Ibara ya 102 ya Katiba ya Muungano: Seif na Balozi Idi vyeo vyao havimo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ibara ya 102 ya Katiba ya Muungano: Seif na Balozi Idi vyeo vyao havimo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 22, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Katiba ya Muungano inaweka utaratibu wa vyeo vikuu vya Serikali ya Zanzibar na inaelezea juu ya vyeo vingine au taratibu nyingine kwa mujibu wa "katiba hii (ya MUungano) na Katiba ya Zanzibar". Je Makamu wa Rais wa Zanzibar Seif na Idi wana nafasi yoyote wanapokuja kwenye Muungano. Kwa mfano, wakisimama mawaziri wa Tanzania na Waziri Mkuu wa Tanzania hawa wanasimama kama viongozi wa kitaifa?
   
 2. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hapo nilipobold ndiyo taratibu iliyofuata.
   
 3. N

  Nuru John Member

  #3
  Nov 22, 2010
  Joined: Aug 26, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua kilichotokea hapo ni kuirekebisha kidogo katiba ya Zanzibar kwa ajili ya kipindi cha mpito kwani Serikali ya Umoja wa Kitaifa si yakudumu ni ya mpito tu,sasa hapo sijui itakuwa accomodated vipi kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,any way ngoja tuwasikie Great thinkers wengine wa JF watatujuza vipi.
   
 4. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,436
  Trophy Points: 280
  :help:
  mkuu hii mada nzito.. wataalamu wa mambo ya kikatiba watusaidie katika hili
   
 5. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  another point for the need of massive overhaul (or, say; retyping) of our constitution
   
 6. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Asante kwa kulitambua tatizo hilo.
  Maalim na Balozi wanatambulika na Katiba ya Zanzibar kama viongozi wa taifa lao. Katiba ya JMT haikurekebishwa kupokea mabadiliko hayo ya karibuni. Tatizo linaonekana hata pale walipoketi Bungeni pembeni mwa spika hivi karibuni.
  Ikumbukwe kuwa wazanzibar walipendekeza Rais wa SMZ arudishiwe cheo chake cha Makamu wa kwanza wa Rais. Kwa hio kuna mambo kibao yanatakiwa kurekebishwa ili kuendana na marekebisho yaliyo fanywa hivi karibuni.
  Suluhu ya tatizo hilo na mengine mengi ya muungano yanatakiwa kuwekwa kwa wadau wote na katiba ya JMT iandikwe upya. Ila ndio hivyo..........ni mvutano tu.
   
 7. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hamjajua kuwa zanzibar ni nchi nyingine bada mnajipendekeza tu?waje huku ili iweje?watu 1m=25ministers = over 70 MP kwenye bunge letu = kikwete atakaoteua kuwa mawaziri halafu bado unataka wengine ni hivi TUMELIWA KWA UJINGA WA VIONGOZI WETU-TUPIGANIE KATIBA MPYA
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwenye protokali ya Jamhuri ya Muungano tuna:

  Rais
  Makamu wa Rais
  Waziri Mkuu wa Muungano
  Rais wa Zanzibar??
  Mawaziri wa Muungano au Makamu wawili wa Zanzibar
  Makamu wa Wawili wa Zanzibar au Mawaziri wa Muungano
  Mawaziri wa Zanzibar
  Wakuu wa Mikoa

  Naomba mnisaidie ikoje?
   
 9. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji, pole sana uko mbali.

  Siku ile Wanatoka Kuzindua Bunge, ilifurahisha kuona Itifaki waliyoitumia kutoka ndani ya Bunge. From that one can judge, nani ni nani katika mpangilio wa vyeo.
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Kiprotokali rais wa Zanzibar anatajwa kabla ya Waziri Mkuu wa Muungano, lakini kikatiba serikali mbili zina operate parallely bila kuingiliana.
   
 11. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Toka kushoto mbele;Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein,Makamu wa Rais Serikali ya Muungano Dk. Mohamed Ghalib Bilali,Waziri Mkuu Mizengo Kayanda Peter Pinda,na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Mh. Seif Shariff Hamad.Kushoto nyuma;Jaji Mkuu Mh. Augustino Ramadhani,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mh Anne Makinda,Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Iddi Seif,Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano,Jaji Frederick Werema na Katibu Mkuu Kiongozi,Mh. Philemon Luhanjo.

  You can now connect the dots . . . . .
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Nov 22, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji naona sasa umeelekeza nguvu zako kwenye katiba....:teeth:

  Safi sana lakini....
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kiranga, vyeo vya Serikali ya Zanzibar vya juu vimewekwa na Katiba ya Muungano na hata muundo wa serikali yake na nguvu zake uko kwenye Serikali ya Muungano. Ndio maana Rais wa Zanzibar anaapa kulinda Jamhuri ya muungano na kiapo cha serikali ya Zanzibar.
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Kumbe unaongelea kutajwa, mimi nilifikiri unaongea hierarchy. Nchi yetu bora katiba na wala si katiba bora. Ndiyo maana tushawahi kuwa na "Naibu Waziri Mkuu" Mrema ambaye hakuwemo hata kwenye katiba.

