Ibara ya 100 ya Katiba ya JMT imewapa wabunge Uhuru wa kujadili Hoja na Mijadala mbalimbali bila kuingiliwa na Mhimili wala Mtu yeyote. Tusiwaingilie

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
FB5E434A-AE89-4AB6-92BD-B58C00C1685B.jpeg

Imetamkwa wazi kabisa wabunge wapo huru kujadili hoja na mijadala mbalimbali bila kuingiliwa na mtu au mhimili wa dola. Ipo wazi katika ibara ya 100 (1) kwa hiyo sioni haja ya kuwapangia nini cha kujadili.

Ibara ya 100 (2) imepigia mstari kabisa kuwa wabunge hawatashitakiwa kwa chochote watakacho jadili wakiwa bungeni.

My take; tuwaache wajadili na kufunguka ili tujue nani ni mwema na nani ni mnafiki.
 
😹😹 Kweli maisha ya Bongo ni marahis, Yaani mtu anaenda "Kudemka" ngoma ya Sindimba then anakula Ml.12 kwa mwezi, per diem, v8, kiinua mgongo Ml.250 Na posho za kila namna.

Na mtu akiwa katika starehe yake hiyo ya Kudemka Hapaswi kuingiliwa na yeyote! Ok acha kesho ngoma iendelee kwa raha zao!
 
😹😹 Kweli maisha ya Bongo ni marahis, Yaani mtu anaenda "Kudemka" ngoma ya Sindimba then anakula Ml.12 kwa mwezi, per diem, v8, kiinua mgongo Ml.250 Na posho za kila namna. Na mtu akiwa katika starehe yake hyo ya Kudemka Hapaswi kuingiliwa na yeyote! Ok acha kesho ngoma iendelee kwa raha zao!
Lazima tuheshimu katiba ya JMT
 
Sasa mbona hao Wabunge wenyewe badala ya kujadili hoja za msingi, wao wana demka tu? Hujafurahia kuona mama akiwakumbusha wajibu wao?

Mbona enzi zile, Hayati alimuagiza Ndugai kwenda kuwashughulikia wapinzani ndani ya Bunge, na yeye akaahidi kuwashughulikia nje ya Bunge! Na haikuchukua hata siku moja, Tundu Lissu akashambuliwa kule Dodoma!
 
Sasa mbona hao Wabunge wenyewe badala ya kujadili hoja za msingi, wao wana demka tu? Hujafurahia kuona mama akiwakumbusha wajibu wao?

Mbona enzi zile, Hayati alimuagiza Ndugai kwenda kuwashughulikia wapinzani ndani ya Bunge, na yeye akaahidi kuwashughulikia nje ya Bunge! Na haikuchukua hata siku moja, Tundu Lissu akashambuliwa kule Dodoma!!
Umepigia jibu mstari hayati alisuburi kuwashughulikia nje sababu hakuwa na mamlaka. Spika mle ndani anawashughulikia wahuni na wenye matusi.
 
Back
Top Bottom