Ibara ya 100 ya Katiba ya JMT imewapa wabunge Uhuru wa kujadili Hoja na Mijadala mbalimbali bila kuingiliwa na Mhimili wala Mtu yeyote. Tusiwaingilie

My take; tuwaache wajadili na kufunguka ili tujue nani ni mwema na nani ni mnafiki.
Na mtu akiwa katika starehe yake hiyo ya Kudemka Hapaswi kuingiliwa na yeyote! Ok acha kesho ngoma iendelee kwa raha zao!
Kwa hizi kodi zetu? hapana, bora hata warudi mitaani serikali inaweza kupanga kila kitu bila matatizo.
Au tuwe na spika mwenye weledi na mwenye afya njema ya akili.
 
Kweli maisha ya Bongo ni marahis, Yaani mtu anaenda "Kudemka" ngoma ya Sindimba then anakula Ml.12 kwa mwezi, per diem, v8, kiinua mgongo Ml.250 Na posho za kila namna.

Na mtu akiwa katika starehe yake hiyo ya Kudemka Hapaswi kuingiliwa na yeyote! Ok acha kesho ngoma iendelee kwa raha zao!
kudemka ndo mama kaniacha hoi
 
Na national assembly ambapo raisi anakuwa hayupo tuliiteje kwa kiswahili au katiba imetafsiri vipi
Kiswahili hakijitoshelezi boss tunatumia neno moja - Bunge.

Lakini Kikatiba (originally written in English) inatofautisha kati ya Parliament na National Assembly.

Hii ni kwa mujibu wa Civics Form II.
 

Imetamkwa wazi kabisa wabunge wapo huru kujadili hoja na mijadala mbalimbali bila kuingiliwa na mtu au mhimili wa dola. Ipo wazi katika ibara ya 100 (1) kwa hiyo sioni haja ya kuwapangia nini cha kujadili.

Ibara ya 100 (2) imepigia mstari kabisa kuwa wabunge hawatashitakiwa kwa chochote watakacho jadili wakiwa bungeni.

My take; tuwaache wajadili na kufunguka ili tujue nani ni mwema na nani ni mnafiki.
Hawajazuiwa kujadili suala wanajadili nini? Hatukuwachagua kwenda kujadili watu bali masuala (issues) ambayo ni ya afya kwa mustakabali wa taifa letu
 
Back
Top Bottom