Mhhh, hawa watu wanatupeleka siko ndo maana wanaleta mambo ya ajabu. Wametufilisi kwa kuchezea pesa za walipakodi then wanaleta mambo mengine ya kijinga kama haya.
Unafiki wa Sitta Ulianza kipindi cha Nyerere kakachapwa viboko
Mjumbe huyo wa NEC na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga aliyejipambanua kupiga vita ufisadi na vitendo viovu ndani na nje ya CCM, alisema historia ya Waziri Sitta inajionesha wazi kwamba ni 'mkorofi na msaliti mkubwa', kwani mwaka 1966 akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alishiriki maandamano hadi Ikulu kupinga sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Alisema katika harakati zao hizo za kupinga sheria hiyo iliyotaka kila mwanafunzi wa Chuo Kikuu lazima ajiunge na Jeshi la Kujenga Taifa, Baba wa Taifa wakati huo akiwa Rais wa nchi na mkuu wa chuo hicho, alilazimika kumchapa viboko Sitta kutokana na usaliti wake huo kwa serikali.
Mgeja alisema mbali na kufanya maandamano hayo, Sitta na wenzake ambao wengine ni marehemu kwa sasa walikuwa na mabango yenye ujumbe mkali kwa serikali, ukiwemo uliosema 'Onyo kali na la mwisho kwa serikali', na kwamba alikuwa akiipinga pia Serikali ya Baba wa Taifa huku akiusifu uongozi wa kikoloni.
"Huyu Sitta ambaye leo hii anawadanganya watu, kipindi hicho akisoma Chuo Kikuu alikuwa akiipinga serikali na kudai afadhali serikali ya kikoloni. Tusipoamini leo usaliti wake huu tunasubiri hadi aje shetani atuambie usaliti wa Sitta ndipo tuamini?
(1) Kwa mujibu wa Katiba hii, Nchi Washirika ni Tanganyika na Zanzibar.
(2) Serikali ya Tanganyika itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Tanganyika.
(3) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Zanzibar.
(4) Nchi Washirika zitatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na Katiba zao.
(5) Nchi Washirika zitakuwa na hadhi na haki sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano na zitatekeleza majukumu yao kwa mambo yote yasiyo ya Muungano katika mamlaka ya Nchi Washirika kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na Katiba za Nchi Washirika.
67.-(1) Kila Nchi Mshirika itateua Waziri Mkaazi atakayeratibu na kusimamia mahusiano baina ya Serikali za Nchi Washirika na kati ya Serikali ya Nchi Mshirika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta
Na Daniel Mjema, Habel Chidawali, Mwananchi
Septemba27 2014
Sitta alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana wakati akielezea kutoridhishwa kwake na kile alichodai ni namna hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Saed Kubenea inavyopotoshwa na wanaomchukia.
Dodoma. Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amesema anapokea meseji za simu zaidi ya 50 kwa siku za kumtukana na kusisitiza ataendelea kupambana kuhakikisha Katiba inayopendekezwa inapatikana.
Sitta alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana wakati akielezea kutoridhishwa kwake na kile alichodai ni namna hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Saed Kubenea inavyopotoshwa na wanaomchukia.
"Kuna baadhi ya vyombo vya habari wananichukia mimi binafsi. Wasichanganye chuki hizo na mchakato wa Bunge Maalumu," alisema Sitta na kuongeza;
"Mimi napokea matusi kila siku. Meseji zisizopungua 50 viongozi wa Chadema wameweka namba zangu katika tovuti nitukanwe kila siku hilo mimi niko tayari na mnaniona niko safi tu wala sihangaiki nalo."
"Lakini sasa Bunge Maalumu ni chombo cha kikatiba, kiko tofauti na mwenyekiti wake. Huwezi kuliadhibu Bunge Maalumu kwa sababu hupendi sura ya mwenyekiti wake," alisema.
Sitta alienda mbali zaidi na kusema, "Kwa hiyo wale wanaoendeleza hayo mapambano tuendelee na tutaendelea kupambana, lakini kazi ya Bunge Maalumu itaendelea na ndugu zangu Watanzania mjue tunaandaa Katiba safi na rafiki kwa wananchi na itapatikana."
Sitta alisema baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo ya kesi ya Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kumekuwa na tafsiri alizosema ni potofu.
Baada ya maelezo hayo alimpa ruksa AG, Jaji Frederick Werema kutoa ufafanuzi.
Jaji Werema alisema Mahakama Kuu, katika kutafsiri kifungu cha 25(1) (2) inakiri kwamba kuna tofauti kati ya kifungu kilichoandikwa Kiswahili na kile kilichoandikwa Kiingereza.
Alisema Mahakama Kuu katika hukumu hiyo imesema mamlaka ya kuandika Katiba Mpya ina maana ni mamlaka ya kuandika na kupitisha katiba inayopendekezwa kwa ajili ya kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.
Takukuru yalitesa Bunge
Wakati hayo yakiendelea suala la kuingizwa ama kutoingizwa kwenye katiba, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), linaonekana kulitesa Bunge la Katiba baada ya kamati 10 kati ya 12 kulirejesha tena jana.
Rasimu iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ililiacha suala hilo kwa maelezo kuwa siyo moja ya mambo ya Muungano na msimamo huo ukaungwa mkono na Kamati ya Uandishi ya Bunge hilo.
chanzo mwananchi
ngoja team lumumba waje kwanza nitarudi baadae
Baadhi ya wanasiasa, wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wanaharakati na wanasheria wamekosoa zoezi la upigaji kura katika kupitisha rasimu ya katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba (BMK), wakieleza liligubikwa na hila, kampeni, uchakachuaji, mabavu, vitisho na kwamba, rasimu hiyo haiendani na matakwa ya wananchi wa Zanzibar.
Baadhi wameeleza kuanza kuchambua rasimu hiyo kifungu kwa kifungu ili kupima uzito na tafsiri ya Ibara 28 zilizofutwa kabla ya kuueleza umma namna maoni yao yalivyochakachuliwa.
Wamesema upitishwaji wa rasimu hiyo ulitawaliwa na mabavu na Watanzania siyo wajinga kwa kuwa wanaona kinachoendelea hivyo wataamua.
Halafu kuna wanaojiita wasomi wanaunga mkono hii blanda, kazi tunayo watz.