Ibara ya 15:1 na 2

Hongereni kwa ku-spin mambo!!! Hivi kujiunga CCM si hiari!!! Kama hukubaliani, si unakuwa nje kama mimi, sasa kuna haja gani ya Ku-spin.

Kila siku zinavyoenda hizi spinning strategy zinaendelea kuweka wazi kwamba kumbe CCM wako fiti zaidi.

Sasa ma-think tank wa Upinzani badala ya kuja na mambo yao... kueneza siasa zao wanapata shida na wanaCCM ambao wanabadilisha katiba yao kwa vikao... wanatoa matamko kwa vikao...

Mkuu,

Wengine si si si wanasiasa ila tunapenda kuona mabadiliko.

CCM kwa sasa inaonekana bado imara mno.

Sasa kama ni hivo itabidi pawepo watu kama Simba Makoni ambae huja kuvuruga uchaguzi kiufundi.
 
Mwalimu angekuwepo na kuona waliyoyafanya kina Mkapa, JK na ukimya wa vigogo wengine wa CCM, angerudisha kadi jangwani!! Hakuwa anajikomba kwa mtu yeyote ndani ya CCM.

Mkuu heshima mbele,

1. sasa ilikuwaje hakurudisha kadi kwenye uchaguzi wa visiwani, ambao sio siri CCM ilishindwa mwaka 1995?

2. NBC ilipouzwa na Mkapa, tena kwa bei poa na chaguo lake mbona hakurudisha kadi CCM?

3. Lowassa aliporudi cabinet, mbona hakurudisha kadi?

Akili yangu eti ina kutu, no way mkuu, katiba ya CCM ni reflcetion ya mawazo ya Mwalimu, tena ndio maana sasa CCm wamemua kumuenzi maana kuna sehemu wamegundua kuwa walikuwa wanakosea, that is my point na ninasema kuwa ili Tanzania tuendelee tunahitaji kuachana na hizo fikra za Mwalimu, huenda zilikuwa valid enzi hizo, lakini sasa hivi tunachohitaji na respect kwa the rule of law ya jamhuri yetu, sio katiba za vyama vya siasa.

Mwalimu, amefanya mengi mazuri kwa taifa letu, lakini the time has now come, tunahitaji kuachana na fikra zilizopitwa na wakati, maana kwa mfano, Mwalimu alijua kuwa Lowassa, ni mla rushwa na ushaidi alikuwa nao, lakini akamzuia tu asiwe rais, badala ya kumfikisha kwenye sheria, sasa cha ajabu ni kipi cha CCM ya sasa kurudia yale yale ya Mwalimu, ya kumruhusu Lowassa kujiuzulu tu? badala ya kwenda kwenye sheria ni kwa sababu bado wanafuata mawazo yale yale yaliyopitwa na wakati.
 
Wewe kweli unampenda Nyerere...
Sitabishana tena na wewe kuhusu yeye...

hhahahaha nimecheka kweli.. ukweli ni kuwa siyo kumpenda Mwalimu bali kuupenda ukweli. Kama mtu akija na kutoa kauli za kuhukumu k.v "fulani alisema hivi" au "alifanya vile" ni jukumu la mtu yeyote mwenye akili timamu kuhoji je ni kweli fulani alisema au kufanya yanayosemwa?

Mtu ambaye hataki kufikiri atakubali mara moja na kusema "duh kumbe fulani alifanya hivi au vile" na kama ni jambo la chuki basi chuki hupandikizwa na kama ni jambo la mapenzi basi mapenzi hupandikizwa.

Kwenye suala la Mwalimu kuna mengi yanasemwa juu yake. Kuwa alisema hivi au alifanya vile; mwisho yanakuwa kama ya Hillary. Tatizo ni kuwa karibu kila kitu ambacho mwalimu alikisema hadharani kimeandikwa mahali (na hapa nina maana tangu aingie kwenye uongozi wa kisiasa wa nchi).

Hivyo mtu akisema Mwalimu alisema hivi mtu ana hiari ya kuamini au kukataa kwa sababu yaliyosemwa yanajulikana, yapo na yanaweza kuthibitishwa. Ndio maana uliposema Nyerere alisema "Bila CCM Tanzania itayumba" nilikukatilia kwa sababu sicho alichosema Nyerere lakini mtu mwingine anaweza kuamini ulichosema.

