Ibada ya ijumaa kuu: Maaskofu katoliki wakazia waraka wao hasa sehemu inayozungumzia siasa za nchi

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Leo kama tunavyojua ni Ijumaa kuu ya kumbukumbu la Yesu Kristo kukamatwa, kuteswa na hatimaye kufa msalabani kwa makosa ya kubambikiwa japo tunajua alikuwa anajua kitakachomtokea toka alipoianza kuhubiri habari njema kwa watu wote
Leo nimeifuatilia ibada kupitia Radio Maria na walikuwa wakirusha ibada ya mojakwamoja kutoka jimbo la iringa iliyokuwa ikiongozwa na baba Askofu tarikisius ngalalekumtwa ambaye pia ni rais wa baraza la maaskofu Tanzania
Lakini pia nimefuatililia Radio tbc taifa pia ibada nyingine ilikuwa ikiendelea
Na msisitizo wao mkuu ulikuwa ni ujumbe walioutoa wakati mfungo wa kwaresma ukiendelea huku wakisisitiza eneo linalozungumzia siasa za nchi yetu huku wakiwataka wananchi kujiandaa na uchaguzi ujao kupata viongozi watakaojali Haki, Amani , demokrasia Utu na maendeleo kwa wakati mmoja huku wakiwataka wananchi kuacha kuchagua chama kwa kuwa wanapochagua chama bila kuangalia mtu mwenye sifa za Haki Amani, demokrasia Utu na maendeleo basi wataishia kuumia na kulalamika kila baada ya uchaguzi unapomalizika huku wakisema malalamiko ya watu kila baada ya uchaguzi kuisha ni dalili ya kuchagua viongozi kichama zaidi badala ya kuangaia taifa kiujumla

Chanzo radio maria na tbc taifa leo katika ibada kuu za ijumaa kuu

Hayo ni kwa uchache tu niliyoyanasa katika ibada za ijumaa kuu leo jioni
 
Hii ni habari mbaya kwa waishio Lumumba,
 
Niwaombe tuu maaAskofu muhubiri ujenzi wa viwanda vya dawa tunapoteza hela nyingi sana za watanzania maskini wanaolipa Kofi kununua madawa.
 
Back
Top Bottom