Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,484
24.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchi
zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya
hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), ni marufuku
kwa mtu yeyote kunyang'anywa mali yake kwa madhumuni ya
kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria
ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili
Je kina Mwanyika walipoenda na kutaka hizi fedha kutoka kwa watuhumiwa wa EPA na kunyang'anya pasi zao na hata magari walifanya hivyo kwa uamuzi wa mahakama gani?