Sasa, kosa kubwa ambalo CCM watakuwa wamelifanya juzi Butiama na ambalo watalijutia ni kukusanya maandishi yote ya Nyerere na kuyatafsiri na kuyaweka pamoja. Bora wafanya baada ya uchaguzi wa 2010 kwani wakifanya kabla ya hapo itakuwa ni kutengeneza mafuta ya kuwakaangia. Believe me, it is not in the interest ya CCM kukusanya maandishi hayo na kuyafanya yapatikane kiurahisi. Itakuwa ni kama Martin Luther alipotafsiri Biblia kwenda Kijerumani na kusababisha reformation!
 
Field Marshall....hapa utakesha ndugu yangu! Mwanakijiji hasikii wala haambiwi la mtu kuhusu Nyerere. Ni bora tu mkubaliane kutokubaliana muendelee na mijadala mingine.
 
Kwa hiyo basi:-
(1) Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa
pamoja wa TANU na ASP tuliokutana leo
tarehe 21 Januari, 1977 mjini Dar es Salaam,
chini ya uongozi wa pamoja wa Mwalimu Julius
K. Nyerere Rais wa TANU na Ndugu Aboud
Jumbe, Rais wa ASP, kwa kauli moja tunaamua
na kutamka rasmi kuvunjwa kwa Tanganika

African National Union (TANU) na Afro Shirazi
Party (ASP) ifikapo tarehe 5 Februari, 1977, na
wakati huo huo kuundwa kwa Chama kipya cha
pekee na chenye uwezo wa mwisho katika
mambo yote kwa mujibu wa Katiba.

Yaaani mkulu wangu MMJ, unaaamini hii mikenge ya Mwalimu? Kama kweli aliwashirikisha kwenye maamuzi muhimu namna hii matatizo ya muafaka yanatokea wapi mkuu?
 
hapa utakesha ndugu yangu! Mwanakijiji hasikii wala haambiwi la mtu kuhusu Nyerere. Ni bora tu mkubaliane kutokubaliana muendelee na mijadala mingine.

Hapana mkuu wangu Nyani, hamna noma mijadala kama hii huwa inaelimisha sana kuhusu tulikotoka, yaaani sababu hasa ya kuwa tulipo sasa, na hii forum ina watu makini sana kwenye kuamua hoja nzito ilipo kwa hiyo usiwe na wasi wasi mkuu wangu,

Ninasema Mwalimu, was great ametufanyia mambo mengi mazuri as a nation, lakini mawazo yake mengi sasa yamepitwa na wakati, ni wakati wa sisi wa-Tanzania kuamua wapi tunataka kwenda, lakini cha muhimu tuanze na kuheshimu sheria zetuza taifa, badala ya mambo ya katiba za chama.
 
Sasa, kosa kubwa ambalo CCM watakuwa wamelifanya juzi Butiama na ambalo watalijutia ni kukusanya maandishi yote ya Nyerere na kuyatafsiri na kuyaweka pamoja. Bora wafanya baada ya uchaguzi wa 2010 kwani wakifanya kabla ya hapo itakuwa ni kutengeneza mafuta ya kuwakaangia.

Mkuu again heshima mbele, sasa CCM watajikaaanga mara ngapi? Maana kama hawakujikaaanga kwenye mafisadi na bado ndio kwanza wanashinda kiteto, basi hata wakuyaweka maandishi yote ya Mwalimu haitasaidia kitu, au?
 
hhahahaha nimecheka kweli.. ukweli ni kuwa siyo kumpenda Mwalimu bali kuupenda ukweli. Kama mtu akija na kutoa kauli za kuhukumu k.v "fulani alisema hivi" au "alifanya vile" ni jukumu la mtu yeyote mwenye akili timamu kuhoji je ni kweli fulani alisema au kufanya yanayosemwa?

Mtu ambaye hataki kufikiri atakubali mara moja na kusema "duh kumbe fulani alifanya hivi au vile" na kama ni jambo la chuki basi chuki hupandikizwa na kama ni jambo la mapenzi basi mapenzi hupandikizwa.

