Ibara 24:1

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
24.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchi
zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya
hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), ni marufuku
kwa mtu yeyote kunyang'anywa mali yake kwa madhumuni ya
kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria
ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili

Je kina Mwanyika walipoenda na kutaka hizi fedha kutoka kwa watuhumiwa wa EPA na kunyang'anya pasi zao na hata magari walifanya hivyo kwa uamuzi wa mahakama gani?
 
Je kina Mwanyika walipoenda na kutaka hizi fedha kutoka kwa watuhumiwa wa EPA na kunyang'anya pasi zao na hata magari walifanya hivyo kwa uamuzi wa mahakama gani?

Yeah Mwanakijiji,

Ila Rais ana mamlaka yapi juu ya katiba?

37.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yali yomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii
au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na
mtu au mamlaka yoyote.

Ibara 24:1 hata hivyo hailindi wezi na wakusema huyu ni mwizi au la ni mahakama pekee
 
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), ni marufuku
kwa mtu yeyote kunyang'anywa mali yake kwa madhumuni ya
kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria
ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili

Je kina Mwanyika walipoenda na kutaka hizi fedha kutoka kwa watuhumiwa wa EPA na kunyang'anya pasi zao na hata magari walifanya hivyo kwa uamuzi wa mahakama gani?

Ili tuweze kujadili hili vizuri bila kupotosha inabidi utupe na sheria husika inayozungumzimwa hapo juu. Bila hivyo tunaweza kwenda katika hukumu ambayo sio sahihi mzee.
 
Yeah Mwanakijiji,

Ila Rais ana mamlaka yapi juu ya katiba?

37.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yali yomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii
au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na
mtu au mamlaka yoyote.

Kwa kutumia mamlaka yake alimtimua BALALI, majukumu mengine aliwaachia akina Mwanyika wachukue hatua.

.
 
Yeah Mwanakijiji,

Ila Rais ana mamlaka yapi juu ya katiba?

37.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yali yomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii
au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na
mtu au mamlaka yoyote.

Nakushukuru kwa hili. Lakini tukumbuke jambo moja huwezi kuisoma katiba yenyewe bila sheria zanazohusika. Kuna vitabu zaidi ya 12 kama sikosei vya sheria ambazo lazima zisomwe kwa pamoja na katiba. La sivyo unakuwa haujakamilisha au kupata linalosemwa na katiba.

MKJJ ambatanisha sheria husika katika hoja yako ili tuone, je sheria waliipindisha au la? Bila hivyo tunacheza
 
Ili tuweze kujadili hili vizuri bila kupotosha inabidi utupe na sheria husika inayozungumzimwa hapo juu. Bila hivyo tunaweza kwenda katika hukumu ambayo sio sahihi mzee.

Katiba ya nchi ambayo iko juu ya sheria zote unazozijua
 
Katiba ya nchi ambayo iko juu ya sheria zote unazozijua

Katiba inasomwa kwa pamoja na sheria za nchi. kote kwenye neno sheria kwenye katiba lazima mtu uisome sheria husika. La sivyo utajuaje hio sheria inasemaje? kumbuka katiba ni pamoja na sheria zake. haiko tupu hivyo...
 
Mzeeba, katiba inaposema sheria husika haina maana sheria hiyo ipo mara moja; yaani Katiba haiakisi uwepo wa sheria kulani bali kimsingi inatoa agizo la kuwepo kwa sheria ya jambo hilo. Sasa ipo sheria ya mambo hayo sikumbuki jina lake;
 
Lakini tayari kwa hilo unalozumgumzia sheria yake ipo. Kwa hiyo kunukuu katiba bila sheria yenyewe inakuwa ngumu mtu kutoa maamuzi kama wakosawa ama la. Najua ugumu wa kuzipata hizi sheria, lakini itakuwa vizuri ikiwepo ili tuweze kuwahukumu kwa haki. La sivyo kifungu cha katiba bila sheria husika hakiwezi kuhukumu mtu
 
The Constitution provides for a bill of rights, notwithstanding the fact that it also makes provision for a number of claw-back clauses. In other words the enjoyment of certain rights and freedoms under the constitution is not absolute, but it is subject to legal regulation.

Kama ulivyoonyesha vizuri...

The Bill of Rights is found in part three of the first Chapter of the Constitution and the fundamental rights and freedom are stipulated in article 12 to 24, article 25 to 28 imposes duties on every individual to duties and obligations to respect the rights of others and society. Article 29 establishes the obligation of society to every individual.

Article 30 of the Constitution limits the application of these rights subject to law and the under the due process of law, as the case may be.

Nadhani ukiisoma hii Ibara ya 30 utaona kwa nini naomba utupe na sheria husika mkuu. Hii sio kusema sioni ukubwa wa hoja yako, hapana. I just want us to get it right
 
Mwanakijiji,kwanza naomba ufafanue,maana quotation yako ya katiba inasema "...bila ya idhini ya sheria....",lakini wewe unauliza iwapo walipewa idhini ya mahakama.Mimi nadhani ndio sababu Raisi alimuweka mwanasheria mkuu ili hatua dhidi ya upotevu wa fedha hizo uwe chini ya uangalizi wa kisheria,sembuse katiba?

Pili,nadhani umemsikia Mh.Spika alivyo wind up hotuba ndefu ya Mr.President kwa kusema hakuna haki za binadamu kwa wabadhirifu wa fedha za umma.Kama motive ya akina Mwanyika ilikua ni kurejesha fedha kwanza,mengine baadae(kama yapo),maadamu mwizi kapatikana,hayo mambo ya kuendekeza woga juu ya mafisadi kwa visingizio na upindishwaji wa sheria na katiba nadhani ndio watu wanapigia kelele kila siku humu JF.

Serikali imekua tooo slow kutake actions dhidi ya mafisadi,na worse enough,japo President anajua ana mamlaka makubwa ambayo hata kama ingekua ni kwa lengo la kuwashugulikia wachache ili wawe fundisho kwa wengine,angeshaonyesha kwa vitendo ile dhamira anayodai kua nayo dhidi ya viongozi wabadhirifu, bado leo amekiri wazi kwamba anaogopa kuja kulipa fidia!

Its so unbelievable kwamba wale wezi wataishia kulipa tu.I still comvince myself kwamba line ya mwisho ya point ya EPA ktk speech ya Rais alisahau kuisoma,iliyoelezea kushtakiwa mara moja kwa wote waliorejesha pesa hizo,maana waligawana kinyume cha sheria.Na kwamba this everning kutakua na breaking news kutoka kwa Rais akitoa maelezo hayo :)

Conclusion:Heri kenda mkononi kuliko kumi nenda rudi.Kwa kuvunja au kutovunja sheria,at least fedha ya EPA itakuja kumfaa mkulima wa kwetu Ng'hungumalwa siku moja.
 
Beautiful.. unapotaka kujenga Taifa la utawala wa sheria basi lazima uwe tayari kutii sheria hizo. Ukikubali kuvunja sheria for the greater good unachofanya ni kufungua mlango wa udikteta. Tatizo langu siyo fedha kurudishwa lakini lazima zirudishwe kwa mchakato wa haki. Kuna kitu kinaitwa Hobeus Corpus ambapo kimsingi ni kuhakikisha kuwa kila mtu anapata nafasi mbele ya mahakama.

Sijui kwa kiasi gani mfumo wetu wa sheria unalo hili.Hatuwezi kuhalalisha uvunjaji wa sheria kwa sababu tuna nia nzuri.
 
Back
Top Bottom