  Kuna watu wamesema kwa sababu hii ni serikali ya mpito hili halishangazi, lakini inakuwa awkward, ndiyo maana hata juzi Hamad alivyotaka kuingia bungeni ilibidi wabunge waulizwe, kwa sababu hatambuliki kwa katiba ya muungano.

  Ingekuwa vizuri mabadiliko ya katiba yaangalie vitu hivi pia.
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Nov 22, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Mimi nina shaka sana kuwa huenda hata viongozi wetu waandamizi katika serikali hawaijui katiba!!
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Katiba yenyewe haieleweki, kila ibara ya pili inaanza kwa kusema "bila ya kuathiri sehemu nyingine ya katiba hii blah blah blah..." clawbacks on clawbacks bonge la labyrinth fulani hivi.

  Sehemu moja wanakwambia kila Mtanzania ana haki ya kupiga na kupigiwa kura, sehemu nyingine wanakwambia ili kupigiwa kura lazima uwe mwanachama wa chama cha siasa. Ile haki iliyotolewa mwanzo inachukuliwa na kifungu cha pili, na the most restrictive clause wins kwa sababu most of the ibaras zinaanza na "bila kuathiri sehemu nyingine ya katiba' or some bull like that.

  Inatakiwa tuondoe huu upuuzi.

  Mara nyingine naona wamefanya makusudi tu
   
 17. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #17
  Nov 22, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Ondoa shaka na amini kuwa viongozi wengi hawajuhi katiba.
   
 18. R

  Rugemeleza Verified User

  #18
  Nov 22, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa muundo wa sasa wa muungano vyeo vyao havitambuliki kwani Katiba ya nchi haijabadilishwa kutambua hivyo vyeo. Hivyo kuja na kupokelewa kama viongozi wenye hadhi ya muungano ni kosa. Na hili ndio limekuwa tatizo la nchi yetu kwani mambo yanabadilishwa kienyeji. Vilevile ukifuata katiba ya sasa Rais wa Zanzibar ni mjumbe wa baraza la mawaziri hivyo ni kama mawaziri wengine chini ya Waziri Mkuu. Hii imebainishwa na Ibara ya 54 ya Katiba inayosema:

  54.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote.
  (2) Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiye atkayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basi mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili Rais na Makamu wa Rais hawapo Waziri Mkuu ndiye ataongoza Mikutano hiyo.

  Kwa hiyo kikatiba Raisi wa Zanzibar katika masuala yote ya Muungano yuko chini ya Waziri Mkuu. Lakini sivyo ilivyo kwani Raisi wa Zanzibar anafanywa kuwa ni kama mtu anayemfuata Raisi na baada ya hapo Makamu wa Raisi na Waziri Mkuu. Huu ni upindishaji wa wazi wa Katiba ya nchi. Kama kuna hoja kuwa mabadiliko ya 8 ya Katiba yalimshusha hadhi Raisi wa Zanzibar hilo ni suala la kufanyia kazi ili lirekebishwa na kumpa hadhi inayomstahili.

  Kuhusu vyeo vya Seif na mwenzake hivyo kwa sasa havitambuliki na katiba yetu na hivyo wanapokuja Bara wao ni raia wa kawaida na hawatakiwi kupewa heshima yoyote ile ya uongozi zaidi ya ule wa vyama vyao. Kwa hiyo ni lazima vyeo hivi vipingwe kikatiba kwamba hadhi wanayopewa haitambuliwi na katiba ya JMT. Pili ni hoja nyingine ambayo inaonyesha kuwa Katiba yetu imepitwa na wakati na ni ni muhimu kwa nchi kuwa na katiba mpya.
   
 19. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji:

  Kwa sababu tupo kwenye katiba. Basi haitakuwa vibaya kuelezea mapungufu ya katiba. Moja ya mapungufu ya katiba ya Tanzania ni kuwa detailed. Na hivyo kufanya katiba yenyewe kuwa kitabu kikubwa na kigumu.

  Hili katiba iwe a living document, vitu vingi vinatakiwa viwe abstract concepts. Kwa mfano kwa ibara ulizoelezea kuhusu serikali ya mapinduzi Zanzibar ilitakiwa iwe abstract concept tu. Katiba ingeweza kusema: "Serikali ya Zanzibar iundwe kwa kufuata taratibu za katiba ya Zanzibar".
  Kwa mfano huu katiba ingewaachia waZanzibar kuunda muundo wa serikali yao wenyewe.

  Mfano mwingine kuhusiana na abstract concept ni kufanya katiba iwe ndogo yenye kueleweka hata kwa mwananchi wa kawaida na yenye kutoa nafasi kwa vizazi vinavyokuja kutafsiri katiba kutokana na wakati wao bila kufanya mabadiliko ya katiba yenyewe. Marekani wana zaidi ya miaka 200 na katiba yao ina kurasa chini ya 40 na mabadiliko yasiopungua 30. Wakati sisi tuna kurasa zaidi ya 100 na bado hakuna kinachoeleweka.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Nov 22, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Yaani hapo mi ndo nachoka kabisa!!

  Hata baraza la mawaziri la Marekani (yenye watu zaidi ya mil. 300) ni dogo kuliko la Tanzania yenye watu mil. 37-40! Go figure.
   
Loading...