Kwenye suala la Mwalimu kuna mengi yanasemwa juu yake. Kuwa alisema hivi au alifanya vile; mwisho yanakuwa kama ya Hillary. Tatizo ni kuwa karibu kila kitu ambacho mwalimu alikisema hadharani kimeandikwa mahali (na hapa nina maana tangu aingie kwenye uongozi wa kisiasa wa nchi).

Hivyo mtu akisema Mwalimu alisema hivi mtu ana hiari ya kuamini au kukataa kwa sababu yaliyosemwa yanajulikana, yapo na yanaweza kuthibitishwa. Ndio maana uliposema Nyerere alisema "Bila CCM Tanzania itayumba" nilikukatilia kwa sababu sicho alichosema Nyerere lakini mtu mwingine anaweza kuamini ulichosema.

Sasa, kosa kubwa ambalo CCM watakuwa wamelifanya juzi Butiama na ambalo watalijutia ni kukusanya maandishi yote ya Nyerere na kuyatafsiri na kuyaweka pamoja. Bora wafanya baada ya uchaguzi wa 2010 kwani wakifanya kabla ya hapo itakuwa ni kutengeneza mafuta ya kuwakaangia. Believe me, it is not in the interest ya CCM kukusanya maandishi hayo na kuyafanya yapatikane kiurahisi. Itakuwa ni kama Martin Luther alipotafsiri Biblia kwenda Kijerumani na kusababisha reformation!

Kuhusu Tanzania bila CCM...nilienda tena kule kwenye podomatic na nikaona kuwa wewe umesema yeye alisema Tanzania bila CCM "madhubuti" itayumba. Pia nikasikiliza tena commentary yako na nikaona kuwa ulikuwa unatafsiri maneno yake. Katika kutoa tafsiri za kauli ya mtu, inawezekana kabisa kutoa tafsiri kwa mtazamo wako wewe kulingana na mambo mengi yanayokufanya utafsiri hivyo unavyotafsiri. Sasa kama wewe ulitafsiri hivyo ulivyotafsiri haina maana mwingine asiyatafsiri hayo maneno kwa mtazamo wake. Labda uniambie kuna mahala Mwalimu ali-clarify alichokuwa ana maanisha.

All in all I like how you passionately defend him and to be honest with you, you are the one I want in my corner when I'm in trouble.
 
Mkuu heshima mbele,

1. sasa ilikuwaje hakurudisha kadi kwenye uchaguzi wa visiwani, ambao sio siri CCM ilishindwa mwaka 1995?

2. NBC ilipouzwa na Mkapa, tena kwa bei poa na chaguo lake mbona hakurudisha kadi CCM?

3. Lowassa aliporudi cabinet, mbona hakurudisha kadi?
Majibu ya maswali yako hayo ni kuwa kama mtu huru alikuwa na haki ya kuamua kurudisha kadi au la kwa misingi yake yeye siyo kwa misingi ya wewe na mimi; kama wakati ule hakuona tayari kurudisha kadi ilikuwa ni haki yake. Tutajua siku moja kwanini hakujiengua CCM na kwanini alijaribu kuisahihisha sana baada ya 1995 ndio maana wakati wa kufa kwake pale London kauli yake ya kwaheri haikuwa "waambieni wanaCCM wangu niliwapenda"..

Akili yangu eti ina kutu, no way mkuu,

Once again, natumia maneno yangu vizuri sana, sijasema akili yako ina kutu, siwezi kusema hivyo, na sitosema hivyo kwa mtu yeyote yule. Nimeandika dakika chache zilizopita nukuu nilichosema mzee usiniwekee maneno kinywani.

katiba ya CCM ni reflcetion ya mawazo ya Mwalimu,
Mzee hii ni hoja tofauti kabisa na uliyotoa mwanzo; mwanzoni ulisema ni yeye aliyebuni na kuandika katiba hiyo? sijui kama unakumbuka lakini sasa unasema ni reflection? Of course ni reflection ya mawazo ya watu wengi akiwemo Nyerere; ni reflection ya wajumbe wa Mkutano mkuu uliounda CCM.

