IBARA 182 RASIMU YA KATIBA Tume Huru ya Uchaguzi 2015

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
549
Kamati ya
Uteuzi
182.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Uteuzi wa Mwenyekiti,
Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi
itakayokuwa na muundo ufuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa ni
Mwenyekiti;
(b) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambaye
atakuwa Makamu Mwenyekiti;
(c) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar;
(d) Spika wa Bunge la Tanzania Bara;
(e) Jaji Mkuu wa Tanzania Bara;
(f) Jaji Mkuu wa Zanzibar; na
(g) Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu.
(2) Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi atakuwa Katibu wa

Kwa matakwa hayo 2015 hapatakuwepo na tume huru ya uchaguzi
 
Kwa muda mrefu nilikuwa sielewi vizuri suala linalotajwa sana na viongozi wa upinzani kuhusu uwepo wa tume huru ya uchaguzi Tanzania. Lakini baada ya kutokutajwa kwa uchaguzi kwa Kata ya DARAJA MBILI sasa ndio nimeelewa somo hilo vizuri. Iko wazi kabisa kuwa Diwani Mawazo aliamua kujitoa CCM na kwenda Chadema na hivyo kulingana na sheria ya uchaguzi anakuwa amejivua nafasi yake ya Udiwani na Kata kubaki bila mwakilishi. Imetokea hivyo kule Mbulu kama sijakosea kwa Diwani aliyekuwa NCCR Mageuzi kwa jina la Tara kuhamia Chadema ambapo katika chaguzi zilizofanyika jumamosi, Kata hiyo imepata mwakilishi. Sasa hapa naomba Chadema hasa Mwenyekiti kwa nafasi aliyonayo bungeni kumuuliza Waziri Mkuu maswali ya papo kwa hapo, tupate majibu ya kina, ni sababu gani zilizozuia kata hii isifanye uchaguzi na kupata mwakilishi wa kutetea matatizo na maendeleo yake?
 
Back
Top Bottom