. naomba mwanga kidogo itanisaidia katika kajiutafiti kangu fulani. Au kipengele hicho hakipo tena na kuwa majaji hawawezi kuondolewa na Rais isipokuwa kwa kanuni iliyowekwa kwenye Katiba?
   
 2. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Many lawyers prefer to read only few like to write. Let the only few share with us the clarification of those sections from their proffesional eyes.

  Back to topic, that concluded Mahakama si huru. Kama watoto wanamtegemea baba kwa uongozi na baba ni mtumwa kisheria, ni upuuzi kwa watoto kusema wako huru.
   
 3. A

  Apta Kayla JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza naomba kufanya marekebisho kidogo, neno 'Ibara' linatumika tupapozumzia KATIBA, kwenye SHERIA tuna 'Kifungu' hivyo unachozungumzia ni Kifungu cha 24 kwenye Sheria Namba 8 ya 2002 Sheria ya Utumishi wa Umma.
  Nadhani umepata point nzuri tu kwamba utaratibu wa kuwaondoa Majaji na Mahakimu wa High Court ni tofauti, kuna procedure za kufuata kama zilivyoelekezwa kwenye Katiba, taratibu hizo zikikamilika Judge/Hakimu huyo anatangazwa amestaafu kwa manufaa ya umma. Kwa hiyo ni kweli Rais anaweza kumstaafisha kazi mtumishi yeyote wa Umma, kwa madaraka aliyopewa na Sheria ya Utumishi wa Umma isipokuwa kwa watumishi hao wa mahakama, anachofanya yeye ni kuanzisha hiyo hoja then taratibu zilizotajwa kwenye katiba zinafuata na zikikamilika na ikathibitika hoja ya Rais in ushahidi na faida kwa Umma, Judge/Hakimu huyo atastaafishwa.
  Nadhani kilichokuchanganya ni hiyo tafsiri ya google ya 'save that where' katika 'content' hiyo isipokuwa pale si tafsiri iliyokusudiwa. Ni kukosekana tu kwa neno zuri la muendelezo ndio kumepelekea ugumu wa kupata tafsiri iliyokusudiwa.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nashukuru sana kwa usahihisho; kwenye katiba inasemwa ni tume ndio kimsingi inafanya uchunguzi na ikiwa na ushahidi wa kutosha inapendekeza kwa Rais jaji au hakimu kuondolewa kwa manufaa ya umma. Kwa hiyo, ni salama kusema kuwa Rais hawezi kumstaafisha jaji wa mahakama kuu au rufani au mtumishi wa mahakama bibila kuhusisha tume. Hawezi tu kutangaza kuwa ameamua kumstaafisha jaji au mtumishi wa mahakama bila kuundwa kwa tume kama article 110 ya katiba inavyotaka?
   
 5. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Kuongezea ni kwamba judge au magistrate ataondolewa kwenye utumishi sio rais anaposema tu bali yeye ataondolewa baada ya judicial commission kukaa na kuamua kama kweli kuna haja ya kufanya hivyo, kwa maana hiyo haki zake zote za malipo na mengineyo hufuata. Hicho ndo kinachoongelewa hapo. Ni kawaida kabisa kwani kumbuka hakuna total independence ya organ of the state bila check and balance. Na ili kupunguza tyranny na unscrupulous behaviour katika kumuondoa judge ndipo commission hukaa kuangalia umuhimu wa kufanya hivyo hapo swali hubakia kama kweli hiyo tume ya maadili ya mahakama itatenda haki kwa mhusika.
   
 6. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hivi Jaji anapotoa maamuzi ya kipuuzi kama alivyofanya kwenye kesi ya Lema Arusha anawajibishwa kivipi na hiyo Commission? au ndio mpaka Rais alianzishe? huku tukiwa tumesahau kuwa huyo huyo Rais ndie alimpendekeza, Akamu interview, akamchagua, akamwajiri, akamthibitisha kazini etc..

  Kweni wenzetu wa Kenya wanafanyaje katika hoja hii?
   
 7. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Mambo ya kenya ni yao mkuu, cha muhimu unatakiwa kufahamu judge anapotoa maamuzi ya kesi anakuwa 'functus officio' na kuna kinga anayopata kwa maamuzi hayo. Kuna njia mbalimbali za kuweza kupata suluhisho kama kukata rufaa nk. Ila kumbuka jaji au hakimu sio watu wa kudhaniwa kuwa na uhuni wa namna hiyo lakini pindi itakapofahamika mahakama ya juu yaweza kutengua hukumu hiyo either by its own motion au kwa kupelekewa.
   
Loading...