tena ndio maana sasa CCm wamemua kumuenzi maana kuna sehemu wamegundua kuwa walikuwa wanakosea,

Hapana, wanaamua kumuenzi kwa sababu wameziacha fikra za Mwalimu na hawana cha kushikilia wanafikiri zile fikra zinaweza kupenyezwa kwao toka kaburini kwa njia ya mnunurisho.

that is my point na ninasema kuwa ili Tanzania tuendelee tunahitaji kuachana na hizo fikra za Mwalimu, huenda zilikuwa valid enzi hizo, lakini sasa hivi tunachohitaji na respect kwa the rule of law ya jamhuri yetu, sio katiba za vyama vya siasa.

Mzee, tumeziacha fikra za Nyerere mbona miaka mingi iliyopita, mbona hatujaendelea? Labda ni kile alichokisema yeye mwenyewe kuwa "kuwa jukumu la uongozi unaofuatia ni kuangalia sisi tumefanikiwa wapi na tumekosea wapi, hivyo kuacha yale tuliyokosea na kushikilia yale ya msingi; lakini nyinyi mmeacha siyo tu tuliyokosea sisi bali hata yale ya msingi!". (Mei Mosi 1995.

Mwalimu, amefanya mengi mazuri kwa taifa letu, lakini the time has now come, tunahitaji kuachana na fikra zilizopitwa na wakati,

Mazuri gani aliyoyafanya Nyerere ambayo tuyaache? Ni fikra zipi za Mwalimua ambazo zimepitwa na wakati? Kwamba maendeleo ni ya watu na siyo vitu ni fikra zilizopitwa na wakati; kwamba kujenga Taifa la watu walio huru na sawa ni fikra zilizopitwa na wakati? Kuwa kabla ya wachache wetu hawajaishi katika anasa wengi wetu wapate mahitaji yao muhimu ni fikra zilizopitwa na wakati? Kwamba elimu ni haki kwa kila mtu imepitwa na wakati? Kuwa mtu ni afya ni fikra zilizopitwa na wakati? kuwa kila mtu ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake ni fikra zilizopitwa na wakati? Kuwa Tanzania ndio kusudio la utumishi wote wa umma ni mawazo yaliyopitwa na wakati? kuwa maendeleo hayaji kwa pesa ni fikra zilizopitwa na wakati? Ni zipi hizi zilizopitwa na wakati mkuu?

maana kwa mfano, Mwalimu alijua kuwa Lowassa, ni mla rushwa na ushaidi alikuwa nao, lakini akamzuia tu asiwe rais, badala ya kumfikisha kwenye sheria,

Mzee usimbebeshe Nyerere ufisadi wa Lowassa. Yaani ni Nyerere tu aliyejua kuhusu hayo unayoyasema kuhusu Lowassa? Mbona hawa wengine wakampa uwaziri hadi uwaziri mkuu? Yaani sasa unamtaka Nyerere angekuwa Polisi, mwanasheria mkuu n.k Mimi nadhani wewe unampa Nyerere nguvu nyingi za kiungu na uwezo mkubwa karibu na wa malaika kiasi kwamba angeweza kufanya yote hayo na huwezi kuona limitations zake kama mwanadamu.

sasa cha ajabu ni kipi cha CCM ya sasa kurudia yale yale ya Mwalimu, ya kumruhusu Lowassa kujiuzulu tu? badala ya kwenda kwenye sheria ni kwa sababu bado wanafuata mawazo yale yale yaliyopitwa na wakati.

Cha ajabu ni kuwa Nyerere alikufa 1999!!!
 
Mzee, tumeziacha fikra za Nyerere mbona miaka mingi iliyopita, mbona hatujaendelea?

Hapana mkuu, kuna maendeleo makubwa sana mkuu, kama freedom of speech, umiliki wa mali binafsi, tatizo ni kwamba maendeleo haya hawakupata wengi kama ambavyo tungetaka, hasa wananchi wa hali ya chini, lakini mabadiliko yapo mengi sana mkuuu, hivi mkuu huoni kuwa siku hizi wananchi tunakula luninga?

Labda ni kile alichokisema yeye mwenyewe kuwa "kuwa jukumu la uongozi unaofuatia ni kuangalia sisi tumefanikiwa wapi na tumekosea wapi, hivyo kuacha yale tuliyokosea na kushikilia yale ya msingi; lakini nyinyi mmeacha siyo tu tuliyokosea sisi bali hata yale ya msingi!". (Mei Mosi 1995.

nia yake ingekuwa ni njema kwa taifa, basi angeyasema mwenyewe aliyoyakosea, na aliyeyakosea ni yeye binafsi maana viongozi wengine walikuwa wanafuata upepo tu! Lakini hata siku moja hakusema alikosea wapi, ndio maan sasa tunahangaika tuu hatujui pa kugusa?

Mazuri gani aliyoyafanya Nyerere ambayo tuyaache? Ni fikra zipi za Mwalimua ambazo zimepitwa na wakati?

Mambo ya maazimio ya Arusha, yamepitwa sana mambo ya maadili ya viongozi yamepitwa sana tunatakiwa kuheshimu sheria za jamhuri sio maadili ya CCM

Kwamba maendeleo ni ya watu na siyo vitu ni fikra zilizopitwa na wakati; kwamba kujenga Taifa la watu walio huru na sawa ni fikra zilizopitwa na wakati?

Maendeleo ya watu mbona yeye mwenyewe yalimshinda kuya-implemment tikaishia kula yanga tu, huku wakubwa na wenye nguvu wakila unga mweupe, angalau sasa hata wanyonge tunapata angalau harufu maana ni hela yako tu, watu walio huru aliwajenga wapi mbona kina Seif Bakari, Seif Hamadi, na Jumbe walipojaribu kuwa huru aliwafukuza? Can you imagine Zitto na Salaa wangekuwepo enzi zile za Mwalimu, saaa hizi wangekuwa wapi?

Haya ndio baadhi ya maandishi ya Mwalimu, ninayosema kila wakati yalikuwa mazuri kusoma tu, ila kwa sasa yamepitwa na wakati tena sana!
 
Mzee usimbebeshe Nyerere ufisadi wa Lowassa. Yaani ni Nyerere tu aliyejua kuhusu hayo unayoyasema kuhusu Lowassa? Mbona hawa wengine wakampa uwaziri hadi uwaziri mkuu? Yaani sasa unamtaka Nyerere angekuwa Polisi, mwanasheria mkuu n.k Mimi nadhani wewe unampa Nyerere nguvu nyingi za kiungu na uwezo mkubwa karibu na wa malaika kiasi kwamba angeweza kufanya yote hayo na huwezi kuona limitations zake kama mwanadamu.

I like this one mkuu, maana Kasori mtu wa karibu sana na Mwalimu, ndiye anaweza kujibu hili, jinsi Mwalimu alivyomzuia Lowassa kuwa rais, na nguvu za ajabu alizokuwa nazo Mwalimu, mpaka kumuita Kawawa mjinga, unasema huyu mtu alikuwa na nguvu za kawaida?
 
Yaani Rufiji unanishangaza. Unataka kusema Mwalimu aliaacha kujenga daraja lako miaka 24 yote aliyokuwa madarakani akisubiri alijenge wakati wa Mkapa? Na mbona hakulijenga wakati wa Mwinyi?

Kwa taarifa yako, Mwalimu hakujali kabisa usafiri wa Kusini. Na aliona Kusini ni kama jela, ndio maana alimsukumiza Kasanga Tumbo huko kwa miaka kumi, kama adhabu.

Unataka kusema Mwalimu aliacha tukose hata sabuni ya kuogea, akisubiri ajenge supermarkets wakati wa Mkapa? Mtu aliyesema kukosekana vitu madukani ni matokeo ya maendeleo unathubutu kumlinganisha na Mkapa? Unamkosea sana haki Mkapa.

Mwalimu alikataza watu wa Songea kuuza mahindi yao nje. Wakati huo huo akawanyima barabara ya kuyaleta Dar, yakabaki yanawaozea tu. Mkapa alikwenda huko akawaruhusu kuyauza kwa yoyote yule. Wewe utasema ni Mwalimu aliwakomboa? Usidanganye.

Mwalimu alipokea nchi iliyokuwa inatumia 20% ya bajeti kwenye Elimu. Alianza kubomoa Elimu kwa matendo, na kwa kuinyima fedha, na kufikia wakati anaondoka madarakani, alishashusha bajeti ya Elimu hadi kufikia asilimia 4.9 tu ya bajeti yote.

Mwalimu aliua shule nzuri kama St. Francis (Pugu), St. Andrew's (Minaki), Miriam College (Kilakala), Assumption College (Weru Weru), etc. Baya zaidi ni kwamba alikataza kabisa kuanzishwa kwa shule nyingine kama hizo.

Mwalimu huyo huyo ndiye aliwafundisha akina Malecela, na CCM kwa ujumla, naman ya kuiba kura. Hilo bado linatutesa.

Labda Mwalimu alikuwa na nia nzuri, lakini ukweli ni kwamba aliturudisha nyuma sana. Si haki useme kazi nzuri za Mkapa ni kazi za Mwalimu.

Hiii nimeitoa hukooo, vipi nayo imekaaje hii?
 
Uuuhuuuu! but wajibu wa pili ni..

Kufanya ufisadi na uhuni ili kuhakikisha kwamba viongozi wote wa CCM wanakuwa mabilionea hasa ikitiliwa maanani kwamba vyombo vyote vya dola viko chini ya CCM. Na kwa kuwa CCM ndiyo yenye nguvu na uwezo basi hakuna baya lolote litakalowapata viongozi wa CCM. Kigumu chama cha mafisadi, kigumu!
 
Hapana mkuu, kuna maendeleo makubwa sana mkuu, kama freedom of speech, umiliki wa mali binafsi, tatizo ni kwamba maendeleo haya hawakupata wengi kama ambavyo tungetaka, hasa wananchi wa hali ya chini, lakini mabadiliko yapo mengi sana mkuuu, hivi mkuu huoni kuwa siku hizi wananchi tunakula luninga?

Mzee maendeleo ya vitu yapo na ni kweli kuna watu wachache wameendelea na kauli yangu ya "mbona hatujaendelea" naifuta kwani siku iqualify nilivyotaka. Maendeleo ambayo tunayazungumzia siyo mabadiliko yanayoendana na wakati, yaani kama ulikuwa na shule 20 halafu miaka 10 baadaye ukawa na shule 40 unaweza kusema umeendelea lakini ukweli ni kuwa umekidhi natural demand ya shule.

Sasa isingiwezekana Tanzania kubakia vile ilivyokuwa pasipo mabadiliko ya ongezeko la vitu; je tulivyoongeza ni bora zaidi kuliko tulivyokuwa navyo?

nia yake ingekuwa ni njema kwa taifa, basi angeyasema mwenyewe aliyoyakosea, na aliyeyakosea ni yeye binafsi maana viongozi wengine walikuwa wanafuata upepo tu! Lakini hata siku moja hakusema alikosea wapi, ndio maan sasa tunahangaika tuu hatujui pa kugusa?

Once again, unazungumza kwa uthabiti kuwa "hata siku moja hakusema alikosea wapi" sasa nikikuonesha kuwa aliwahi kusema alikosea wapi utafuta kauli hiyo na hiyo kuthibitisha kuwa hujafuaitilia yote aliyoyasema na unajenga hoja kwa imani siyo facts? Well, nitakusaidia.

Alifanya interview mwezi Disemba 1998 karibu mwaka mmoja kabla ya kifo na aliulizwa na mwandishi wa "New Internationalist Magazine" toleo la 309:

Sehemu ya Mahojiano ilikwenda hivi:

IB: What were your main mistakes as Tanzanian leader? What should you have done differently?

MJN: There are things that I would have done more firmly or not at all. For example, I would not nationalize the sisal plantations. This was a mistake. I did not realize how difficult it would be for the state to manage agriculture. Agriculture is difficult to socialize. I tried to tell my government that what was traditionally the family's in the village social organization should be left with the family, while what was new could be communalized at the village level. The land issue and family holdings were very sensitive. I saw this intellectually but it was hard to translate it into policy implementation. But I still think that in the end Tanzania will return to the values and basic principles of the Arusha Declaration.

Mzee katoa mfano! viongozi hawaogopi kukiri makosa na kusema walikosea wapi. Na madai yako kuwa hakuwahi kusema amekosea wapi hayana ukweli, kwa sababu nimekupa mfano mmoja kama hautoshi niombe nitakupa mwingine na mwingine tena.
Mambo ya maazimio ya Arusha, yamepitwa sana mambo ya maadili ya viongozi yamepitwa sana tunatakiwa kuheshimu sheria za jamhuri sio maadili ya CCM

Mzee, nakuomba usome Azimio la Arusha halafu nioneshe ni nini kilichopitwa na nakuhakikisha utakuta kitu kimoja tu ambacho na mimi sikikubali. Azimio bado lina uhai ni wahuni wale walioliua kule leo hii hawana cha kushikilia. Wamebakia kutembelea kaburi.

Maendeleo ya watu mbona yeye mwenyewe yalimshinda kuya-implemment tikaishia kula yanga tu, huku wakubwa na wenye nguvu wakila unga mweupe, angalau sasa hata wanyonge tunapata angalau harufu maana ni hela yako tu, watu walio huru aliwajenga wapi mbona kina Seif Bakari, Seif Hamadi, na Jumbe walipojaribu kuwa huru aliwafukuza? Can you imagine Zitto na Salaa wangekuwepo enzi zile za Mwalimu, saaa hizi wangekuwa wapi?

mzee kujenga Taifa si lelemama, hivi umesoma historia ya Wamarekani? Umeshawahi kumsikia mtu anaitwa Benedict Arnold au watu wengine ambao walikuwa upande wa Mfalme.Kujenga Taifa siyo kula keki, believe me, compared to others around us.. Mwalimu alifanya kazi kubwa kweli, nisingetaka kuzaliwa nchi nyingine yoyote ya kiafrika isipokuwa Tanzania chini ya Nyerere. Hivi unafikiri kina Mkapa ndio wangekuwa Marais wa Kwanza Tanzania ingekuwa ilivyo sasa? thubutu!! tungeuza hadi jengo lenyewe la Ikulu.

Kweli baadhi yetu hatuna shukrani na mchango wa Taifa ambalo leo tunasema tunafurahia. Mzee wakati wa Nyerere tulikula Yanga.. leo hii watu bagamoyo wamekufa kwa kula mizizi!!! Mzee tulikula Yanga na tulikuwa na afya, Ethiopia katika njaa ile ile waliimbiwa "we are the world". Tuwe na shukrani kaka, niishi katika nchi ambayo angalau naweza kula Yanga, kuliko nchi ambayo wachache wanakula pilau wengine tunaishia mizizi. Nenda pale Mwaloni uone ni watu wangapi huishia kuokoteza vidagaa pale, ni wangapi wanakula mapanki (well matamu pia).

Haya ndio baadhi ya maandishi ya Mwalimu, ninayosema kila wakati yalikuwa mazuri kusoma tu, ila kwa sasa yamepitwa na wakati tena sana!

Nakupa changamoto, pick any writing of Mwalimu na unioneshe kuwa yamepitwa na wakati na kwanini yamepitwa na wakati.
 
Yaaani mkulu wangu MMJ, unaaamini hii mikenge ya Mwalimu? Kama kweli aliwashirikisha kwenye maamuzi muhimu namna hii matatizo ya muafaka yanatokea wapi mkuu?

Mzee mbona unaruka hoja; hivi Nyerere alishauri nini baadaya matokeo ya 1995 kuhusu Zanzibar? Hivi unafikiri kama wangemsikiliza tungekuwa na matatizo haya. Ningependa kuwaona hawa wajumbe wa ASP na TANU waliokuwa wamezungukwa na vikosi vya jeshi na walioshikiwa bunduki kichwani kuambiwa wasema "sisi"!
 
Ninasema Mwalimu, was great ametufanyia mambo mengi mazuri as a nation, lakini mawazo yake mengi sasa yamepitwa na wakati, ni wakati wa sisi wa-Tanzania kuamua wapi tunataka kwenda, lakini cha muhimu tuanze na kuheshimu sheria zetuza taifa, badala ya mambo ya katiba za chama.

naomba unisaidie ni mambo gani ambayo yalimfanya Mwalimu kuwa "great"? na naomba unipe kiasi kidogo tu cha "mambo mengi mazuri" kwa Taifa ambayo Nyerere aliyafanya. Halafu ni mawazo yake yepi "mengi yamepitwa na wakati"?
 
Mkuu again heshima mbele, sasa CCM watajikaaanga mara ngapi? Maana kama hawakujikaaanga kwenye mafisadi na bado ndio kwanza wanashinda kiteto, basi hata wakuyaweka maandishi yote ya Mwalimu haitasaidia kitu, au?

Mzee do not underestimate the power of a book! rudi kwenye historia utashangaa. Ndio maana leo tunawasoma kina Socrates na Plato! na wao waliishi miaka ileeee!! Fikra zenye nguvu hazipitwi na wakati. Kwenye dhana za elimu, falsafa ya mwalimu kuhusu elimu inafundishwa hata leo. Jaribu kugoogle "Nyerere and Education" utashangaa na utajua we had a great thinker in our midst.

Binafsi nawashauri CCM wasichapishe maandishi ya Mwalimu kwa ajili ya usalama wao wenyewe kwani wananchi wakifunguka mawazo na kuelewa ni nini Mwalimu alikuwa anasimamia, wamekwisha. Kama anavyojiita mtu mmoja hapa "nikifufuka mmekwisha"; na mawazo ya Mwalimu yakipata uhai mpya, mafisadi wa Tanzania watakiona cha moto!
 
I like this one mkuu, maana Kasori mtu wa karibu sana na Mwalimu, ndiye anaweza kujibu hili, jinsi Mwalimu alivyomzuia Lowassa kuwa rais, na nguvu za ajabu alizokuwa nazo Mwalimu, mpaka kumuita Kawawa mjinga, unasema huyu mtu alikuwa na nguvu za kawaida?

Mzee kumuita mtu mjinga haihitaji nguvu, kuwaita watu wazima wapumbavu inahitaji nguvu ya hoja. Nyerere aliuita uamuzi wa CCM wa kipumbavu na walikuwa wanamkodolea macho! Mjinga hubakia kuwa mjinga hata kama anavaa suti na kumuita mjinga humuongezei sifa ambayo hana.
 
naomba unisaidie ni mambo gani ambayo yalimfanya Mwalimu kuwa "great"? na naomba unipe kiasi kidogo tu cha "mambo mengi mazuri" kwa Taifa ambayo Nyerere aliyafanya.

Alituletea uhuru on time, na pia alituletea umoja, akaondoa udini na ukabila.

Halafu ni mawazo yake yepi "mengi yamepitwa na wakati"?

1. Maazimio ya Arusha, yaani viongozi lazima wawe masikini kwa maana kwamba viongozi wote wa upinzani sasa na CCM wote wangetakiwa kuwa un-qualified under mawazo ya Mwalimu, maana sio unaona karibu wote wako sawa kipesa.

2. Mambo ya chama kushika hatamu yamepitwa sana.

3. Wananchi kuogopeshwa kuzumgumza ukweli wa siasa ya taifa lao, yalipitwa hayo.

4. Wananchi wote kwenye taifa kuwa sawa, au siasa za ujamaa leo ni a big joke hilo limewashinda hata wa-Rusi waanzilishi wa ujamaa wake, haya yamepitwa kabisaaa na time.

5. Siasa kwenye uchumi, yaani mwenyekiti wa tawi la CCM kiwandani anamtisha meneja, hayo yamepitwa sana.

6. Elimu bure na afya bure, ndio hayo taifa letu linalipia mpaka leo.

Mkuu wangu MMJ, kama kweli unaataka maendeleo na mabadiliko kwa taifa letu, kisiasa na kisheria, licha ya uchumi, basi please achana na mawazo haya yaliyopitwa na wakati, tunataka mawazo mapya ya kizazi kipya, sasa upinzani nao wakiaanza kuimba nyimbo za zamani za CCM sasa nafuu yetu wananchi itatoka wapi?

mkuu wangu nitarudi baadaye hii ngoma bado mbichi.....!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom